Majibu ya Kikwete na BBC: Tumevuna tulichokipanda | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Majibu ya Kikwete na BBC: Tumevuna tulichokipanda

Discussion in 'Great Thinkers' started by Rev. Kishoka, Jul 22, 2011.

 1. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #1
  Jul 22, 2011
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Nikirejea mahojino kati ya Rais Kikwete na mwandishi wa BBC majuzi kuhusiana nasuala la umeme, hisia kadhaa zinakuja akilini mwangu, masikitiko, kicheko na hasira!

  Kama nilitarajia majibu yenye kuleta maana, basi nilikosea sana, lakini sikutegemea kuona majibu yaliyokosa busara na umakini na zaidi uungwana wa kukiri kuwa kuna makosa katika mipango na utekelezaji wa kazi katika uongozi wa ais Kikwete.

  Ingekuwa rahisi sana kwa Kikwete kupokelewa kwa kusamehewa kama angekiri wazi kuwa Serikali yake ilifanya makosa katika mipango hii ya kuzalisha umeme na angejibebesha msalaba mzima na kusema tumeanza kazi mpya na tutaliangalia kwa upya kwa kasi, basi tungemuelewa.

  Lakini Rais kajibu kwa ghadhabu, kiburi, kejeli na masikhara. Zaidi anawabeza wale wanaohoji kwa nini bado tunaendelea na tatizo hilo.
  Cha kusikitisha ni Rais kulaumu mvua na ukame na hata kudai Serikali haiwezi kuleta mvua. Swali langu kwa Rais KIkwete, leo hii ambapo inafahamika wazi dunia nzima kuwa kuna mizunguko ya hali ya hewa ambayo imevurugika, somo la njaa na ukame wa mwaka 1974, 1984, 1994 na hata miaka ya 2000, halijaingia katika akili za watawala au mtawala wetu?

  Yeye si Mchumi, je wachumi si watu wanaobobea katika takwimu na mipango? Je alishindwa vipi kuling'amua hili hata pale alipokuwa Waziri katika wizara ya Maji na Nishati kwa miaka 6? Je si yeye au katika uongozi wake ndipo Tanzania iliingia mkataba na IPTL hata kama alikwisha hama Nishati, lakini si alikuwa Hazina alipoidhinisha fedha?

  Leo anapojitapa na kujisifia kuzalisha umeme wa megawati 300 kwa kipindi cha miaka minne, je umeme huo uko wapi leo hii ikiwa tunaambiwa hakuna mafuta na gesi ya kutosha na mitambo mingine ni mibovu? Je atatuambia nini ilhali inafahamika wazi kuwa hizo megawati 300 zimanuka harufu ya rushwa na hujuma kama Dowans?

  Anapodai kuwa mitambo ya kuzalisha umeme haijengwi siku moja, je kasahau kilio cha Mchungaji mwaka 2006 alipoomba Rais akutane na GE akienda Marekani kwa swahiba wake George Bush?

  Kama yeye ni kiongozi makini, je tatizo hili la umeme kalivalia njuga gani? Mbona Kenya wamejenga mfumo wa umeme wa Upepo kwa miaka mitatu bila kutokwa jasho au kusubiri upungufu wa maji na ukame waanze kuhaha kutafuta miradi uchwara ya kuzalisha umeme?

  Kama yeye ni kiongozi fanisi, je mbona hajatumia ile methali ya kinga ni bora kuliko tiba kwa kuwa mstari wa mbele kuagiza hiyo mitambo ambayo haiuzwi kama shati la mtumba?

  Rais Kikwete ametudhihaki Watanzania na kukishusha hadhi cheo na dhamana aliyopewa. Na zaidi, ameonyesha wazi dharau yake pale alipoamua kumuonyesha dharau ya wazi Mbunge Mnyika na kumfanya aonekane ni mwendawazimu ilhali ni viongozi wake na uongozi wake uliojaa ahadi za uongo, uvivu na ukosefu wa umakini katika kufanya kazi.

  Lakini, sitaendelea kumchutumu sana, maana niliiona hili la uongozi wa kizembe tangu awali.

  Majibu aliyotoa yanaonyesha ni Kiongozi asiyejali lolote linalotokea ndani ya nchi, haelewi kwa nini Tanzania ni masikini, anawabembeleza wahalifu wajisalimishe, uchumi unadidimia lakini yupo tayari kuzitumbua fedha zaidi kwa safari, semina na vikao vya kufundishana kazi na kuvuana magamba huku akilalamika na si kuonyesha ushupavu an umadhubuti wa kuwa Rais na hata mwenyekiti wa Chama chake CCM.

  Watanzania tumevuna tulichokipanda! Wala tusiwalaumu CCM pekee yaom bali ni sisi sote kama Taifa kwa kukubali kwa umoja iwe ni kupitia kura zetu za ndiyo au hapana, au hata kuendelea kutazama uongozi huu wa awamu ya nne ukijiendeaa tuu kama jongoo au konokono bila kuelewa ni wapi dira inasema tuelekee.

  Tumelelea mfumo mbovu wa watu kutokuwajibika, na haya ni matunda ya watu wasiowajibika au hata kuogopa kuwa wana wajibu wa kuwajibika kwa dhamana na kazi walizopewa.

  Haijali ni nani atakuwa Rais wetu 2016, lakini kwa mwendo huu wa uongozi huu tuliouona na watu ndani ya chama cha CCM na hata Serikalini watu wanakubali kuburuzwa na kiongozi asiye makini na mwenye silika za uzembe na masikhara kama haya, basi safari yetu ni ndefu mno.

  Ili kuelewa kuwa tunaongozwa na mtu asiyethamini dhamana aliyopewa, tafakari vicheko vya dharau au masikhara alivyofanya wakati akiulizwa maswali ya msingi kuhusu tatizo hili la ukame.
  Ama kweli Tanzania ni kichwa cha Mwendawazimu!
   
 2. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #2
  Jul 22, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  Wengine tuliwaambia ile mwaka 2005 lakini mkatuona ni watu wa ajabu.
   
 3. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #3
  Jul 22, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 17,972
  Likes Received: 726
  Trophy Points: 280
  Kweli kabisa,sioni vision yoyote.
   
 4. Zing

  Zing JF-Expert Member

  #4
  Jul 22, 2011
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 1,780
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Hivi Rais wetu ni mchumi kweli?

  Mi nadhani mambo ya JWTZ kile cheo cha Kanali vili delete mpaka kwenye recycle bin anything to do with uchumi kwenye "RAM" yake.
   
 5. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #5
  Jul 22, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,762
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Lakini inawezekana ni kweli kuwa yeye siye mvua but kwa uwezo wake wa kuelewa!
   
 6. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #6
  Jul 22, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  mmh, lakini si handsome jamani?
   
 7. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #7
  Jul 22, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,762
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  sasa kama huo uhandsome ni mali sana alete umeme! Au tumweke kwenye box asiishe!
   
 8. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #8
  Jul 22, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Nikimwangaliaga huyu Mkwer.e kwenye TV naishia kucheka tu! Nadhani mnajua sababu.
   
 9. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #9
  Jul 22, 2011
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,571
  Likes Received: 4,688
  Trophy Points: 280
  Mkuu Rev. Kishoka, kutarajia busara na umakini kutoka kwa huyu mcheza kiduku ni sawa kutegemea guta libebe 40 feet container lililojaa mzigo wa vyuma. Watanzania tukubali kuwa nchi hii haina rais, kuna sharobaro anajiita rais tu.
   
 10. Magulumangu

  Magulumangu JF-Expert Member

  #10
  Jul 22, 2011
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 3,040
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135

  Mkulu alikuwa anarap au maana sikuelewa alichokuwa anaongea mie...kila kitu unajua sisi, unajua sisi, wewe nani? Rais hatuna tena hatuna na hatuna.....
   
 11. Magulumangu

  Magulumangu JF-Expert Member

  #11
  Jul 22, 2011
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 3,040
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  wewe mkuu mpaka umuone kwa TV? mie nikiona tu jina Kikwete du naanza kucheka sana, sometimes hata nikiona tu herufi mbili za mwanzo Ki...tayari kicheko hicho
   
 12. Magulumangu

  Magulumangu JF-Expert Member

  #12
  Jul 22, 2011
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 3,040
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  ana ROM tu huyu mkuu hiyo RAM aitoe wapi?
   
 13. Mentor

  Mentor JF-Expert Member

  #13
  Jul 22, 2011
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 18,658
  Likes Received: 8,211
  Trophy Points: 280
  Nalia..pole.
  Nalia..pole sana!
   
 14. Mzalendo80

  Mzalendo80 JF-Expert Member

  #14
  Jul 22, 2011
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,385
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Si bora wewe unacheka mimi nashikwa na Hasira natamani nimrukie na kuanza kumchapa Makonde. Kwanza hata kwenye hii Post nimeshikwa na hasira Juzi niliona gazeti lina picha yake nikalichoma moto jinsi nisivyompenda kwa ajili ya kuliagamiza Taifa langu. Aaggghhhhh anatia Kinyaa ni bora ukanyage mavi kuliko kuiona picha yake
   
 15. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #15
  Jul 22, 2011
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,552
  Likes Received: 1,899
  Trophy Points: 280
  Madhara ya kuwachagua viongozi waliomwamgusha mwalimu ndo haya.Hii kauli ya kejeli si mpya kwa viongozi waliomrithi mwalimu.Ni kauli zilizokuwa zikitolewa na viongozi hao toka wakiwa mawaziri.Hata Christian Kisanji alishawahi kutoa kauli kama hizi kipindi alipokuwa waziri wa maji chini ya Mwinyi.Nilikuwepo huko Same Sekondari na ziara ya waziri huyo tuliisubiria tukidhani itakuwa ya matumaini kwa kusikilizwa vilio vyetu vya ukame wa maji wa kupindukia na kuja na solutions.

  Nakubaliana na ukweli kwamba tunavuna tulichopanda.Sioni vongozi kabisa.

  Kwa upande mwingine,nimesoma mahojiano na BBC nimechoka.Tofauti na wengineo,kwangu ni vigumu kuamini kwamba hizo ni kauli za viongozi waliopewa dhamana.Siamini kabisa kuwa Tanzania haina watu wenye kufikiri beyond this.Wenye kuweza kutufanikisha hawapewi nafasi.Na ukiangalia,wananchi milioni 40 wanachaguliwa viongoz/Kiongozi na wananchi milioni 4 tu,yani ten pasenti ya wananchi wanawatuvunisha milioni arobaini haya makapi.
   
 16. Mo-TOWN

  Mo-TOWN JF-Expert Member

  #16
  Jul 22, 2011
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,626
  Likes Received: 138
  Trophy Points: 160
  Pole mkuu wengi tumesikitika sana kwa ile interview...it was a terrible one...arrogance, incompetence, disregard for people who are suffering because of power shortage...you name it...he simply showed the world that he as president of the country had no idea of the consequence of power shortage to economy of TZ..
   
 17. n

  ngokowalwa Senior Member

  #17
  Jul 22, 2011
  Joined: Jul 22, 2011
  Messages: 155
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mkuu usichoke kusema mwisho wake utaeleweka na wengi
   
 18. F

  Froida JF-Expert Member

  #18
  Jul 22, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Kikwete ni Zigo tulijadili sana kwenye thread alianzisha Pasco hapa tutalibeba lakini likizidi uzito tutalibwaga ,KIKWETE ni disaster Dunami bin sunami maafa zaidi yaja unaona serikali ilivyofilisika
   
 19. Janjaweed

  Janjaweed JF-Expert Member

  #19
  Jul 22, 2011
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 9,528
  Likes Received: 882
  Trophy Points: 280
  Mimi nikikwangalia JK najihisi kama namwangalia mama yangu mzazi akiwa uchi........... he is an insult to say the least
   
 20. yutong

  yutong JF-Expert Member

  #20
  Jul 22, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 1,604
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  amini kichwa chako, usiamini moyo wako
   
Loading...