Majibu ya Kikwete na BBC: Tumevuna tulichokipanda

FaizaFoxy;2274623]Kitu ambacho nadhani unashindwa kukikubali ni kuwa, Kikwete kafanya mengi ya maana kwenye suala la umeme.
Alipochukua nchi kakumbana na mambo mengi sana, na kwa kibajeti chetu finyu afanye mangapi kwa pamoja?
Kama JMK kafanya mengi ya maana kwa maana ya maana, basi Nyerere atakuwa amefanya ya maajabu. Ni kutoka ukoloni tukiwa na Pangani tu, na Kibajeti finyu aliwekeza katika umeme kuliko mwingine yoyote aliyefuata. Kibajeti finyu aliacha vyanzo ambavyo vilimsaidia JK akiwa mwanafunzi hadi kuwa Rais. JMK amewekeza wapi kwa maana ya kuwekeza. Jenereta Nyerere alinunua tuna ushahidi(mpango wa maendeleo 1963).
Katika priorities alizokuwa nazo, hili la umeme lipo na hajalisahau, utakumbuka kwamba, alipochukua urais nchi ilikuwa kizani. Akafanya haraka haraka iletwe mitambo ya emergency, matokeo tunayajua, na kwa bahati nzuri zikanyeesha mvua nzuri sana tukawa hatuna haja hata ya kuiwasha hiyo mitambo
Akiichukua nchi alikuwa ndani ya serikali kwa miaka zaidi ya 20 kama waziri wa fedha, Nishati na Mambo ya nje, zote zikiwa wizara zenye uhusiano na nishati kama resource, policy maker au katika contract kama za IPTL.Hana excuse yoyote.
Matokeo hatuyajui kwasababu hatukuona umeme, ni matokeo gani mazuri yaliyotokana na mitambo ya emergency?
Ukame ule alioukuta Kikwete uliambatana na njaa kali sana, Kikwete akasema hafi mtu hapa. Akafanya kila njia na kweli hakufa mtu kwa njaa ile. Bahati nzuri sana mvua ile iliyojaza mabwawa ya hifadhi kwa ajili ya umeme, ilitusaidia kwa miaka minne mfululizo, na kina cha maji kilikuwa kizuri tu, sasa fedha inayohitajika sana sehemu zingine, ikaanza kutumika huko, kwenye mashule, mabarabara, ma university na mitambo ya umeme iliyokuwepo Ubungo ilionekana kuwa itatosha kabisa kama kuna tatizo
Nakumbuka wilaya ya Ulanga na Kilombero kuna ma DC walipoteza kazi kwa kuficha ukweli wa njaa katika wilaya zao, Lowassa atakuwa shahidi wangu. Kwa nchi kama Tanzania kujua watu waliokufa kwa njaa sio jambo la kuaminika hata kidogo. Hanang walipelekewa chakula wakati fulani baada ya BBC kutangaza, sasa serikali hiyo itawezaje kusema hakufa mtu tukaamini.
Njaa inaweza kuua kwa njia mbili. 1) Haraka kwa kukosa mlo 2) kwa matokeo ya muda mrefu. Kukiwa na njaa watoto wataathirika kwa marasmus na Kwashiokor, ikitokea maradhi kama surua au kuhara basi huharakisha vifo vyao. Ingawa atakuwa amefariki kwa surua, lakini kitaalamu inasemwa amefariki kwa complication of measles as a results of severe malnutrition, hapa unaona njaa inavyoua in long term. Kusema hakufa mtu you need more than just saying it.
Kilichotokea baada ya hapo ni wimbi la wawekezaji, wimbi la matumizi ya umeme yasio ya kawaida na umeme ukawa unahitajika na unaongezeka kwa 14% kila mwaka. Kikwete akaagiza mitambo kama mahitaji ya maongezeko, ghafla tumekumbwa na ukame, mitambo ambayo iliagizwa ku cover ongezeko la kawaida la kila mwaka ndio inatumika kujaziliz umeme ambao haufuliwi kwa ajili ya kupungua vina vya maji kwenye mabwawa. Hapo jamani ni nani wa kumlaumu? ingekuwa hajafanya kweli, mimi ningekuwa wa kwanza kumlaumu.
Wawekezaji wa kichina pale kariakoo hawawezi kuleta ongezeko lolote la maana katika nishati. Wawekezeji wote wakubwa katika sekta ya madini inayotumia umeme mwingi waliingia wakati wa Mkapa. Kama yupo mwekezaji waliyeletwa na JMK tufahamishwe.
Ni JMK alikuwa waziri wa mambo ya nje kwa miaka 10, ongezeko la wawekezaji alipaswa alijue kwasababu mikataba yote alishiriki 100%. Kama angechanganya na maarifa ya uwaziri wa nishati hili lisingekuwa tatizo, kusema ukame ni kisingizio cha kushindwa kutumia maarifa na ulaghai wa mikataba ya nishati ambayo yote ina mikono yake. Lakini JMK anajua tatizo la mabwawa ya umeme au ana hisi? ni huyu alituambia tatizo ni mtera kujaa matope, na wafugaji bonde la usangu, sasa ukame je anajua tatizo hasa!!
Kumbukeni kuna sababu ambazo zinakuwa nje ya uwezo wa yeyote awaye, lakini kizuri ni kwamba Kikweye hata kwa hilo hajasema hapana hapa ndio mwisho, kawekeza kwenye mkaa wa mawe, kawekeza kwenye upepo na sasa anahuisha umeme wa steigler.
Haya yote yana play book, hakuna mradi hata mmoja kati ya uliyotaja unaotokana na ubunifu wa serikali ya JMK, in fact alipaswa kufanya haya akiwa waziri wa fedha, nishati na mambo ya nje.
Data zinaonesha average yake ya kuwekeza kwenye umeme kwa mwaka ni way above wote waliomtangulia. Wakati wenzake waliwekeza wastani wa 7.5MW kwa mwaka yeye anawekeza 50MW kwa mwaka, hilo nii kubwa sana na kasema itaongezeka kufikia uwiano wa 200MW kwa mwaka kabla ya kumaliza muda wake. Its a big achievement uki compare na wote waliopita. Na vilevile akabadilisha sheria ya monopoly kwenye umeme ili wafuaji binafi waweze kuwekeza na matokeo tunayaona
Amejenga vyanzo vingapi katika national level. Amewekeza 50MW wapi? kama ni ununuzi wa jenereta je hiyo ni renewable energy source and is it sustainable. Hebu tuambie ziko wapi ambazo tutasema hizi ni za JMK hakutumia ubunifu wa mtu mwingine.
 
Maggid,

..wa-Tanzania wamechoka kusikiliza ahadi, michanganuo, maelezo ya juhudi zilizofanyika, etc etc.

..wa-Tanzania wanataka umeme. PERIOD.

..Raisi alipoingia madarakani miaka 6 iliyopita alilikuta tatizo hili, na mpaka leo ameshindwa kulitatua.

..wa-Tanzania wa leo wanataka RESULTS, they have no time kukusikiliza na porojo za juhudi na mipango.

Shauri zako FaizaFoxy akikusikia....utakiona cha ntema kuni!
 
Hivi toka 2005 hadi leo hii tumetumia kiasi gani kwenye kugharimia umeme wa dharura?
Awali ya yote nakiri kuwa sina data za uhakika kuhusu gharama halisi.
Pili inaniwia vigumu kujua gharama halisi kwa sababu kuna 'direct and indirect cost'.
Tatu kuna vimiradi vingi vingine tumekuwa tunalipia capacity charges tusizozijua.

Direct cost ni zile zinazotumika kununua mitambo, na indirect cost ni kama zile zitokanazo na procedure. mfano tulikaa miezi 10 tukisubiri umeme wa Richmond ambao haukuwepo na kwa muda huo tuliathirika kiuchumi, gharama za uratibu, vikao na taratibu zingine.

Kuna capacity charges tulikuwa nazo tangu enzi na tuliendelea nazo kuanzia hiyo 2005 kama IPTL. Halafu kukawa na vimalipo kwa akina Songas, Aggreko n.k.

Anyway, ni mchango tu mwenye data atusaidie kwa kuanglia 'in broad spectrum'
 
Nguruvi, I know the answer but I just want people to think for a second.. kwamba TUKO TAYARI KUTUMIA FEDHA NYINGI KUFANYA KITU KIDOGO, KULIKO KUTUMIA FEDHA KIDOGO KUFANYA KITU KIKUBWA, AU FEDHA NYINGI KUFANYA KITU KIKUBWA ZAIDI. Kwa ufupi, kiasi tulichogharimia umeme wa dharura, majenereta, mafuta na vikolombwezo vingine vyote kuweza kuzalisha 300MW alizozifia JK kingeweeza kujenga Stielger's Gorge Dam mara 3!! kuzalisha over 2000MW..

Go figure.
 
Nguruvi, I know the answer but I just want people to think for a second.. kwamba TUKO TAYARI KUTUMIA FEDHA NYINGI KUFANYA KITU KIDOGO, KULIKO KUTUMIA FEDHA KIDOGO KUFANYA KITU KIKUBWA, AU FEDHA NYINGI KUFANYA KITU KIKUBWA ZAIDI. Kwa ufupi, kiasi tulichogharimia umeme wa dharura, majenereta, mafuta na vikolombwezo vingine vyote kuweza kuzalisha 300MW alizozifia JK kingeweeza kujenga Stielger's Gorge Dam mara 3!! kuzalisha over 2000MW..

Go figure.

You are definately going to make FF so mad and angry at you and all of us...yaani unamgambira JK is s....
 
IPTL inazalisha umeme kutumia maji? unanchekesha! labda maji rejeta ya kupoozea engine.

Sikukusudia kusema mitambo ya IPTL inatumia maji, maana yangu ni kwamba ukame haukuanza hivi karibuni hata wakati wanajenga IPTL walishaona kabisa kwamba hali ya mvua sio nzuri ndo maana wakaopt mradi wa kutumia mafuta ingawa na wenyewe uligubikwa na rushwa lakini idea ilikuwa ni nzuri, sasa swali kama waliweza kujenga IPTL kwa nini anticipation hiyo hiyo isingetumika kujenga miradi mingine mikubwa kwa kuzingatia vyanzo vilivyopo vimezidiwa na hali ya mvua si nzuri hadi wamesubiri 2007 halafu mheshimiwa anasema tatizo lilisasabishwa na ukame na wewe bila aibu unatetea na kusifia kafanya kazi kubwa?
 
Hivi toka 2005 hadi leo hii tumetumia kiasi gani kwenye kugharimia umeme wa dharura?
Labda kwa kuanzia tu bofya HAPA. Hii ndio miradi ya Jk ktk kupunguza matatizo ya umeme ambayo yameongezeka. IPTL nayo sijui inategemea matakwa ya Mungu, na kama kawaida yao wazalishe wasizalishe - Wanalipwa!
 
Nguruvi, I know the answer but I just want people to think for a second.. kwamba TUKO TAYARI KUTUMIA FEDHA NYINGI KUFANYA KITU KIDOGO, KULIKO KUTUMIA FEDHA KIDOGO KUFANYA KITU KIKUBWA, AU FEDHA NYINGI KUFANYA KITU KIKUBWA ZAIDI. Kwa ufupi, kiasi tulichogharimia umeme wa dharura, majenereta, mafuta na vikolombwezo vingine vyote kuweza kuzalisha 300MW alizozifia JK kingeweeza kujenga Stielger's Gorge Dam mara 3!! kuzalisha over 2000MW.. Go figure.
Inafikirisha sana, na tungeelewa endapo basi hicho kidogo kinaonekana. Richmond haina udogo wa kipimo chochote. Mtu akifanya utafiti mzuri utakuta nusu ya pesa hizo zipo kwenye account Jersey Island au Uswisi, siku hizi wananunua assets south Africa.

Stiegler ukienda kwenye maktaba za chuo kikuu ni mradi uliokuwa na study kuanzia wakati wa jerumani kama kumbu kumbu zipo sawa.
Walishiondwa kuendeleza kama Nyerere wanacho cha mbadala kuonyesha, najiuliza waliofuata walifanya nini?

Hivi unafungaje safari kwenda kumualika mwekezaji ukiwa huna reliable source za energy! kuna mwekezaji gani atakuja kuwekeza kwanza ili asubiri umeme wa Ngeleja wa mwaka 2015. Ngonjera, maagizio, ngano na ushairi vinatubakiza tukiitikia bila vibwagizo mahususi. Kibwagizo cha sasa ni ukame pengine mwaka kesho ni matope, na unaofuata ni miundo mbinu mibovu.

Watanzania nasi tunasehemu yetu ya lawama, pesa kama za umeme wa dharura ambazo hata kwa uchache zingeweza kujenga stigler moja, tutaridhika tu bila kupaza sauti. Sana sana tutashangilia jinsi jiji linavyopendeza kwa villa na mansions bila kujua ni kodi zetu.

Nilishangaa katika nchi mmoja kuna mradi ulipangiwa milion $73,890. Kwa sababu zisizoelezeka gharama zikafikia 74,645. Kilichofuata ni watu kupukutishwa kazi na wengine kupanda kizimbani. Wengine wakafutiwa usajili na bodi za ujenzi na ukandarasi. Na ni wazi waliohusika hawatapata kazi tena katika serikali au shirika lolote kutokana na record zao chafu. Nani atazembea next time !!!

Sasa hata matumizi ya pesa zetu yanaidhinishwa kwa hongo,sijui taasisi husika zitarudishaje hizo milion 50@.
 
Hii mada ingelisomeka: Majibu ya Kikwete na BBC: Tumevuna tulichoandikiziwa.
"No comments Mkuu!"
 
Mahakama yamwachia Gire wa Richmond
Send to a friend


Thursday, 28 July 2011 21:32
0diggsdigg

Nora Damian
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuachia huru mfanyabiashara Naeem Gire aliyekuwa anakabiliwa na kesi ya kughushi na kutoa taarifa za uongo kuhusu kampuni ya Richmond. Uamuzi huo ulitolewa jana na Hakimu Mkazi Wariyalwande Lema aliyekuwa anasikiliza kesi hiyo. Hakimu Lema alisema upande wa mashtaka umeshindwa kuthibitisha kesi dhidi ya mashtaka waliyomshtaki nayo Gire.
Alisema ushahidi wa upande wa mashtaka ulikuwa ni dhahifu na kwamba usingeweza kumfanya mshtakiwa huyo ajitetee. "Naiondoa kesi hii chini ya kifungu namba 230 cha Mwenendo wa Makosa ya Jinai kwasababu upande wa mashtaka umeshindwa kuthibitisha mashtaka dhidi ya mshtakiwa,"alisema Hakimu Lema.

Hakimu Lema alisema hakuna sehemu yoyote ambayo mshtakiwa huyo aligushi na kwamba vitu vyote vilifanywa na Mohamed Gire ambaye ni kaka wa mfanyabiashara huyo.

Baada ya uamuzi huo, upande wa mashtaka kupitia kwa Wakili wa Serikali, Shadrack Kimaro ulisema utakata rufaa kupinga hukumu hiyo. "Tunaomba tupewe nakala ya mwenendo wa kesi na nakala ya hukumu kwa ajili ya kwenda ngazi za juu zaidi,"alisema Kimaro.
Gire alikuwa akidaiwa kuwa, Juni, 2006 jijini Dar es Salaam alitoa taarifa za uongo kwa wajumbe wa timu ya majadiliano ya Serikali, kuwa Kampuni ya Richmond LLC ya Texas, Marekani, ina uwezo wa kuzalisha umeme ili apewe zabuni.

Mfanyabiashara huyo pia alikuwa akidaiwa kuwasilisha hati ya nguvu ya kisheria iliyotolewa Machi 3, 2006 ikimuonesha kuwa aliruhusiwa na Mwenyekiti wa kampuni hiyo, Hemed Gire ambaye ni kaka yake kufanya kazi za kampuni hiyo hapa nchini. Mwisho.

My take:
Tunakumbuka sula la Richmond lilizuiliwa kuongelewa kwasababu lipo mhakamani. Huko halikuwa suala la mitambo bali kusema uongo.
Likazuiliwa bungeni na mitaani.Wengine tulifahamu ulikuwa usanii kwa kutumia sheria ili kuzima mijadala.

Mtakumbuka ubenea wa Mwanahalisi aliporudi kutoka India alisema atataja wahusika. Ghafla wakakamatwa wapiga debe mwananyamala na kufikishwa mahakani ili kuzui mjadla wowote. Baada ya muda wakaachiwa huru kama Gire alivyoachiwa. Mnakumbuka wakati wa sakata la mengi na akina Manji na Rostam, mjadala ulipopamba moto wakakimbilia mahakamani na kuzuia.

Ninachosema hapa ni kuwa udanganyifu kwa wananchi ndio njia ya kututawala na hili watawala wamefanikiwa.
Swali ni je, hili la Richmond ambalo sasa hakuna kesi tutaweza kumhoji JMK kwenye mikuatano ya waandishi wa habari? (hajafanya tangu Richmond iibuke)
Je bunge lipo huru sasa kulijadili tena?
Je hiki ndicho wananchi wa Tanzania walitarajia juu ya udhalimu mkubwa unaolipelekea taifa kwenye giza?
Je huu ndio uwekezaji wa JMK katika nishati?
kwa mwendo huu tutaweza kutatua tatizo la nishati?
Je si kweli Richmond ina mikono mikubwa iliyojaa uchafu unaolihujumu taifa kwa sasa!!

 
Back
Top Bottom