Naendelea kushangazwa na hoja zako juu ya uamuzi wa CCM wa kusimamia Ilani yake ya Uchaguzi. Lakini baada ya kusoma tamko lako la mwisho NIMEGUNDUA UELISHWA TANGO PORI JUU YA NINI KILITOKEA MWANZA, HIVYO SI KOSA LAKO SANA JAPO KAMA KIONGOZI KUWA MAKINI NA UNACHOLISHWA, ULINDE HESHIMA YAKO.
Ref thread ya TAMKO la CHADEMA: KAULI ya CHADEMA juu ya watumishi wa umma kutoa taarifa katika mikutano ya CCM
Katika andiko lako umekiri SI KOSA KUWAITA WATEULIWA WA KISIASA NA KUWATAKA KUELEZEA UTEKELEZAJI WA ILANI YA UCHAGUZI!!! Sasa hebu niambie ni wapi tumewaita watendaji ambao sio wateuliwa wa kisiasa? Kwasababu hata hiyo hoja ya Mwanza aliyeitwa kwenye ule mkutano ni Mkuu wa Wilaya Ndg. Konisaga, yeye Mkuu wa wilaya ambaye kwa mujibu wa sheria ulizozielezea kabla ana mamlaka ya kutaka taarifa kutoka kwa watendaji anaowasimamia wakati wowote aliamua yeye kwa mamlaka aliyo nayo kuja kwenye kikao na wasaidizi wake...jambo la kawaida sana na jema hasa mnapojadili mambo ya maendeleo ya watu. Kwenye kile kikao wakati yeye ana ripoti akasema kuna tatizo kubwa la maji, barabara na umeme kwenye eneo lake analosimamia na bahati mbaya watendaji wa maeneo hayo aliwaita waje kusikia(KUSIKIA) WENYE ILANI WANASEMAJE JUU YA MALALAMIKO YA WANANCHI KWENYE MAENEO HAYO HAWAKUJA.
Sasa la kwanza hawa watendaji hawakuitwa na CCM waliitwa na Mkuu wa wilaya kwa barua rasmi za kiofisi toka kwa DC. CCM ilimwita Mkuu wa wilaya, ambae licha ya kuwa kada wake, ni mjumbe wa vikao halali vya CCM na anawajibu wa kuwasilisha utekelezaji wa ilani kwenye vikao vya CCM. Tens CCM ilimwita DC kwa barua rasmi kama DC. CCM haikumwita Meneja wa Tanroads wala Tanesco.
Isipokuwa baada ya DC kutoa taarifa ya kukaidi kwa hawa mameneja nikasema tena kwa ukali si sawa HAWA NI WATUMISHI WA UMMA, KWAO KUITWA TENA NA BOS WAO KWENDA KUELEZEA UTEKELEZAJI WA MAENEO YAO YA KAZI SI KWA CHAMA TU HATA KWA WANANCHI WA KAWAIDA KABISA NI SEHEMU YA WAJIBU WAO. NDIO NAMNA BORA YA WATUMISHI WA UMMA KUWAJIBIKA KWA UMMA...MNAPOSEMA NGUVU YA UMMA HUKU MKIPUUZA UMMA NI UNAFIKI UNAONUKA.
Ndio maana hata mikoani kote tulipotaka maelezo ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi tuliwabana MAWAZIRI, MA RC, MA DC, WABUNGE NA MADIWANI NA SI ZAIDI YA HAPO... SASA UKIMBANA WAZIRI CHINI YAKE YUPO MKURUGENZI AU RAS NK WAKIBANANA WAO HILO HALITUHUSU SISI... SISI TUNASHUGHULIKA NA HUYU WA KWETU BASI.
SASA SEMA NA HAWA NI KOSA SISI KUWABANA JUU YA UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU YAO.
##########
MAJIBU ya Mhe. John Mnyika:

Nape,
Walatini wanamsemo ambao kwa kiswahili rahisi humaanisha maandiko hubaki, mlichokifanya Mwanza wewe na viongozi wengine wa chama chako kiliandikwa, mfano: CCM yabuni mbinu mpya kwa hiyo unataka kusema kwamba magazeti yaliwasilisha maneno? Na sio magazeti tu, baadhi ya vituo vya televisheni vilirusha, na hayakuwa maneno yako pekee siku ile, weka hapa mkanda wa wote mliozungumza siku ile na umma wenyewe utaweza kupima ukweli ni upi.
Nashukuru kwamba maelezo yako yanamaanisha kwamba umeanza sasa kutambua kwamba CCM haina mamlaka ya kuwaita wakurugenzi na maafisa wa Halmashauri, wakurugenzi na wafanyakazi wa mashirika ya umma kuja kujieleza na kutoa taarifa kwenye vikao vya CCM. Kwa maelezo yako umethibitisha usahihi wa nilichokisema hapa: JOHN MNYIKA: Balozi Sefue na Yambesi watoe kauli iwapo Serikali imetoa waraka wa maagizo kwa watumishi wa umma kutoa taarifa katika mikutano ya CCM kinyume cha maadili
Kama kuna tatizo la maji, umeme na barabara na mnataka taarifa ya utekelezaji wa ilani ya CCM kuhusu masuala hayo, huyo mkuu wa wilaya ndiye aliyepaswa kutoa. Kama hakuwa na uwezo maana hana uwezo kwa kuwa yeye ndiye mwenyekiti wa kamati ya ushauri ya wilaya (DCC) ambayo hao wanohusika na maji, umeme na barabara ni wajumbe, na yeye ndiye anafanya kazi kwa niaba ya serikali na rais katika eneo lake. Hivyo, kama chama makini, badala ya kulaumu kwa watumishi wa umma kutokufika (ambao sio wajibu wao na maadili ya utumishi wa umma yanawakataza kutoa taarifa kwenye mikutano ya vyama), mlipaswa kumwajibisha huyo mkuu wa wilaya kwa masuala yanayohusu vyombo vya serikali kuu, na kwa mambo yanayohusu Serikali za Mitaa mlipaswa kuwahoji Meya na madiwani wenu; namna wanavyoisimamia serikali katika maeneo husika. Hata mkuu wa wilaya angeweza pia kutoa majibu kwa niaba yao kwa kuwa kuwa mujibu wa sheria, kupitia DCC Halmashauri huwasilisha pia taarifa zao.
Kuwajibika kwa umma ni tofauti na kuwajibika kwa CCM, ikiwa mkuu wa wilaya angetaka TANROADS, TANESCO nk wawajibike kwa umma angeitisha mkutano wa kiserikali na kuwataka wajieleze kwa wananchi bila kujali vyama vyao na sio kikao cha ndani cha CCM. Ikiwa CCM inataka kuonyesha uwajibikaji mbele ya umma iwaite viongozi wake wa kuchaguliwa madiwani, wabunge nk wenye wajibu wa kuisimamia serikali wajieleze kwenye chama sababu za kushindwa kuvisimamia hivyo vyombo vya kiserikali iwe ni TANROADS, TANESCO, halmashauri nk. Ikiwa CCM ina malalamiko dhidi ya mtumishi yoyote wa umma kuna utaratibu wake kwa mujibu wa sheria ya utumishi wa umma, na kama inabidi chama ndio kinasimamia sasa nidhamu ya watumishi wa umma, basi hawana niliowataja kwenye kauli hii: JOHN MNYIKA: Balozi Sefue na Yambesi watoe kauli iwapo Serikali imetoa waraka wa maagizo kwa watumishi wa umma kutoa taarifa katika mikutano ya CCM kinyume cha maadili na wawakilishi wao katika ngazi ya mikoa, wilaya, kata, mitaa/vijiji wameshindwa kazi, waachie ngazi.
Bado hujajibu hoja nilizozieleza kwenye: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...tokeo-ya-kukimbia-shule-masikini-chadema.html , kwa sasa naelekea kwenye mikutano na wananchi Manzese kuanzia muda mfupi ujao mpaka usiku saa nne; nitarejea baada ya hapo na kutoa maelezo ya ziada iwapo utakuwa umejibu hoja kwa hoja.
JJ