Majibu kwa Mnyika na CHADEMA juu ya watumishi wa umma na mikutano ya CCM

Honey K

JF-Expert Member
Sep 14, 2008
629
72
Naendelea kushangazwa na hoja zako juu ya uamuzi wa CCM wa kusimamia Ilani yake ya Uchaguzi. Lakini baada ya kusoma tamko lako la mwisho NIMEGUNDUA UELISHWA TANGO PORI JUU YA NINI KILITOKEA MWANZA, HIVYO SI KOSA LAKO SANA JAPO KAMA KIONGOZI KUWA MAKINI NA UNACHOLISHWA, ULINDE HESHIMA YAKO.

Ref thread ya TAMKO la CHADEMA: KAULI ya CHADEMA juu ya watumishi wa umma kutoa taarifa katika mikutano ya CCM

Katika andiko lako umekiri SI KOSA KUWAITA WATEULIWA WA KISIASA NA KUWATAKA KUELEZEA UTEKELEZAJI WA ILANI YA UCHAGUZI!!! Sasa hebu niambie ni wapi tumewaita watendaji ambao sio wateuliwa wa kisiasa? Kwasababu hata hiyo hoja ya Mwanza aliyeitwa kwenye ule mkutano ni Mkuu wa Wilaya Ndg. Konisaga, yeye Mkuu wa wilaya ambaye kwa mujibu wa sheria ulizozielezea kabla ana mamlaka ya kutaka taarifa kutoka kwa watendaji anaowasimamia wakati wowote aliamua yeye kwa mamlaka aliyo nayo kuja kwenye kikao na wasaidizi wake...jambo la kawaida sana na jema hasa mnapojadili mambo ya maendeleo ya watu. Kwenye kile kikao wakati yeye ana ripoti akasema kuna tatizo kubwa la maji, barabara na umeme kwenye eneo lake analosimamia na bahati mbaya watendaji wa maeneo hayo aliwaita waje kusikia(KUSIKIA) WENYE ILANI WANASEMAJE JUU YA MALALAMIKO YA WANANCHI KWENYE MAENEO HAYO HAWAKUJA.

Sasa la kwanza hawa watendaji hawakuitwa na CCM waliitwa na Mkuu wa wilaya kwa barua rasmi za kiofisi toka kwa DC. CCM ilimwita Mkuu wa wilaya, ambae licha ya kuwa kada wake, ni mjumbe wa vikao halali vya CCM na anawajibu wa kuwasilisha utekelezaji wa ilani kwenye vikao vya CCM. Tens CCM ilimwita DC kwa barua rasmi kama DC. CCM haikumwita Meneja wa Tanroads wala Tanesco.

Isipokuwa baada ya DC kutoa taarifa ya kukaidi kwa hawa mameneja nikasema tena kwa ukali si sawa HAWA NI WATUMISHI WA UMMA, KWAO KUITWA TENA NA BOS WAO KWENDA KUELEZEA UTEKELEZAJI WA MAENEO YAO YA KAZI SI KWA CHAMA TU HATA KWA WANANCHI WA KAWAIDA KABISA NI SEHEMU YA WAJIBU WAO. NDIO NAMNA BORA YA WATUMISHI WA UMMA KUWAJIBIKA KWA UMMA...MNAPOSEMA NGUVU YA UMMA HUKU MKIPUUZA UMMA NI UNAFIKI UNAONUKA.

Ndio maana hata mikoani kote tulipotaka maelezo ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi tuliwabana MAWAZIRI, MA RC, MA DC, WABUNGE NA MADIWANI NA SI ZAIDI YA HAPO... SASA UKIMBANA WAZIRI CHINI YAKE YUPO MKURUGENZI AU RAS NK WAKIBANANA WAO HILO HALITUHUSU SISI... SISI TUNASHUGHULIKA NA HUYU WA KWETU BASI.

SASA SEMA NA HAWA NI KOSA SISI KUWABANA JUU YA UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU YAO.

##########
MAJIBU ya Mhe. John Mnyika:

Nape,

Walatini wanamsemo ambao kwa kiswahili rahisi humaanisha maandiko hubaki, mlichokifanya Mwanza wewe na viongozi wengine wa chama chako kiliandikwa, mfano: CCM yabuni mbinu mpya kwa hiyo unataka kusema kwamba magazeti yaliwasilisha maneno? Na sio magazeti tu, baadhi ya vituo vya televisheni vilirusha, na hayakuwa maneno yako pekee siku ile, weka hapa mkanda wa wote mliozungumza siku ile na umma wenyewe utaweza kupima ukweli ni upi.

Nashukuru kwamba maelezo yako yanamaanisha kwamba umeanza sasa kutambua kwamba CCM haina mamlaka ya kuwaita wakurugenzi na maafisa wa Halmashauri, wakurugenzi na wafanyakazi wa mashirika ya umma kuja kujieleza na kutoa taarifa kwenye vikao vya CCM. Kwa maelezo yako umethibitisha usahihi wa nilichokisema hapa: JOHN MNYIKA: Balozi Sefue na Yambesi watoe kauli iwapo Serikali imetoa waraka wa maagizo kwa watumishi wa umma kutoa taarifa katika mikutano ya CCM kinyume cha maadili

Kama kuna tatizo la maji, umeme na barabara na mnataka taarifa ya utekelezaji wa ilani ya CCM kuhusu masuala hayo, huyo mkuu wa wilaya ndiye aliyepaswa kutoa. Kama hakuwa na uwezo maana hana uwezo kwa kuwa yeye ndiye mwenyekiti wa kamati ya ushauri ya wilaya (DCC) ambayo hao wanohusika na maji, umeme na barabara ni wajumbe, na yeye ndiye anafanya kazi kwa niaba ya serikali na rais katika eneo lake. Hivyo, kama chama makini, badala ya kulaumu kwa watumishi wa umma kutokufika (ambao sio wajibu wao na maadili ya utumishi wa umma yanawakataza kutoa taarifa kwenye mikutano ya vyama), mlipaswa kumwajibisha huyo mkuu wa wilaya kwa masuala yanayohusu vyombo vya serikali kuu, na kwa mambo yanayohusu Serikali za Mitaa mlipaswa kuwahoji Meya na madiwani wenu; namna wanavyoisimamia serikali katika maeneo husika. Hata mkuu wa wilaya angeweza pia kutoa majibu kwa niaba yao kwa kuwa kuwa mujibu wa sheria, kupitia DCC Halmashauri huwasilisha pia taarifa zao.

Kuwajibika kwa umma ni tofauti na kuwajibika kwa CCM, ikiwa mkuu wa wilaya angetaka TANROADS, TANESCO nk wawajibike kwa umma angeitisha mkutano wa kiserikali na kuwataka wajieleze kwa wananchi bila kujali vyama vyao na sio kikao cha ndani cha CCM. Ikiwa CCM inataka kuonyesha uwajibikaji mbele ya umma iwaite viongozi wake wa kuchaguliwa madiwani, wabunge nk wenye wajibu wa kuisimamia serikali wajieleze kwenye chama sababu za kushindwa kuvisimamia hivyo vyombo vya kiserikali iwe ni TANROADS, TANESCO, halmashauri nk. Ikiwa CCM ina malalamiko dhidi ya mtumishi yoyote wa umma kuna utaratibu wake kwa mujibu wa sheria ya utumishi wa umma, na kama inabidi chama ndio kinasimamia sasa nidhamu ya watumishi wa umma, basi hawana niliowataja kwenye kauli hii: JOHN MNYIKA: Balozi Sefue na Yambesi watoe kauli iwapo Serikali imetoa waraka wa maagizo kwa watumishi wa umma kutoa taarifa katika mikutano ya CCM kinyume cha maadili na wawakilishi wao katika ngazi ya mikoa, wilaya, kata, mitaa/vijiji wameshindwa kazi, waachie ngazi.

Bado hujajibu hoja nilizozieleza kwenye: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...tokeo-ya-kukimbia-shule-masikini-chadema.html , kwa sasa naelekea kwenye mikutano na wananchi Manzese kuanzia muda mfupi ujao mpaka usiku saa nne; nitarejea baada ya hapo na kutoa maelezo ya ziada iwapo utakuwa umejibu hoja kwa hoja.

JJ
 

BONGOLALA

JF-Expert Member
Sep 14, 2009
16,515
11,824
mkuu hawa ni watendaji,kazi yao sii kwenda kwenye majukwaa ya ccm,dc,council kutoa taarifa!wanawajibika ktk bodi zao
 

Kakende

JF-Expert Member
Aug 18, 2012
2,741
1,231
Nape achana na mambo madogomadogo haya ya Mnyika. Tayari tunajua afisa kilimo si jukumu lake kusoma utekelezaji mbele ya vyama, ni jukumu la wanasiasa kwenda kwa afisa kilimo na kumuomba hizo ripoti then msomeane wenyewe.

Hiyo hoja yako haitakusaidia. Tuelezee hatima ya mabilioni ya Uswis
 

Ulukolokwitanga

JF-Expert Member
Sep 18, 2010
8,402
7,950
Acha usanii wa maneno wewe Nape, tumeona kwa macho yetu na kusikia kwa masikio yetu yule mama aliyejichubua katibu wa CCM akijigamba kuwa apelekewe majina ya hao watendaji ataweka saini kupitisha yaende ngazi za juu washugulikiwe...

Wewe baada ya kukumbana na aibu ya jana kuja na maneno ya kashfa dhidi ya Mnyika kuwa alikimbia shule lakini watu wakaonesha hapa kuwa form 4 Mnyika alipata Division 1 ya point 7 wewe ulipata division 4; na form 6 Mnyika alipata div 1 ya point 3 wewe ukapata division ZERO, umeamua kuja kivingine kwa heshima ya mgongo wa chupa kujidai kumwita Mnyika mbunge wako. Kinachokupa kiburi ni uwezo wako wa kununua vyeti hadi cha Masters kwa kuwa ninyi CCM mmeingiza ufisadi hadi kwenye elimu.

By the way bosi wako JK ana PhD tano, DR DR DR DR DR Kikwete, but alivyokuwa chuo GPA yake ilikuwa 2.1, ambayo chuo wanaita GPA ya kuku. Ndio maana CCM inapwaya sana kiuongozi kwa kuwa watu wenye IQ za kuku ndio mnaongoza chama na nchi. Mwenzio Mwigulu alifeli darasa la saba akaacha jina la Lameck Madelu na kununua la Mwigulu Nchemba.

CCM is full of failures
 

Alvin Slain

JF-Expert Member
Aug 30, 2011
6,376
3,618
Nape huna jipya zaidi ya kushambulia mtu binafsi kwa kukosa namna ya kujibu hoja!
 

Mlengo wa Kati

JF-Expert Member
Feb 16, 2011
2,730
491
chadema mara nyingi wamekua wakiongozwa na matamanio ya 2015,na hili limewafanya hata kukurupuka kutoa matamko,hivi chama kinacho shinda uchaguzi kazi yake nini zaidi ya kuongoza selikali? chadema wanataka tuamini kuwa hata halmashauri wanazo ongoza watumishi hawaguswi kabisa? kama wana mbana meya nae meya ana mbana mkurugenzi,mkurugenzi nae ana wabana wakuu wa idara,nao wakuu wa idara wana shuka chini na hatimae wananchi wanaona utekelezaji! kwa tamko lenu chadema mlishauriwa na mlevi!
 

Nicas Mtei

JF-Expert Member
Dec 21, 2010
11,560
7,073
Bwanamdogo Kapotolo
hakuna anayeshindana hapa, tunazungumza. Mimi kuzungumza na mbunge wangu wewe inakuuma nini? Umeamkaje hata hivyo?

Pamoja na povu lote ulilomwaga sijaona pahala umejibu hoja za Mnyika.. Naona umebwabwaja tu bila kueleweka.. Iambie CC yenu ikae, mjipange jinsi ya kumjibu Mnyika. Wewe mwenyewe hauwezi kushndana na Mnyika. Unavyoendelea kukurupuka unakiaibisha Chama Cha Majangili{CCM} Pia unajiaibisha wewe mwenyewe. Kajipangeni upya.
 

Imany John

JF-Expert Member
Jul 30, 2011
2,921
1,133
katibu mwenezi mwenye uwezo wa kutumbuiza mbele ya mafisadi kwa uhodari wa kupapasa nyuzi sita za gitaa.

Leo unatumia keyboard,je unadhani nasisi tunaweza kukusifia kama wafanyavyo hao wanaokushabikia pindi utoapo burudani?
 

Leak

JF-Expert Member
Feb 22, 2012
49,750
35,817
Nnauye Jr bwana, naona kidogo umeanza kujifunza kuwa na hekima baada ya kupata funzo kutoka kwenye hile thread yako ambayo umeikimbia mwenyewe.

Unapenda kuuliza Maswali na upate majibu, hivi we umejibu maswali yakule kwenye thread uliyo hianzisha mwenyewe?.

Alaf bado ujaelewa ulicho funzwa jana na John Mnyika ngoja atakuja kuongezea ili ushibe vyema!
 
Last edited by a moderator:

sosoliso

JF-Expert Member
May 6, 2009
8,538
9,433
Sasa la kwanza hawa watendaji hawakuitwa na CCM waliitwa na Mkuu wa wilaya kwa barua rasmi za kiofisi toka kwa DC. CCM ilimwita Mkuu wa wilaya, ambae licha ya kuwa kada wake, ni mjumbe wa vikao halali vya CCM na anawajibu wa kuwasilisha utekelezaji wa ilani kwenye vikao vya CCM. Tens CCM ilimwita DC kwa barua rasmi kama DC. CCM haikumwita Meneja wa Tanroads wala Tanesco.

Nape.. Unakataa kwamba hawa hawakuitwa na CCM bali na "boci" wao DC.. na hapo hapo unakiri kwamba DC ni kada wenu ambae ni mjumbe halali wa vikao vya CCM..! Waje kwenye mkutano wa CCM waelezee utekelezaji ilani ya chama..! Unaona hiyo ni sawa kweli..? Ndio maana tunazidi kupoteza mwelekeo..

Maamuzi ya kiutendaji yanachanganywa na siasa.. Mnyika yuko right kutoa tamko kama lile.. Please Nape & co concentrate kwenye kurudisha imani toka kwa wanachama wenu na sio kuingilia mambo ya utendaji wa wafanyakazi..
 

diwan

JF-Expert Member
Apr 1, 2012
308
111
Jibu hoja Makini za JJ. Huwa mnaita watumish mfano ule mkutano wa Kigoma mliwaita Mu.Nape naona hapa umepotea na mjichanganye kuwafukuza muone.
 

Imany John

JF-Expert Member
Jul 30, 2011
2,921
1,133
Jibu hoja Makini za JJ. Huwa mnaita watumish mfano ule mkutano wa Kigoma mliwaita Mu.Nape naona hapa umepotea na mjichanganye kuwafukuza muone.

Thanx bwana diwani,naona unawawakilisha vema wananchi wako hapa jf.
 

manuu

JF-Expert Member
Apr 23, 2009
4,067
10,707
Big up Nnauye Jr atleast umeonyesha ishara ya 2015 hamtakimbia midahalo ya papo kwa papo, Na naona mnaanza kuchukua uzoefu na umeamua kuanza na Mnyika.

Ushauri wangu ebu Mnyika aje huku na debate ianze rasmi na sisi wengine tutakuwa marefarii.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

18 Reactions
Reply
Top Bottom