Maji yakipwa huenda wapi?

Hilo la maji kupwa na kujaa mbona dogo sana. Jiulize nje ya mfumo wa hili jua letu wapi mwisho. Na huo mwisho nyuma yake au mbele yake kuna nini?

Hapo utaambiwa ni kama vile kujiuliza mwisho wa namba za kuhesabia ni nini. Ipi namba ya mwisho.
 
Nini kinachohamisha maji ya bahari kutoka point moja kwenda nyingine?
Wanasayansi wanasema maji ya bahari huvutwa na mwezi, kwahiyo ule upande ambao mwezi upo basi maji yataegemea huko na kusababisha upande mwingine ukose maji. Kwahiyo wakati upande fulani wa bahari duniani umejaa maji kuna upande mwingine maji yanapungua.
 
mkuu mwezi unaingiaje hapo?
Mwezi ni moja ya bodies ambazo huzunguka dunia. Na ndo ipo jirani zaidi na dunia, hivyo kimsingi kama ilivyo kwa Dunia, mwezi nao una kani ya uvutano au gravitational force ambayo inavuta kila kilichopo duniani katika usawa wake.

Sasa basi, kutokana na muundo wa maji hauna particles zilizoshikamana kama maada zingine basi ni rahisi kuathiriwa na mvutano huo ambao unaanzia kwenye Jua.

Kwahiyo upande ambao unatazamana na mwezi ambao huzunguka dunia basi maji ya bahari ya upande huo ambayo yamechukua asilimia kubwa ya dunia yatafuata uelekeo huo na kutengeneza kupwa na kujaa kwa maji baharini.
 
Faka25 njoo huku
 
nimependa sema sijaelewa.
 
Hilo la maji kupwa na kujaa mbona dogo sana. Jiulize nje ya mfumo wa hili jua letu wapi mwisho. Na huo mwisho nyuma yake au mbele yake kuna nini?

Hapo utaambiwa ni kama vile kujiuliza mwisho wa namba za kuhesabia ni nini. Ipi namba ya mwisho.
Naelewa 100% unachomaanisha. Lazima tufikie hatua, kama wanadamu, tuamini na kukubali kwamba sayansi yetu hii, ama angalau tunavyoielewa sasa, haina maelezo ya kutosheleza kuhusu ulimwengu.

Ndiyo maana sayansi inazungumzia ^visible universe.^ It means inatambua fika kwamba universe is almost as though ni infinite au hata unfathomable.
 
nimependa sema sijaelewa.
Ameeleza vizuri sana, kwa ufupi. Nadhani ambacho kinaweza kuleta utata kwa baadhi ni namna ambavyo mwezi unaweza kuyavuta maji.

Fikiria mwezi kama sumaku, then dunia na kila kitu (na maji pia) ni sumaku. Kwa hiyo vinavutana. Sasa maji kwa vile hayashikamani, yanavutwa na kuhama kulingana na uelekeo wa mwezi na jua angani.

Ikumbukwe kwamba mwezi (na jua) huwa sehemu tofauti tofauti angani, na hii huamua ni wapi kwenye uso wa dunia kuna kani yake ya uvutano mkubwa zaidi.

Palipo na kani kubwa ya uvutano, maji huvutwa zaidi na hivyo hujaa (high tide). Palipo na kani ndogo ya uvutano, maji hupwa (low tide).
 
Sawa sana mkuu. Umeleeweka mpaka hapo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…