Maji ya kisima yamechafuka.

Speaker

JF-Expert Member
Aug 12, 2010
6,324
2,238
Kachimbe kisima wewe mwenyewe ndugu yangu na unywe maji yako peke yako.
Usishiriki na mwingine,Ni hatari kubwa sana.

Hakika,maji ya kisima cha watu wengi yameingiliwa na mdudu,
ukiwa na kiu usiyaonje,Utaambukizwa.

Siku hizi kiu ya maji imeongezeka sana,watu wanayanjwa maji kila wakati,...
mengine yanauzwa kila kona ya barabara,..mengine hutolewa bure.
Nani atapona?

Kwa sababu maji yameingiliwa na mdudu,yanapatikana kiurahisi sana.
Ukipita kote utayaona,usiyanywe.

Yapo yaliyowekwa kwenye chupa kubwa na ndogo,wengi wanakimbilia yaliyo
kwenye chupa ndogo wakidhani ndio salama,wana jidanganya....
Hayo ndio machafu kupindukia.

Tafadhalini sana wapendwa,chimba kisima chako mwenyewe.
Chota maji vile utakavyo,chemsha mara kwa mara na usiyanywe na mtu mwingine
nawe utakuwa salama.

Kuweni na weekend njema.
 
na mie nina rig ya kuchimbia visima
naweza kujua sehemu ya kuchima kisima kwa matokeo mazuri zaidi

at a reasonable price
discount ipo.
 
Ujumbe wako umesikika mbali kupitiliza mipaka.
Mazoea ya kubadilisha kisima cha maji kila leo ndio hatari ya kutojua maji yapi yako safi kuyanywa.
Kisima chako mwenyewe utakitunza vizuri kila siku na kuhakikisha kimefunikwa virus hawaingii.
Wengi tuna kawaida ya kuchota maji na kuyanywa kwa domo toka kiganjani, hakuna hakika ya safi au la na hatuna fulsa ya kuyachemsha .
Wengine tamani ya kisima cha mbele au kisima kinachopatikana kwa urasihi hukimbilia kuchota maji kumbe ndio kipindupindu kimejaa.
Weekend tunapopumzika ndio kiu inatushika zaidi na mara nyingi hata maji ya kisima changu hayazimi kiu ila kisima cha jirani kina maji ya kuzima kiu.

Mimi kufa na kupona na kisima changu, maana visima vingine sina nafasi ya kuhakiki usalama wa maji yake.

Yes weekend njema na tujihadhari na maji ya visima mbalimbali hasa ya maji bei poa, na hasa visima vinayvozagaa ovyo mitaani, utakuja shtukia siku mtu unaharisha na kutapita kipindupindu kisicho na tiba huku mtu anachungulia na kuyaona mauti yanavyomchelewesha, maji haya ya visima balaa, maana wengine haturidhii kupata kikombe kimoja cha ndani, tunataka visima vya kulee vyenye kutoa vikombe zaidi vya kunywa, hapo mambo ni mkorogo wa kutojijua na mwendoo huu kipindupindu kitakaponishika sitajua ni kisima kipi ambacho hakikuwa na maji salama.
 
Duh! umemwelewaje mleta mada yakhe? Una drill babukubwa ati? Au ndo mwenye kisima unataka tujikimu kwako? Una hakika na maji yako hayana virus?
 
Mchimba kisima...? Kaingia mwenyewe! Kaingia.

Hii Jamii forums ni meli inayokusanya wengi kuanzia watoto wachanga hadi maajuza na vibabu. Hilo usishangae maana ndivyo alivyosoma mstari kwa mstari na kuuelewa wakati we unaangali ujumbe gani umebebwa katika mada hii.
 
Ngoja nijichimbie cha kwangu pekeangu, na ntahakikisha nikigongea maji kwa jirani nayachemsha.
 
Tafadhalini sana wapendwa,chimba kisima chako mwenyewe.
Chota maji vile utakavyo,chemsha mara kwa mara na usiyanywe na mtu mwingine
nawe utakuwa salama.

hivi kiumbe chaweza kweli kujichimbia kisima chake yenyewe na kunywa maji chenyewe bila ya kuingiliwa? Nijuavyo Muumba ndiye awezaye kukuwezesha ukaqfanikisha hayo....pekee yako huwezi................kwanza uwezo wa kukichimba hicho kisima hatuna. pili kisima nacho kinasikia kiu na chaweza kutafuta maji kutoka kwenye visima athirika na kukusogezea wewe vijirusi kutoka visima hatarishi...................................mambo siyo mepesi hivyo......................mtegemee Muumba kwa yote atakuongoza njia stahiki..........
 
Tangu lini rig ikatoa maji? Mtajikimu vipi maji kwenye rig?

Mie nachimba visima kwa matokeo mazuri, kwa bei nafuu na pungufu unaongea.

Duh! umemwelewaje mleta mada yakhe? Una drill babukubwa ati? Au ndo mwenye kisima unataka tujikimu kwako? Una hakika na maji yako hayana virus?
 
Ujue profesa anaweza chomwa sindano na nesi ambaye ni fomu foo tu.

Si kila mara zinahitajika akili nyingi hivyoo.
Hii Jamii forums ni meli inayokusanya wengi kuanzia watoto wachanga hadi maajuza na vibabu. Hilo usishangae maana ndivyo alivyosoma mstari kwa mstari na kuuelewa wakati we unaangali ujumbe gani umebebwa katika mada hii.
 
ukishachimba cha kwako mwenyewe utajuaje kama watu hawaji kukuibia ukitoka????labda ukifunike na ukitie kofuli
 
mimi huwa nachimba kwa selulu. wakati wakati wa kuchimba navaa gloves na mabuti pia. siwezi chimba pekupeku coz naogopa wadudu.
 
Vingine si visima ni mabwawa , yatumika kama josho
Ng'ombe na punda wanawa,hata mamba na viboko
 
Ujumbe wako umesikika mbali kupitiliza mipaka.
Mazoea ya kubadilisha kisima cha maji kila leo ndio hatari ya kutojua maji yapi yako safi kuyanywa.
Kisima chako mwenyewe utakitunza vizuri kila siku na kuhakikisha kimefunikwa virus hawaingii.
Wengi tuna kawaida ya kuchota maji na kuyanywa kwa domo toka kiganjani, hakuna hakika ya safi au la na hatuna fulsa ya kuyachemsha .
Wengine tamani ya kisima cha mbele au kisima kinachopatikana kwa urasihi hukimbilia kuchota maji kumbe ndio kipindupindu kimejaa.
Weekend tunapopumzika ndio kiu inatushika zaidi na mara nyingi hata maji ya kisima changu hayazimi kiu ila kisima cha jirani kina maji ya kuzima kiu.

Mimi kufa na kupona na kisima changu, maana visima vingine sina nafasi ya kuhakiki usalama wa maji yake.

Yes weekend njema na tujihadhari na maji ya visima mbalimbali hasa ya maji bei poa, na hasa visima vinayvozagaa ovyo mitaani, utakuja shtukia siku mtu unaharisha na kutapita kipindupindu kisicho na tiba huku mtu anachungulia na kuyaona mauti yanavyomchelewesha, maji haya ya visima balaa, maana wengine haturidhii kupata kikombe kimoja cha ndani, tunataka visima vya kulee vyenye kutoa vikombe zaidi vya kunywa, hapo mambo ni mkorogo wa kutojijua na mwendoo huu kipindupindu kitakaponishika sitajua ni kisima kipi ambacho hakikuwa na maji salama.

Dah,mkuu candid nashukuru umenielewa kupita maelezo.
Wengine wanachimba kisima chao wenyewe lakini matunzo yanakua madogo.
Matokeo yake hadi mijusi wanaingia kuogelea humo na kuchafua kisima.

Hata ukichimba kisima chako mwenyewe na usiende nje,kama hukitunzi vyema
na kukijali lazima maji yatachafuka na utaugua vibaya.
 
Ngoja nijichimbie cha kwangu pekeangu, na ntahakikisha nikigongea maji kwa jirani nayachemsha.

Hahaha,unagongea maji kwa jirani tena na unakisima chako tayari?
Urafi huo,yanaweza kukutokea puani na yakaharibu afya yako bana.
Duh
 
Duh! umemwelewaje mleta mada yakhe? Una drill babukubwa ati? Au ndo mwenye kisima unataka tujikimu kwako? Una hakika na maji yako hayana virus?

Yeye anadhani mada inapaswa kuwa kwenye Business Forum.
Hapa ndipo mahala husika.
 
hivi kiumbe chaweza kweli kujichimbia kisima chake yenyewe na kunywa maji chenyewe bila ya kuingiliwa? Nijuavyo Muumba ndiye awezaye kukuwezesha ukaqfanikisha hayo....pekee yako huwezi................kwanza uwezo wa kukichimba hicho kisima hatuna. pili kisima nacho kinasikia kiu na chaweza kutafuta maji kutoka kwenye visima athirika na kukusogezea wewe vijirusi kutoka visima hatarishi...................................mambo siyo mepesi hivyo......................mtegemee Muumba kwa yote atakuongoza njia stahiki..........

Topic yangu imeegemea kwenye maandiko yaliyo andikwa na mfalme solomon,....
katika kitabu cha Mithali 5:15
Drink water from your own cistern, running water from your own well

Mungu ndiye anaye kupa nguvu za kuchimba kisima chako,na hekima anayo kupa ndio itakuwezesha
kukitunza kisima chako vyema ili wadudu na wanyama wasiingie kuyachafua.

Lakini huwezi kukaa tu ukasubiri akwambie lini uanze kuchimba,...alitupa hekima na maarifa ya kuamua
lini ufanye nini.....Unakumbuka Story ya Nuhu?

Kwanini aliamua kumtoa kunguru nje aangalie kama maji yamekwisha?
Kwanini alimtoa tena Njiwa aangalie hali ya maji?

Kwanini hakusubiri tu Mungu amwambie,...maji yameisha bana toka nje?

Alifanya aliyoweza kufanya,...lakini mwisho Mungu alimwambia Yes,it's time toka nje.
Genesis 6-15
 
ukishachimba cha kwako mwenyewe utajuaje kama watu hawaji kukuibia ukitoka????labda ukifunike na ukitie kofuli

Yes,umeuliza swali na kujibu mwenyewe.
Lakini kufuli usilichukulie "literally",....kufuri limebase kwenye spiritual beliefs.
 
Back
Top Bottom