Mbunge alazimishwa Kunywa Maji machafu na Wananchi wake

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,646
109,031
Tafadhali naomba kujua hawa Wananchi wa hilo Jimbo wangependa GENTAMYCINE niwape Zawadi gani kwa Kunifurahisha hivi?

Na Mimi sasa najiandaa kuanzisha Kampeni ya chini chini na Wananchi wa Jimbo langu ili Mbunge Wetu Samjo Samjo ( Muongo Muongo ) japo ni Mtumishi wa Mola ( Maulana ) nae akija Jimboni Kwetu tunuokoteshe Takataka Ngumu zilizojazana Mitaani Kwetu na atuambie kwanini hadi leo hajatupeleka Japan na Australia kujifunza Uvuvi wa Samaki wa Kisasa.

Kwa wale mnaotaka Kusoma hii Taarifa ya Mbunge aliyelazimishwa kunywa Maji Machafu na Wananchi wake katafuteni Nakala ya Gazeti pendwa la JAMVI LA HABARI la Leo ( tarehe 5 August, 2023 ) ipo katika Ukurasa wa Nne ( 4 )

Kudos sana Kwenu nyie Wananchi!!!

==============

Wakazi wa mitaa ya Milupwa na Misunkumilo Manispaa ya Mpanda wamelalamikia Changamoto ya ukosefu wa maji ambapo inawalazimu kutumia maji yasiyo safi na salama.

Mbele ya Mbunge wa Jimbo la Mpanda mjini Sebastian Kapufi leo Augosti 4, 2023 wakazi hao wamesema eneo hilo halina bomba hata moja wanatembea umbali mrefu kwenda kuchota maji machafu.

"Kupitia wimbo wakiwa wamebeba chupa ya plastiki iliyo na maji yasiyo salama walimuomba kunywa maji hayo ishara ya kutatuliwa kero hiyo," amesema.

"Walisikika kwa sauti moja tunaomba unywe pombe hii uone ilivyo tamu," zilisikika sauti zao.

Joyce John mwananchi wa eneo hilo, amesema maji hayo yanawaathiri kiafya kwa kuwa wamekuwa wakiugua matumbo ya kuhara mara kwa mara na watoto wao.

"Tumekuja nayo makusudi anywe maana tunafahamu hawezi kunywa anaogopa, atusaidie kuisimamia serikali itatue changamoto hii," amesema Joyce.

Diwani wa Kata ya Misunkumilo Matondo Kanyigu akagongela msumari suala hilo akidai litatufutiwe mwarobaini ili kunusuru hali hiyo.

“Mbali na changamoto hizo pia wanakabiliwa na changamoto ya barabara na nishati ya umeme, vitu hivi tukivipata wakazi hawa wataendelea kuwa na raha,” amesema.

“Watakuwa na imani na serikali yao inayoongozwa na Chama Cha Mapinduzi, Mbunge barabara ya kutoka Misunkumilo-Utemini kuelekea misheni, wananchi wanahoji ni lini itakamilika,” amesema Kanyigu.

Aidha Kapufi kabla ya kutolea majibu kero hizo akahitaji kupata ufafanuzi kuhusu ukosefu wa maji kutoka ofisi ya Mamlaka ya Majisafi mjini Mpanda (Muwasa).

“Yupo mwakilishi hapa naomba uwaeleze wananchi hii kero itapatiwa ufumbuzi lini ili wananchi waondokane na tatizo hilo?” ameeleza.

Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi mjini Mpanda, Rehema Nelson akataja mikakati miwili ya muda mfupi na mrefu ili kukabiliana na changamoto ya maji.

“Nimesikitika kuona yale maji mliyompa mbunge wenu, mmesema mnayatumia kunywa, mkakati wetu wa kwanza tumeona kuna uhitaji wa kuwachimbia kisima wakati mkakati wa muda mrefu ukiendelea,” amesema.

Ameongeza kuwa mkakati wa muda mrefu ni wa kusambaza maji kutoka bwawa la Milala ambapo hadi sasa mkandarasi yupo eneo la mradi anaendelea kufanya usanifu na unatarajiwa kukamilika Oktoba 2025.

“Kwa huu muda mfupi tutamtuma meneja ufundi aje aangalie hili eneo na litafanyiwa utafiti, tutawachimbia kisima mpate maji safi,” amesema Rehema.

Hatimaye Mbunge Kapufi akawaondolea wasiwasi wananchi kuwa Serikali inatambua kilio chao na imeanza kutekeleza mradi mkubwa wa maji katika miji 28 nchini.

“Mpanda tumepata bahati ya kusambaziwa maji kilometa 42 ni nyingi ikilinganishwa na maeneo mengine, pia kuna mpango mkakati wa kuleta maji kutoka Ziwa Tanganyika,” amesema Kapufi.

Changamoto ya barabara amewaomba wananchi kutoa ushirikiano ili waletewe greda la kutengeneza yeye yupo tayari kuchangia jitihada zao.

“Mapinduzi wananchi walichangia nikawaongezea, wananchi wa Shanwe nao wamesema tayari wana shilingi milioni moja na laki tano greda linagombaniwa,” amesema.

Amesema halmashauri kupitia bajeti ijayo imekusudia kutenga Sh100 milioni kwa ajili ya kuchonga barabara.

“Tarura nao awamu hii wameongezewa fedha za kutosha kwaajili ya maboresho ya barabara, natumia fursa hii kumshukuru sana rais wetu,” amesema.

MWANANCHI
 
Tafadhali naomba kujua hawa Wananchi wa hilo Jimbo wangependa GENTAMYCINE niwape Zawadi gani kwa Kunifurahisha hivi?

Na Mimi sasa najiandaa kuanzisha Kampeni ya chini chini na Wananchi wa Jimbo langu ili Mbunge Wetu Samjo Samjo ( Muongo Muongo ) japo ni Mtumishi wa Mola ( Maulana ) nae akija Jimboni Kwetu tunuokoteshe Takataka Ngumu zilizojazana Mitaani Kwetu na atuambie kwanini hadi leo hajatupeleka Japan na Australia kujifunza Uvuvi wa Samaki wa Kisasa.

Kwa wale mnaotaka Kusoma hii Taarifa ya Mbunge aliyelazimishwa kunywa Maji Machafu na Wananchi wake katafuteni Nakala ya Gazeti pendwa la JAMVI LA HABARI la Leo ( tarehe 5 August, 2023 ) ipo katika Ukurasa wa Nne ( 4 )

Kudos sana Kwenu nyie Wananchi!!!
weka picha basi
 
Kumbe degree yako ukaipoteza kwa kundikia hivyo vigazeti? Ndo maana humu unabwabwaja tu
Wewe Degree yako ingekusaidia ungekuwa Unafumuliwa Mirinda Orange yako kila mara mpaka Manesi wa Mwanyamala Hospital wamechoka kukufanyia Cleaning ya eneo Korofi lako?
 
Wewe Degree yako ingekusaidia ungekuwa Unafumuliwa Mirinda Orange yako kila mara mpaka Manesi wa Mwanyamala Hospital wamechoka kukufanyia Cleaning ya eneo Korofi lako?
Sasa umeandika nini? Mie darasa la nne ujue. Una la ziada?
 
Tafadhali naomba kujua hawa Wananchi wa hilo Jimbo wangependa GENTAMYCINE niwape Zawadi gani kwa Kunifurahisha hivi?

Na Mimi sasa najiandaa kuanzisha Kampeni ya chini chini na Wananchi wa Jimbo langu ili Mbunge Wetu Samjo Samjo ( Muongo Muongo ) japo ni Mtumishi wa Mola ( Maulana ) nae akija Jimboni Kwetu tunuokoteshe Takataka Ngumu zilizojazana Mitaani Kwetu na atuambie kwanini hadi leo hajatupeleka Japan na Australia kujifunza Uvuvi wa Samaki wa Kisasa.

Kwa wale mnaotaka Kusoma hii Taarifa ya Mbunge aliyelazimishwa kunywa Maji Machafu na Wananchi wake katafuteni Nakala ya Gazeti pendwa la JAMVI LA HABARI la Leo ( tarehe 5 August, 2023 ) ipo katika Ukurasa wa Nne ( 4 )

Kudos sana Kwenu nyie Wananchi!!!
Maji hayo hayakuwa machafu isipokuwa hayakuchujwa wakihofia watapunguza virutubisho vya chumvichumvi, mbona kila siku miaka yote yanatumika na wanaishi.
 
Maji hayo hayakuwa machafu isipokuwa hayakuchujwa wakihofia watapunguza virutubisho vya chumvichumvi, mbona kila siku miaka yote yanatumika na wanaishi.
Wewe ndiyo huyo Mbunge uliyenyweshwa hayo Maji Machafu na Wananchi au? Pole sana Mheshimiwa kama utakuwa ni Wewe.
 
Wewe ndiyo huyo Mbunge uliyenyweshwa hayo Maji Machafu na Wananchi au? Pole sana Mheshimiwa kama utakuwa ni Wewe.
Hata wakimwesha maji haisaidii lolote. Wanachotakiwa kufanya ni kupigana ili mfumo uliomuweka huyu mbunge uondoke na serikali inayoweka kipaumbele kwenye kununua mashangingi ibadilike au ibadilishwe.
 
Kama nyie ndiye mnajisifia kwa kuwa vipanga wa uandishi wa habari, DP world wana haki kutunga ule mkataba
Yeah I'm so much proud being a Pressman , Communication Expert and Critical Thinker from my lovely Varsity Saint Augustine Mwanza.
 
Back
Top Bottom