Maji Uhai yana ladha mbaya

Maji Uhai yana ladha mbaya

Utadhàni kuwa yamechotwa baharini, maji ya kunywa ya Uhai yana ladha ya chumvi nyingi isiyofaa kwa kunywa na kutuliza kiu TFDA na tbs mko wapi?
Wewe naona unautani na TBS na ISO! Huyatumia sana maji ya Uhai ni maji bora kabisa. Napata sio chini ya lita mbili kila siku , wewe naona uliuziwa yanayoandaliwa vichochoroni.
 
ila kama unataka maji ya kunawa uso, kupiga mswaki, kunawa mikono, kusukutua, kushusha/kupandisha pH ya mwili, kuponya kiungulia, n.k. basi nunua hayo yenye majina mengine. Lakini maji ya kunywa ni colorless, odorless, tasteless, shapeless. Yanatumika katika kukata kiu ya mtu mwenye kiu.

Maji yakunywa ni shapeless!!!!! nimejikuna nimekenua meno mwenzenu
 
Kwenye ukweli acheni tuseme!
uhai itakua imechakachuliwa haswaa, nilishanunua maji kariakoo sikufika robo nikatupa ni machungu mnoo wakati mwingine unakuta chumvi.
Nakuyajua kama si uhai halisi ni hadi ufungue unywe
 
Sio uhai, hapo umekunywa maji ya bomba, vijana wengi wanafake hayo maji.
 
Haya ndio tunayosema muache kukariri, pH unajua ni nini? Kwa taarifa yako kuna maji yana pH mpaka 10.

hebu tujuze vizur hapo wengi umetuacha,ph mpaka kumi ni nini acid au base?
 
hebu tujuze vizur hapo wengi umetuacha,ph mpaka kumi ni nini acid au base?

pH 10 inakuwaje acid? Kwa pH level 7 ni neutral, chini ya 7 ni acidity na zaidi ya 7 ni basic (alkaline). Na mwili unahitaji alkaline zaidi (ku-neutralise acids).
 
Maji ya kunywa ya uhai yana ladha mbaya chumvi isiyofaa kwa matumizi ya kunywa. Hivi wanachota baharini? TFDA na tbs toeni majibu kuhusu maji haya. Kunywa Chumvi nyingi kuna madhara kiafya.
Kama umeigundua adha ya maji ya uhai kwamba hayana ladha basi tumia mwanya huo kuwa in fursa ya kuanza kufanya biashara hiyo ya kusindika maji.
Vitu vya msingi kuwa Navyo ni : (1)Eneo (2)Chanzo cha maji (3)Filter za uhakika (4)Vibali mfano TBS ,TFDA n,k .Ili uweze kupata soko inabidi uweze Kutoa maji bora kuliko hayo ulioyataja na uuze kwa bei ileile au chin kidogo.
 
Maji ya kunywa ya uhai yana ladha mbaya chumvi isiyofaa kwa matumizi ya kunywa. Hivi wanachota baharini? TFDA na tbs toeni majibu kuhusu maji haya. Kunywa Chumvi nyingi kuna madhara kiafya.

maji ndanda ndio kiboko yao maji bariiidiiii na natural kabisa!
 
Jamani tusilete ubishi usio na maana maji ya uhai hizi chupa mpya sio mazuri yana chumvi nyingi km kuna makosa yarekebishwe atapoteza wateja mimi nilishaacha kuyatumia
 
Maji haya hayafai kwa afya ya binadamu. Usiangalie vibali kwani kwa nchi hi hata wewe ukitaka kibali cha tbs au kingine chochote unapata bila shida. Maji ya uhai hayafai kwa afya ta binadam yana chumvi sana.
 
Nimependa huu mjadala Jiulize mwenyewe ulishawahi kuona Watu wanakunywa maji ya Uhai kwenye mikutano mikubwa hata president Obama alikunywa maji ya Kilimanjaro pia ukiangalia mikutano mingi katika kumbi maarufu utaona watu wakinywa kilimanjaro hata timu ya taifa ya Brazil walikunywa kilimanjaro walivyokuja Maji ambayo Coca-Cola wanataka kuyanunua kwa mengi kwa hela ndefu sana ili brand iwe inapatikana world wide! Kifupi ni maji mazuri usishangae siku moja unaona watu na wachezaji wakinywa kwenye World cup.....

Athari za Maji yenye Chumvi.

Maji yenye chumvi yana athari kubwa sana kwa binadamu ikiwemo FIGO kushindwa kufanya kazi kwa kitaalamu huitwa (Kidney Failure) ambayo husababishwa na moja ya sababu kunywa maji yenye Chumvi nyingi Ndiyo maana Wavuvi wengi huwa wana maji yao ya kunywa wakikwepa chumvi ya maji ya bahari.


Kuhusu ladha.

Maji mara nyingi hayatakiwi kuwa na Ladha wala Harufu so ukiona maji yana radha ujue yana kasoro na huenda kemikali nyingi zimeyabadilisha hayo maji.
 
Siku zote unadhani kuwa watu wote wanatumwatumwa ovyo kama wewe ulivyo, utazikwa na pesa? jali maisha ya wenzio utapata thawabu kwa mungu. Kama kitu hakifai rekebisha kifae ili kitumike kwa watu wote. Ikulu na wabunge sio wajinga kuacha kutumia maji Uhai, yana kasoro.
kwa hiyo wanaotumia wote ni wajinga!!
 
pH 10 inakuwaje acid? Kwa pH level 7 ni neutral, chini ya 7 ni acidity na zaidi ya 7 ni basic (alkaline). Na mwili unahitaji alkaline zaidi (ku-neutralise acids).

Teh teh teh! kwi kwi kwi.... oooi jamani mbavu zangueee.... Mwili unahitaji maji kuzima kiu unayojisikia sio ku-neutralize acid. Kazi ya ku-neutralize acid is a secondary purpose. Viko vyakula na matunda venye kazi hiyo ya ku-neutralize acid mwilini ambavyo mtu anatakiwa kula. Lakini 99.9% ya wotu wote na viumbe vingine duniani huwa wanakunywa maji ili kuponya kiu yao wanayojisikia sio kuponya acid. Hivyo basi, kazi ya kwanza (basic) ya maji ya kunywa ni kukata kiu na nyingine zote ndo zifuate. Kama maji hayapozi kiu maji hayo yana kasoro kubwa, maana yanashindwa ku-regulate the body osmolarity effectively hivyo thirsty center itaendelea kudai maji ya kunywa kwa kuwa body cells zimekosa maji (intracellular body fluid imepungua). Hayo maji yenye pH 10 ni maji ya kunywa maalumu kwa kazi maalumu kwa watu maalum.
 
uhai yana PH 7.3 ukilinganisha na maji mengine kama masafi ya dewji yana PH 7.0.(maji mazuri ya kunywa yanatakiwa kuwa na PH 7.0) utaona kwamba ya dewji ni maji mazuri sana, kilimanjaro, ndanda, lulu, sayona yana PH 7.2 ambayo bado ipo juu. nadhani bakhresa anashindwa kumanage purification kwa sababu anazalisha in bulk quantity. ila masafi ndo yana take over bcoz ni maji fresh alafu bei poa. In next few days uhai drinking water will face extinction asipojirekebisha.
 
Azam tv ina udini, mara maziwa yake sio halisi na sasa maji ya uhai yana chumvi... duh! Haya tutafika.
 
"pH of Drinking Water;
Although the pH of pure water is 7, drinking water and natural water exhibits a pH range because it contains dissolved minerals and gases. SURFACE WATERS TYPICALLY RANGE FROM PH 6.5 TO 8.5 WHILE GROUNDWATER RANGES FROM PH 6 TO 8.5. WATER WITH A PH LESS THAN 6.5 IS CONSIDERED ACIDIC. This water typically is corrosive and soft. It may contain metal ions, such as copper, iron, lead, manganese and zinc. The metal ions may be toxic, may produce a metallic taste, and can stain fixtures and fabrics. The low pH can damage metal pipes and fixtures."

http://chemistry.about.com/od/ph/f/What-Is-The-Ph-Of-Water.htm

Kuna maji yanaitwa UDZUNGWA., NILINUNU KITONGA. NILITAKA PIGA CM KWA MKEMIA MKUU WA SERIKALI.
 
Back
Top Bottom