Muke Ya Muzungu
JF-Expert Member
- Jun 17, 2009
- 3,444
- 264
Majimarefu Asema Picha Imetengenezwa
Amemaliza maongezi na wakili maarufu jijini kuiburuza CHADEMA na MWANANCHI Mahakamani Jumatatu kwa kumchafulia jina na heshima yake ndani ya chama na jamii kwa ujumla
"Picha hii nilipigwa nikiwa na huyu mbunge mwenzangu, Vicent Nyerere (kulia), lakini huyu wa kushoto (Joshua Nassari) hakuwepo karibu yangu kabisa! Yeye alikuwa mbali akiamrisha vijana wanichome moto tena akiwa na hasira, tofauti na anavyocheka katika picha hii. Huu ni mchezo mchafu wa kuunganisha picha kwenye kompyuta uliofanywa na CHADEMA na kwa makusudi gazeti hili likaichapisha, baada ya kuona kwamba hatua aliyofanya Nassari ya kutaka niuawe jana ni mbaya sana. Nitalishitaki gazeti hili". Analalamika Mbunge wa Korogwe Vijijini Stephen Ngonyani wakati akionyesha picha inayomuonyesha akiwa katika furaha ya hali ya juu yeye, Nyerere na Nassari. Picha hiyo imechapishwa jana ukurasa wa kwanza gazeti la Mwananchi.Vilevile ukurasa wa kwanza gazeti la Tanzania Daima.