Maji Marefu Kuishitaki CHADEMA .....!!!!!

Muke Ya Muzungu

JF-Expert Member
Jun 17, 2009
3,444
264
Majimarefu Asema Picha Imetengenezwa
Amemaliza maongezi na wakili maarufu jijini kuiburuza CHADEMA na MWANANCHI Mahakamani Jumatatu kwa kumchafulia jina na heshima yake ndani ya chama na jamii kwa ujumla





"Picha hii nilipigwa nikiwa na huyu mbunge mwenzangu, Vicent Nyerere (kulia), lakini huyu wa kushoto (Joshua Nassari) hakuwepo karibu yangu kabisa! Yeye alikuwa mbali akiamrisha vijana wanichome moto tena akiwa na hasira, tofauti na anavyocheka katika picha hii. Huu ni mchezo mchafu wa kuunganisha picha kwenye kompyuta uliofanywa na CHADEMA na kwa makusudi gazeti hili likaichapisha, baada ya kuona kwamba hatua aliyofanya Nassari ya kutaka niuawe jana ni mbaya sana. Nitalishitaki gazeti hili". Analalamika Mbunge wa Korogwe Vijijini Stephen Ngonyani wakati akionyesha picha inayomuonyesha akiwa katika furaha ya hali ya juu yeye, Nyerere na Nassari. Picha hiyo imechapishwa jana ukurasa wa kwanza gazeti la Mwananchi.Vilevile ukurasa wa kwanza gazeti la Tanzania Daima.
 
Kwani kuna kosa gani kuwa jirani na Nassari mbona sijamwelewa ama amesahau nani alikuwepo, labda wamemtisha waliomweka madarakani akaona kuna kuwekwa pembeni. Awe wazi tu!!
 
huyu atakua bado anaamini siasa ni uadui..au ndio ile ya mwenyekiti wenzangu hawatanielewa. Nahisi adui mkubwa wa ccm ni chadema na sio matatizo ya mtanzania
 
Arejeshe pesa ya kuuza kitapeli mali za marehemu babamkwe wa kenya kwanza kabla ya kushitaki!
 
Huyu jamaa mimi simuelewi ukiangalia hiyo picha kwa makini unaona kabisa anachosema si kweli, kama alikuwa na Vincent iweje aonekane anamuangalia Nassari! na anasema Nassari alikuwa anaamlisha vijana wa Chadema wamchome moto, kwa mazingira ya kawaida mtu anayetishiwa kuchomwa moto angekuwa na sura ya kutishika maana usalama wake ungekuwa hatarini lakini tofauti na yeye anavyoonekana kwenye picha akiwa na furaha sana,ina maana alikuwa anafurahia tishio hilo! haya ndio matatizo ya waganga wa kienyeji kuwa wana siasa!mbona sasa hatishii kulishitaki na Tanzania Daima maana nalo lilipandika picha hiyo!
 
Hapo wa kushtakiwa ni chadema au mwananchi? Au mwananchi communications ni mali ya chadema????
Hawa watu sijui walipataje ubunge!!!
 
Heeeeeeeee
Hivi kwa nini anaitwa maji marefu???????????????
Nini kiini cha hili Jina???????????????

Tafakari
 
ni vizuri mara nyingine kusikia skendo ka izi kwa chadema because natural mchezo ukishakuwa mchafu haumalizwi na msafi
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom