Maji aliyoahidi JK zimewekwa rangi za CHADEMA

Mamndenyi

Platinum Member
Joined
Apr 11, 2011
Posts
44,689
Reaction score
64,731
Wana JF Salamu sana.
Wakati wa kampeni zake za kuingia ikulu JK aliahidi maji na umeme kwenye kijiji kimoja kilichopo mkoa wa pwani.

Kweli ikatangazwa tenda akapatikana mkandarasi. Mchakato ukaanza na kazi imefikia mwishoni mwishoni.

Maajabu yaliyopo ni kwamba lile tenk kubwa la kupokelea maji ili yasukumwe kwa wanakijiji limepakwa rangi za Chadema.

Ina maana rais atakapoenda kufungua hayo maji atakuwa anazindua mradi wenye rangi za Chadema.

Kwenye kuuliza kilichosababisha kufikia huku hakuna anayefahamu.

Hivi nyie viongozi tokea shina hadi serkali kuu inakuwaje hata msitupie macho kwenye miradi mikubwa kama hii?

....... nyie waosha vinywa matusi sitaki. ............
 
​Matusi ndo nini!?
 
Mkuu CCM ni kichwa cha mwendazimu pamoja na nyie mnaoendelea kuichagua kwa kudanganywa na chumvi ama sukari na vitenge,

Mmeshawapa ridhaa wanasahau matatizo yenu,..
 
Ngumu kutoka madarakani.
 
CHADEMA na viongozi wake ni watu wa ajabu kweli. Wanapenda sana kujisimika katika jamii (wapenda sifa).

Maji yamepatikana kwa sasa utawasikia CHADEMA na viongozi wake wakidai ndiyo wameleta. Wakati maji hayakuwepo, walikuwa wanasema, CCM imeshindwa kuleta maji katika kijiji hicho wakati serikali ya CCM ndiyo inakusanya kodi.
 
Mkuu Jibu hoja acha kutafuna maneno,.

Ccm wamewaachia wapiga kura wao matanki matupu.
 
CHADEMA na viongozi wake ni watu wa ajabu kweli. Wanapenda sana kujisimika katika jamii (wapenda sifa).

Maji yamepatikana kwa sasa utawasikia CHADEMA na viongozi wake wakidai ndiyo wameleta. Wakati maji hayakuwepo, walikuwa wanasema, CCM imeshindwa kuleta maji katika kijiji hicho wakati serikali ya CCM ndiyo inakusanya kodi.

Hawa makandarasi wana njama. Wanaweka itikadi kwenye miradi ya serkali.
 
Wana JF Salamu sana.
Wakati wa kampeni zake za kuingia ikulu JK aliahidi maji na umeme kwenye kijiji kimoja kilichopo mkoa wa pwani.

Kweli ikatangazwa tenda akapatikana mkandarasi. Mchakato ukaanza na kazi imefikia mwishoni mwishoni.

Maajabu yaliyopo ni kwamba lile tenk kubwa la kupokelea maji ili yasukumwe kwa wanakijiji limepakwa rangi za Chadema.

Ina maana rais atakapoenda kufungua hayo maji atakuwa anazindua mradi wenye rangi za Chadema.

Kwenye kuuliza kilichosababisha kufikia huku hakuna anayefahamu.

Hivi nyie viongozi tokea shina hadi serkali kuu inakuwaje hata msitupie macho kwenye miradi mikubwa kama hii?

....... nyie waosha vinywa matusi sitaki. ............
Nlidhani mjanja kumbe gamba bana
 
cdm ni mpango wa MUNGU , tanks zilikuwa plain lakini ghafla zina rangi ya ukombozi ! MwanaDiwani ni bora ukatubu dhambi zako .
 
Hawa makandarasi wana njama. Wanaweka itikadi kwenye miradi ya serkali.
Siyo njama tu, bali pia wanajenga mazingira ya ubaguzi kama kilivyo chama cha CHADEMA.

Kwanza mradi wa maji umefanywa na serikali ya CCM. Hakuna hata senti moja ya CHADEMA iliyochangia kwenye mradi.

Pili, Kama maeneo yote ambayo miradi imefanywa/inafanywa na serikali ya CCM ingekuwa inapaka rangi ya bendera ya CCM, nadhani nchi karibia yote ingekuwa imetapakaa bendera ya CCM.

Serikali ya CCM haipaki rangi za bendera ya CCM kwa sababu inatambua kuwa, waliochangia na kufanikisha miradi mbali mbali kwa njia moja au nyingine ni wananchi wote.

Hilo suala lazima lifanyiwe kazi kama kweli wamepaka rangi ya bendera ya CHADEMA.
 
chadema na upinzani wenzie sasa wameamua kuficha maovu yao kupitia ukawa, kwanza itambulike kuwa meadi kama huo si wa CCm wala chama flani, hiyo ni mali ya wananchi kama wananchi..

chadeMA kama chadeMA kupiga chata ni dalili tosha kuwa, hawana uhakika na wanachofanya kwa wananchi!

poor fighting strategies!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom