Mbio Za Urais: Prof. Lipumba Anakuja, Na Chupa Ya Maji Mkononi! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbio Za Urais: Prof. Lipumba Anakuja, Na Chupa Ya Maji Mkononi!

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by maggid, Oct 17, 2010.

 1. m

  maggid Verified User

  #1
  Oct 17, 2010
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Na Maggid Mjengwa,

  MBIO za Urais zimeshika kasi. Media imekazana kuandika habari za JK na Slaa. Habari za CCM na CHADEMA. Kuna aliye kwenye mbio wanamsahau, kwa bahati mbaya au kwa makusudi. Ni Profesa Ibrahim Lipumba ( CUF).
  Katika wote wanaoshiriki mbio za Urais, Prof. Lipumba ndio mwenye uzoefu zaidi wa njia wanayokimbilia. Alianza mwaka 1995, ni kwenye uchaguzi mkuu wa kwanza wa vyama vingi.
  Alishiriki mdahalo wa kwanza wa wagombea urais. Ingawa, aliibuka wa pili kwenye mdahalo ule uliomwacha Ben Mkapa akiongoza na Mrema akiambulia nafasi ya tatu na John Cheyo akikamata mkia, bado Mashirika ya habari ya kigeni yalimpa Prof. Lipumba alama za juu zaidi.
  Lipumba ni mpiganaji mahiri. Mwaka 1995 aliingia kwenye mbio za Urais kama ' Profesa'. Hilo lilikuwa kosa, akalirudia tena mwaka 2000. Katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005, Profesa Ibrahim Lipumba alionekana zaidi kama ' Ibrahim Lipumba'. Profesa aliamua kushuka chini.
  Nakumbuka kukutana nae kwa mara ya kwanza mwezi kama huu, Oktoba 2005. Ni pale Isimila Hotel, Iringa. Ni Hotel ya kawaida kabisa. Rafiki yangu Saed Kubenea alikuwa kwenye msafara wa Lipumba na ndiye aliyefanya maandalizi ya mimi kukutana na Lipumba.
  Ilikuwa siku ya Alhamisi, nilifika pale Isimila Hotel kunako saa tatu asubuhi. Aliponiona, Profesa Lipumba alinijia akiwa mwingi wa tabasamu. " Kumbe, ndiye wewe Maggid!" Alitamka huku akionyesha furaha. Mkono wa kushoto alikamata jarida la Rai na chupa ya ‘Maji Afrika'. Saed Kubenea alisimama kando kupisha mazungumzo yetu.
  Nilimwona Profesa Lipumba kuwa ni mtu wa kawaida sana. Kuna wakati kwenye mazungumzo yetu tukiwa tumesimama alikuwa akipukuta vumbi kwenye suruali yake kwa kutumia gazeti la Rai. Lipumba anaongea kwa mpangilio na kwa kutulia. Kushiriki kwake katika uchaguzi wa 1995 na 2000 kumempa uzoefu zaidi katika kinyang'anyiro hiki. Lipumba ana uwezo na kipaji cha kufafanua mambo magumu yakaeleweka kwa mtu wa kawaida. Kuna wakati nilimsikia akitoa mfano wa ajira elfu moja zenye uhakika kwa vijana zinavyoweza kuathiri maisha ya mama mwuza vitumbua. Profesa Lipumba alitamka; " Ndugu zangu, bila ya vijana hawa kuwa na ajira na kipato , mama huyu atashinda na vitumbua vyake vikimtazama !."
  Hakika, Lipumba ana uwezo pia wa kutengeneza sentesi fupi na zenye kishindo; Msikilize anaposema; "Wananchi nikopesheni kura zenu, nitawalipa maendeleo!" Hizi ni baadhi tu ya nguvu za Ibrahimu Lipumba katika rethorik, sanaa ya kuzungumza.

  Ndio, Profesa Lipumba hata hii leo , bado yumo kwenye mbio za kusaka kura kwa wapiga kura wapatao milioni 19. Na Profesa Lipumba safari hii anaonekana kutumia mbinu za kijeshi zaidi. Anakwenda kwanza kule ambapo anaamini kuna matumaini ya kupata ushindi, matumaini ya kuvuna kura.
  Itakumbukwa, Lipumba alianza kampeni zake kwenye ‘ngome' ya CUF. Ni mikoa ya Kusini, Lindi na Mtwara. Huko Profesa ‘alipiga kambi'. Kama safari hii atatoka patupu hata kwenye ngome yake, basi, Profesa atalazimika kutafakari upya kama aendelee kuwapo kwenye uongozi wa juu wa CUF au awapishe wengine.
  Baada ya kule Kusini, tulimwona Profesa akichagua maeneo ya kwenda. Na kila alikokwenda kulikuwa ni kule ambako CUF imeonekana kuungwa mkono.
  Staili yake ya kampeni imebadilika pia. Profesa Lipumba wa leo, anavutia zaidi wasikilizaji na watazamaji. Lipumba haonekani sana juu majukwaani. Ameshuka chini, anaongea na wapiga kura akiwa karibu nao sana. Kila mahali anapofika, anaunganisha masuala makubwa na yale ya mahali hapo. Ameacha staili ya kutumia muda mwingi kukishutumu Chama Cha Mapinduzi. Profesa anasisitiza zaidi nini atakifanya, yeye na chama chake. Kile ambacho CCM wameshindwa kukifanya.
  Kabla ya mikutano ya hadhara, Profesa anafanya jitihada za kuikaribia jamii ya mahali hapo. Mathalan, atakwenda hospitali kuwaona majeruhi wa vurugu za vijana wa CCM na CHADEMA. ( Mara) . Akiwa hospitalini ataongea kuhusu umuhimu wa kushindana kwa hoja na si kupigana. Si profesa yule wa CUF ya ' Jino kwa Jino'. Na hatusikii siku hizi habari za ' Blue Guards'. Kama kutakuwa na habari za kontena lililosheheni visu kukamatwa na CUF ndio wakawa watuhumiwa, basi, habari hiyo itatiliwa mashaka na wengi.

  Profesa Lipumba atakwenda sokoni . Huko ataongea na wananchi, atauliza bei ya vyakula. Kule Musoma tukamwona Profesa akipima nguo kwa fundi cherehani, alitaka fundi huyo amshonee suti yake. Pale Bunda Lipumba akamtembelea nyumbani kwake Mzee Raphael, mwanachama wa CUF wa miaka mingi. Kule Geita tumemwona Lipumba akizungumza na wachimbaji madini wadogowadogo akiwa kwenye machimbo hayo.

  Ndio, tumemwona Lipumba akibeba mawe kuweka chini ya tairi na hata kusukuma gari kule Kondoa . Ni wakati msafara wake ulipokwama njiani. Tumemwona Lipumba akishiriki shughuli ya mazishi kule Mafia na Kagera. Kwamba kila anapokwenda kukampeni, Profesa Lipumba anatafuta habari kuhusiana na mahali hapo, ikiwamo na habari mbaya kama misiba. Kwenye misiba kuna wapiga kura.

  Hii nayo ni staili ya kampeni anayoionyesha Lipumba katika uchaguzi huu. Kushuka chini kwa watu. Mgombea usijikite tu kwenye kukusanya watu, unapaswa pia kuonekana iliko mikusanyiko ya watu. Nimepata kumwambia raia mmoja wa kigeni aliyeshangazwa na ratiba ya JK Mkoani Iringa, ratiba ambayo ilikuwa nyuma ya wakati kwa saa kadhaa. Nilimwambia; " In Africa, Presidential is Communal". Kwamba ' Afrika Urais ni jamii'. Mgombea urais ukiacha kusimama njiani kuongea na wanakijiji wanaokuomba ufanye hivyo. Sababu? Eti unawahi ratiba, basi, na kura zao kwako umeziacha pale pale.

  Tukirudi kwa Profesa Lipumba, bila shaka, Lipumba anajivunia pia nguvu za chama chake, CUF. Chama hiki kiliundwa Mei 28, 1992. Ni chimbuko la kuunganishwa kwa Chama cha kutetea haki za Wananchi (Civic Movement) kwa upande wa bara na chama cha KAMAHURU cha Zanzibar.
  CUF inatokana na vuguvugu la mageuzi nchini. Ingawa NCCR-mageuzi kilikuwa ni cha kwanza cha upinzani, CUF kilikuwa chama cha pili kusajiliwa katika mfumo wa vyama vingi baada ya CCM. Hii ilitokana na sura yake ya muungano kuonekana dhahiri. Hii ni moja ya nguvu kubwa za CUF. Hakuna anayejisumbua kuweka hadharani, ukweli kuwa, kwa sasa, CUF ni chama pekee cha siasa, chenye uhakika wa kuwa na wawakilishi bungeni kutoka Unguja, Pemba na Bara.
  Udhaifu wa CUF: Kama ilivyo kwa vyama vingine vya upinzani kama CHADEMA, bado hakijawafikia wapiga kura wengi vijijini, hususan bara. CUF ni chama pekee cha upinzani kilichokuwa na wabunge wengi katika bunge lililopita. Hivyo basi, kilipata ruzuku zaidi. Bado ni ajabu kuwa CUF imeshindwa kutumia ruzuku hizo kujitangaza na kujiimarisha zaidi bara.
  Hata hivyo, nguvu za CUF Zanzibar ni fursa kwa chama hicho kujiimarisha bara. Idadi kubwa ya wabunge wa CUF inaamanisha kiasi kikubwa cha ruzuku watachokipata. Ruzuku ikitumiwa vizuri inaweza kukikuza chama hata bara.
  Tishio. Tuhuma za kuwa CUF kinakumbatia uislamu ni tishio kwa chama hicho. CUF imegubikwa na wingu la mashaka ya baadhi ya Watanzania juu ya chama hicho na uislamu. Kimsingi tuhuma hizi dhidi ya CUF ni propaganda za kisiasa kutoka kwa wapinzani wa chama hicho. Hazina ukweli. Wanaokipiga vita chama hicho, hususan bara, wamefaulu kuipaka CUF rangi ya udini. Ni jukumu la CUF wakiongozwa na Mwenyekiti wao ( Taifa) , Profesa Lipumba, kujitetea na kujibu hoja hizi kwa vitendo, hivyo wakaeleweka na wapiga.


  mjengwa
   
 2. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #2
  Oct 17, 2010
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,839
  Likes Received: 11,959
  Trophy Points: 280
  Kama ameshikilia drip ya kwinini nitakuelewa.
   
 3. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #3
  Oct 17, 2010
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,050
  Likes Received: 3,958
  Trophy Points: 280
  Mjengwa unazigawanya kura za Kikwete maana masheik waliokacha shule walisema, "hawa wote ni wenzetu na ni bora tumpigie yule mwenye uhakika zaidi!! tafakari! mwenzenu kivipi?"
   
 4. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #4
  Oct 17, 2010
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,523
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Mjengwa. So what?
   
 5. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #5
  Oct 17, 2010
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135

  mjegwa then what? :A S 103:
   
 6. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #6
  Oct 17, 2010
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,365
  Likes Received: 7,000
  Trophy Points: 280
  kam huo ni mtazamo wako Mjengwa basi hilo litakuwa ni pigo kubwa sana kwa Chama chako cha CCM, kwa Muktasari/habari yako, CUF wana nguvu kusini hii ina maana watapata kura nyingi kusini, Chadema watachukua Mashariki, Nyanda za Juu na magahribi hapo pia CCM watapata kapa, tukija kanda ya Mashariki na kati patakuwa na furugu ya kugawana kura kati ya vyama vyote lakini kwa ujumla CCM na Chadema ndio watapambana sana, kufuatana na huo mgawanyiko wa kimazingira Chadema ndio wana Nafasi kubwa ya kushinda kwa idadi ya Kura zitakazo patikana Kaskazini, Nyanda za juu na Magharibi plus na hizo za mgawanyiko za Mashariki na kanda ya kati
   
 7. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #7
  Oct 17, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Mjengwa.
  umejenga hoja kwa Lipumba na jamaa zake lakini umeacha namna walivyoshiriki kuibaka demokrasia ktk uchaguzi mkuu wa CUF. Pia nashangaa unavyompromoti mtu ambaye miaka yooote anagombea tu wala hana dalili ya kushinda. Pia tafakari kuhusu yeye kama Lipumba angelikuwa fair kwa kukubali safari hii kuiunga mkono CHADEMA maana wao walimuunga mkono past chaguzis.

  Pia historia ya CUF imejaa uzandiki na hila. naamini wakumbuka walichomfanya muasisi wa chama hicho na mpaka wakamtoa nje kabisa. je hayo siyo historia ya kumpima Lipumba? Ktk mawazo yangu neno LIPUMBA maana yake ni Pumba kuuuubwa isiyo na maana yeyote
   
 8. Tusker Bariiiidi

  Tusker Bariiiidi JF-Expert Member

  #8
  Oct 17, 2010
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 4,753
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  CUF ni CCM B!
   
 9. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #9
  Oct 17, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  Hivi mjengwa hay ukiyaweka kwenye lie blog yako unaonaje
   
 10. George Maige Nhigula Jr.

  George Maige Nhigula Jr. Verified User

  #10
  Oct 17, 2010
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 470
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Ndugu Mjengwa,

  Nafurahi sana kwa kutumia muda wako kutuletea taarifa nzuri ya wasifu na historia ya Prof Ibrahim Lipumba, mimi mwenyewe binafsi, Lipumba has earned my respect and admaration kwa kujitahidi kupambana kuleta mabadiliko ya kudemokrasia na ushindani wa vyama vya siasa, hali kadhalika mchango wake katika maendeleo na mageuzi ya kiuchumi Tanzania wakati wa serikari ya awamu ya pili chini ya Raisi Mstaafu Alhaji Ali Hassan Mwinyi kama mshauri wake wa Mambo ya Uchumi, hali kadhalika mchango wake katika ujenzi wa uchumi wa Uganda kama personal advisor wa Raisi Yoweri Mseveni,

  Hali kadhalika kuna mapungufu fulani flani ambayo Prof Lipumba Kama Mwenyekiti wa Taifa wa CUF alibidi ayashughulikie na kuonesha nia ya dhati na utashi wa dhati wa kisiasa wa kutimiza ndoto za kuleta mageuzi na economic reforms kwa kuiondoa ccm Madarakani, Nimekuwa very disappointed na CUF na Prof Lipumba hususani kwenye uchaguzi wa mwaka huu pale CUF walipopatwa na kigugumizi cha kuunganisha nguvu na CHADEMA ili kuweza kufikia malengo ya kuleta mageuzi kwa kushika dola na kuuongoza serikari.

  Nadhani Majjid utakumbuka kuwa Chadema imekuwa na mkakati wa kuji imarisha kwanza na kuwa na reccord nzuri ya kuweza kuwaonesha wananchi na kuwashawishi kwa nini wanastahili kupewa dhamana ya kuongoza nchi yetu, na kazi hiyo chadema wameikamilisha kwa ufanisi mkubwa, mosi, CHADEMA hawakuwahi kukurupuka na kuweka mgombea wa uraisi huko nyuma kwa sababu walikubaliana na hali halisi ya kisiasa ya wakati huo hivyo basi walijitokeza hadharani kuunga mkono wagombea wa vyama vya upinzani waliokuwa na nguvu na nafasi ya kupata support kubwa ya wananchi, mwaka 1995 Chadema waliunga mkono NCCR-MAGEUZI na mgombea wao Ndugu Augustino Mrema,, hali kadhalika baada ya NCCR-MAGEUZI kushindwa kujiimarisha zaidi na kusambaratika, mwaka 2000, CHADEMA waliunga mkono CUF na mgombea wao Prof. Ibrahim Lipumba na Seif Sharif Hammad Kwa Zanzibar, Mwaka 2005 CHADEMA hawakuona haja ya kuendelea kuunga mkono vyama vingine hivyo wakaamua kusimamisha mgombea wa uraisi ili kupata fursa ya kukitangaza chama na kupata wabunge, lakini waliendelea kuunga mkono CUF upande wa ZNZ,

  Ufanisi na umakini wa wabunge wa chadema bungeni umewapa hamasa wananchi wengi kutambua umuhimu wa kuwa na wabunge wengi wa upinzani bungeni, hivyo basi chadema wamepokelewa vyema na wanachi wengi kutokana na mchango wao katika masuala mengi muhimu yanayohusu maslahi ya Taifa, na hilo limefanikiwa kutokana na ushirikiano mzuri wa kiongozi wa upinzani bungeni, RASHID MOHAMED na msaidizi wake DR. SLAA.

  Hivyo basi kitendo cha CHADEMA kumpitisha Dr Slaa kama mgombea wa Uraisi ilikuwa ni mafanikio makubwa sana kuleta upinzani na hamasa kwa uchaguzi wa mwaka huu, kwani ni ukweli ulio wazi kuwa Dr Slaa amewapa changamoto kubwa chama Tawala na ana nafasi kubwa ya kuibuka mshindi kama uchaguzi utakuwa huru na wa haki, hivyo kama CUF na Prof Lipumba walikuwa watu makini, kulikuwa na umuhimu mkubwa wa kumuunga mkono mgombea wa chadema kwa nafasi ya uraisi na kuingia mkataba na CHADEMA kuhusu mgawanyo wa kusimamisha wabunge majimboni, hali kadhalika, mgawanyo wa ruzuku, hili ni swala ambalo linawezekana kufanyika na kupata ushindi wa bila jasho kubwa, kwani Prof Lipumba amekuwa akigombea Uraisi kwa vipindi vitatu mfululizo bila mafanikio makubwa na hii ni awamu ya nne na bado hana nafasi ya kushinda hivyo angekuwa mtu mwenye utashi wa kweli wa kisiasa angeweza kulipa fadhila kwa chadema na kukubali hali halisi ya kisiasa nchini, but that is not the case kwa CUF na Prof. Lipumba.

  Hivyo basi inanipa wasiwasi kama CUF au Prof Lipumba wana nia ya dhati ya kupata nafasi ya kuindoa CCM madarakani na kuunda serikari ya Jahmuri wa Muungano wa Tanzania, ijapokuwa nimekwisha wahi kuona tamko la Prof Lipumba hapo awali kuwa ameshindwa kutoa support kwa Dr Slaa eti kwa sababu alichelewa kutangaza nia ya kugombea! ijapokuwa alimwagia sifa Dr. Slaa kuwa ni mzalendo wa kweli na amefanya mambo makubwa kwa taifa, lakini hiyo statement ilikuwa ya kiungwana ijapokuwa swala la kuunganishaa nguvu lilikuwa ni muhimu sana hata sasa hivi ampapo bado kuna mda wa kufanya hhivyo baada ya kuona kukubalika na nafasi kubwa ya Dr Slaa kushinda.

  Hivyo naona kama Prof Lipumba amepoteza mweleekeo wa chama chake hapo baadae kwa kushindwa kutambua alama za nyakati na kuwa seheemu muhimu ya mabadiliko ambayo watanzania tumeyasubili kwa mda mrefu sasa, hivyo Bwana Majjid ningependa uweze kuwasilisha kilio changu kwa Prof Lipumba kuwa ule umakini na umaarufu wake unapotea kabisa kutokana na kuanza kuingiwa na ubinafsi na kuupuza hali halisi ya kisiasa.

  Hali kadhalika Ningependa kutoa ombi raisi kwa Raisi wwetu mtarajiwa DR. WILBROAD PETER SLAA kuwa baada ya kushinda uchaguzi huu tunahitaji kutumia taaluma ya Prof Lipumba hivyo you can still reach out to him post election na kujua kama anaweza ku play a role kama waziri wako wa FEDHA NA UCHUMI, hali kadhaliko kuna watu wazuri CUF ambao they can do good things for this country kama RASHID Mohammed na Juma Haji Duni, Dr. Slaa anaweza kuwafikiria kuwapa baadhi ya wizara ili tuweze kutumia mchango wao kwa maslahi ya Taifa, Kwani ni kawaida ya Chadema kuzingatia maslahi ya Taifa kwanza kabla ya maslahi ya chama.
   
 11. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #11
  Oct 17, 2010
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,050
  Likes Received: 3,958
  Trophy Points: 280
  Inahusiana vipi na habari ya hii article yako? waandishi wengine ni udini na njaa tu vinawashushua au unataka tuanze kuchunguza hayo maji ya Africa na hilo gaezeti la Rai ni vya nani?
   
 12. WABUSH

  WABUSH JF-Expert Member

  #12
  Oct 17, 2010
  Joined: Oct 14, 2010
  Messages: 285
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyo ndiye Mjegwa!! Msome kwa makini.....
   
 13. Butola

  Butola JF-Expert Member

  #13
  Oct 17, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,221
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Mkuu usiende huko,hakuna chama kilicho kisafi katika hilo.
   
 14. Kunta Kinte

  Kunta Kinte JF-Expert Member

  #14
  Oct 17, 2010
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 3,660
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Du! kaaazi kweli kweli!
   
 15. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #15
  Oct 17, 2010
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Heshima kwako Maggid,

  Binafsi nakubaliana na sehemu kubwa ya wasifu na uzoefu wa muda mrefu wa Prof I Lipumba.Mkuu Maggid Prof Lipumba ameshindwa kabisa kukifanya chama cha CUF kionekane kama chama cha kitaifa.ajenda kuu ya CUF ni kushinda Zanzibar na hata wanapotekea wanasiasa wazuri Tanzania bara wanaminywa sana ili ajenda ya Zanzibar isife.Wapo wanachama wazuri waliotaka kuifanya CUF ijikite Tanzania bara wakaishia kuondolewa kwenye nafasi za juu mfano mzuri ni Bwana Lwakatare alijitahidi kuipeleka CUF kanda ya ziwa na sehemu nyingine Tanzania bara.

  Uongozi wa juu CUF ni wazanzibar na unahakikishiwa ndani ya katiba yao lazima uendelee kubaki hivyo.Matokeo yake CUF inakosa nguvu Tanznaia bara yenye watu milioni 40 na kujikita kwenye siasa za watu milioni 1.Nimeshindwa kupata mantiki ya kisayansi inakuwaje chama chenye Prof mashuhuri na mwenye kuheshimika kimataifa ashindwe kubaini kwamba CUF lazima iwekeze sana Tanzania bara ili siku za usoni ishike dola [serekali]
   
 16. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #16
  Oct 17, 2010
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280

  Heshima kwako Msanii,

  Nitajie chama kilicho na demokrasia Tanzania !.
  CHADEMA walifanya uchaguzi akajitokeza Zitto kugombea nafasi ya uenyekiti taifa yaliyompata kila mmoja wetu anajua.
   
 17. Peasant

  Peasant JF-Expert Member

  #17
  Oct 17, 2010
  Joined: Sep 27, 2007
  Messages: 3,949
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ukiona hivyo ujue hiyo blog yake imechemsha sana, labda imejaa udaku mtupu na hakuna objective thinking.
   
 18. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #18
  Oct 17, 2010
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Hivi Maggid ana blog naye? This is a piece of information to me
   
 19. Mlalahoi

  Mlalahoi JF-Expert Member

  #19
  Oct 17, 2010
  Joined: Aug 31, 2006
  Messages: 2,065
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Alright.Chama kilicho na demokrasia Tanzania ni CCM pekee.Isn't that what you wanted to hear?
   
 20. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #20
  Oct 17, 2010
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,565
  Likes Received: 1,652
  Trophy Points: 280
  "Kimsingi tuhuma hizi dhidi ya CUF ni propaganda za kisiasa kutoka kwa wapinzani wa chama hicho. Hazina ukweli. Wanaokipiga vita chama hicho, hususan bara, wamefaulu kuipaka CUF rangi ya udini. Ni jukumu la CUF wakiongozwa na Mwenyekiti wao ( Taifa) , Profesa Lipumba, kujitetea na kujibu hoja hizi kwa vitendo, hivyo wakaeleweka na wapiga."

  HUYU JAMAA BWANA BARA NDIO NANI SASA SI USEME TU NI CCM! AU UNAJIFANYA HUJUHI NANI ANAYE ENEZA UDINI?
   
Loading...