Wana JF Salamu sana.
Wakati wa kampeni zake za kuingia ikulu JK aliahidi maji na umeme kwenye kijiji kimoja kilichopo mkoa wa pwani.
Kweli ikatangazwa tenda akapatikana mkandarasi. Mchakato ukaanza na kazi imefikia mwishoni mwishoni.
Maajabu yaliyopo ni kwamba lile tenk kubwa la kupokelea maji ili yasukumwe kwa wanakijiji limepakwa rangi za Chadema.
Ina maana rais atakapoenda kufungua hayo maji atakuwa anazindua mradi wenye rangi za Chadema.
Kwenye kuuliza kilichosababisha kufikia huku hakuna anayefahamu.
Hivi nyie viongozi tokea shina hadi serkali kuu inakuwaje hata msitupie macho kwenye miradi mikubwa kama hii?
....... nyie waosha vinywa matusi sitaki. ............