Baada ya kusikiliza taarifa mbalimbali na kusoma sources mbalimbali naona sasa ugumu wa hii vita. Dalili zinaonesha kuwa serikali ya shirikisho ya Comoro na rais wake Ahmed Abdallah Mohamed Sambi inaungwa mkono na Iran. Hii inanisaidia kuelewa kwa nini Libya, Sudan zimekuwa mstari wa mbele kuunga mkono uvamizi wa Anjouan, wakati South Africa (waungaji wa Marekani na Uingereza) anapinga. AU imeingizwa mtegoni hapa, na hii vita ni ngumu. Bila shaka huyu Col Mohamed Bakar anapata kiburi chake kutoka kwa wanaowapinga washirika wa Sambi (hasa Iran), sitashangaa Marekani ikawa upande wa Bakar (by proxy, hawatasema kwenye vyombo vya habari, lakini wanayo kwenye sera kutokana na maelewano yao mabaya na Iran). Tanzania ndio tuko pagumu zaidi, maana Bush tuko naye, na Ahmadinejad pia tuko nae. Kazi ipo!
Huyu Wangwe alishaniboa mimi, hivi kasoma Katiba? Rais ana madaraka yote ya kupeleka majeshi yetu mahali popote na hahitaji kibali cha Bunge! Siyo vizuri yes, ndivyo katiba ilivyo absolutely.. akitaka aanzishe kelele za kutaka mabadiliko ya Katiba. Vinginevyo, ni bora kukaa kimya kuliko kuzungumzia kitu ambacho mtu hujui.
We are in trouble as a country when it comes to leadership. Kwa mtu mwenye mamlaka makubwa kwa kiwango chake ungetegemea aonyeshe umakini. But you know what, TZ tunaamini viongozi huzaliwa na sio lazima watengenezwe. I imagine mtu kama huyo angepata angalau semina ya leadership for few days baada ya kuchaguliwa naamini angeweza kuwa makini zaidi. Halafu jambo zito kama hili la jeshi utakubalije kuongea kabla hujajiridhisha kwamba unachoongea unakielewa. Ndo hapa nasema tumegeuza siasa zetu kuwa club za mabishano, unabishia tu jambo madamu uonekane wewe upo upande mwingine. Tuna shida kuliko tunavyojijua!
Lunyungu muda mfupi maana yake nini? Am dying for the news jamani!Nitawapa habari zaidi muda mfupi ina hali ni mbaya sana jamani .
Field Marshall,Mkuuu Icadon,
Wewe ninakuaminia na nyeti za hii operation, endelea kutuletea vitu vya uhakika mkuu!
Field Marshall,Mkuuu Icadon,
Wewe ninakuaminia na nyeti za hii operation, endelea kutuletea vitu vya uhakika mkuu!
Field Marshall,
hata mimi nimeridhika sana na upashaji habari wa Icadon na analysis zake za mambo ya kijeshi. Lakini amekataa mapendekezo yangu ya kumpandisha cheo. Ananikumbusha wamamuziki fulani wa Jeshi la Kenya, nadhani wa Them Mushrooms waliokataa kupandishwa vyeo wakihofia upigaji muziki usingewezekana tena!
I am not a supporter of CCM and its government BECAUSE OF CORRUPTION AND MISMANAGEMENT. But credibility should be accorded where it is due. I fully support this mission huko Comoro. Hivi wananchi wenzangu mnaposema African problems for African solutions, mna maana gani? who are the Africans? au ulitegemea wazungu waje kufa huko eti wanapigania waafrica? Hii mission ina baraka zote za AU, TZ na wenzake hawajavamia illigally. So I think Membe is very right in what is doing as our foreign policy chief!
Saa na wakati huu vikosi vya majeshi ya Jumuiya ya Afrika vimeanza mapambano ya kukikomboa kisiwa cha Anjouan ili hatimaye kurudi katika shirikisho la Comoro.
Vikosi hivyo vikiongozwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania wanashiriki katika Operesheni Demokrasia Komoro yenye lengo la kumuondoa Rais aliyejipachika Bw. Mohammed Bacar.
Hivyo saa na wakati kama huu ambapo vijana wetu wako katika hali ya hatari na ambapo wanayaweka maisha yao hatarini ni kitendo cha kutokuwajibika kwa baadhi ya wanasiasa kudai kuwa Rais amevunja Katiba wakati kipengele wanachokinukuu hakihusiki na mapigano haya.
Kitendo cha kutumia mapigano hayo kujipatia pointi za kisiasa nakipinga na kinaonesha ni jinsi gani baadhi ya wanasiasa hawajui Katiba lakini wakati wanajeshi wetu wako kwenye mapigano wao wanaongoza jitihada za kuwavunja moyo.
Kama raia wa Tanzania naomba nitumie nafasi hii kutuma salamu za ushindi kwa Jeshi la Wananchi, kwa Amiri Jeshi Mkuu na kwa makamanda na wapiganaji wote huko Comoro ili hatimaye wafanye kazi tuliyowatuma kwa haraka, ufanisi na kuhakikisha kuwa maisha ya raia yanalindwa kwa kiasi chote kinachowezekana.
Saa na wakati kama huu, hakuna Chadema, CUF, CCM au SAUT Tanzania ni moja na hatima yake ni moja, na ni jukumu la kila raia kusimama na kutakia ushindi vikosi vyetu na haya mambo ya kulalamika yaje baadaye siyo wakati risasi zinarushwa.
Kwa jeshi letu, USHINDI NI LAZIMA!
Mungu Ibariki Tanzania,
Mungu Ibariki Afrika.
NB: Kwa matangazo yangu ya leo tembelea http://www.klhnews.com na usisahau kutumia search injini yetu pale.
Title: KLH News Episode: Operesheni Demokrasia Comoro - Wangwe angekaa kimya!
http://mwanakijiji.podOmatic.com/entry/eg/2008-03-24T22_32_09-07_00