Majeruhi wa valentine

Valentine Day=Siku ya waachanao, na kuna series ya watu pia walikosa vyumba kitaa, these are also victims!!

Na wale waliosikia huu mlio..."the number you are tryng to call is switched off/not reachable."..saa 2, saa 3,..5...8...12...1 usiku..hadi 6 usiku same answer, are also victims...Hawa nao wajitokeze hapa!!
 
Leo siku ya kufungua mabox ya valentine.(boxing day). Najua wengi wana maumivu sana saaaaana, zaidi nawahurumia wale waloamua jana kuupoteza ubikra wao wakidhani ni siku sahiihii halafu wakaachwa leo asubuhi.
 
sasa bana kwenye redio station moja jana walikuwa wanatoa "free divorce" nikimaanisha
watalipa kila kitu kuanzia lawyer na kila kitu ambacho unatakiwa ulipe wakati mnapena talaka.

hiyo competition ilikuwa wiki nzima watu wengi kweli waliingia kushindana..
akachaguliwa mshindi mmoja jana siku ya valentine . the catch was unatakiwa
umpigie mpenzi wako simu siku hiyo ya vallentine na kumwambia kuhusu divorce na
umuache mume au mkeo wakati kila mtu anakusikiliza kwenye redio..

Kasheshe mpauko.
akachaguliwa dada mmoja aliejitambulisha kwa jina la Sam au Samather .
huyo dada akasema anataka kuacha na mume wake sababu kibao .. mpaka
dakika za mwisho anaulizwa bado unataka kumpigia mumeo simu na kuachananae
wakati kila mtu anakusikiliza.. ?? dada anasema ndio bila hata mashaka..

Muda wenyewe..
muda ulipofika hao watangazaji wa redio wakampigia simu huyo mumeo simu ilioita
akapokea mwanamke mwingine.. hao watangazaji wakamuomba huyo mwanamke waongee na mume wa Sem..
huyo mdada akasema yeye ndo mume wa Sem.. kilichofuata hapo ni cosovo nato.. hawa watangazaji waliumbuliwa
na hao ma lesbian mbele ya kila mtu aliekuwa anasikiliza. walikuwa hawataki kuachana bali walitaka tu kuwachamba
na kuwaumbua hawa watangazaji kwa walivyokuwa wanasisitiza hayo mambo....

Kwa anae taka kusoma zaidi habari yote hapo chini ..
Lesbian couple prank The Rock’s pranksters | Express Online
 
Nimeamini kuwa mapenzi bila pesa siku hizi hayaendi,heri kwa wazazi wetu ambao walipendana zamani na hakukuwa na mambo mengi ambayo yanataka utumie pesa katika kufanikisha mapenzi tofauti na sasa.
 
Kuna kijana jana ka wini lakini kwa kulazimisha, aliomba ruhusa kazini lakini hakumwambia mchumba wake na mipango ya kesho yake ilikuwa inaanzia jioni. Ila lengo lake lilikuwa akipigwa chenga aifuate huko huko. Asubuhi katumiwa message kuwa dia unatoka saa ngapi kazini kijana kajibu kumi na moja akasema aaa kumbe nitawahi mama kasema nimsindikize kwa rafiki yake Mkuranga, kijana akamwambia mnaondoka saa ngapi? akasema saa nne asubuhi. jamaa si alikuwa mitaaani saa nne akaenda nyumbani na corolla yake akamkuta mama na vikazi vya hapa na pale mrembo kajikoki kwa ajili ya kutoka. Sasa kijana akamwambia mama nimekuja kuwasindikiza Mkuranga, mama akasema mkuranga kuna nini? Binti akaanza kusema mama umesahau ee basi usiwe unaniambia safari zako. jamaa akajua jibu lake. Hakukata tamaaa akamchukua mpaka usiku harafu akamwambia mahusiano yao ndo yameisha.
Sasa yule dada kumsingizia mama yake ndio nini? na kama safari mama alikuwa haijui yeye mbona alishavaa ayari kwa safari?
 
Nimeamini kuwa mapenzi bila pesa siku hizi hayaendi,heri kwa wazazi wetu ambao walipendana zamani na hakukuwa na mambo mengi ambayo yanataka utumie pesa katika kufanikisha mapenzi tofauti na sasa.
ulikubwa na nini mpaka useme hivi?
 
Mi ni mmoja kati yao. Niliekua namtegemea alipotea kabisa
Nimeshinda na nguo yangu ya red, makeup ikaharibika yote kwa machozi,
Nikiangalia JF namuona full kujiachia tu! ... Imeniuma sana...
Valentine's day SUKS!!!
 
Back
Top Bottom