Ndugu zangu kuna mgogoro wa ardhi unaondelea hivi sasa maeneo ya Majoe na mtu anayedai kwemba hilo ni eneo lake. Mwanzoni mwa mwezi huu zaidi ya nyumba 48 wakazi wake walitolewa kwenye nyumba zao kwa amri ya Mahakama ilihali kesi ya msingi bado ipo Mahakamani.
Wananchi wamekosa kabisa ushirikiano toka Serikalini na vyombo vya dola. Muhusika amezungushia mabati kwenye hilo eneo na kuweka walinzi. Cha kushangazi siku 3 zilipopita uongozi wa Majembe kwa kushirikiana na walinzi waliowaweka wameiba madirisha ya aluminium kwenye baadhi ya nyumba.
Polisi walikwenda kwenye eneo la tukio na kuwakuta walinzi lakini hakuna hatua zozote zile zilizochukuliwa. Polisi wanakataa kuwaruhusu wananchi kwenda kwenye nyumba kuangalia uharibifu uliofanywa. Kesi inaunguruma tena kwa hati ya dharura Jumatano wiki ijayo.