DOKEZO Majembe Auction Mart waiba madirisha Majohe

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Acha kabisa yani mtaani kwetu kuna mmoja anadai eneo lote la mtaa wetu ni lake( ni makazi mapya) enzi za Magu alipoleta za kuleta akazimwa akatulia tuliii, baada ya kifo cha Magu tu alitoka kama umeme kalianzisha upya na wakati mpaka kesi alifuta mwenyewe
Wakati mwingine huwa sielewi
Hao watu wanakuwaga wapi mpaka watu wanajenga kunahamiwa halafu baadae wanasema maeneo ni yakwao??
Why wasijitokeze awali kabisa wanapoona watu wanaanza kupaendeleza??
Yaani watu wajenge wahamie pageuke mji halafu unakuja kusema ni eneo lako unakuwa wapi muda wote huo hayo yakifanyika.
 
Mimi nachojua, ukiwa na mgogoro wa ardhi na mtu binafai, inawezekena kuzungumza nje ya mahakama. Ni serikali tu ndio huwa inatumia nguvu kubomoa nyumba za watu hata kama kesi ipo mahakamani, au hata kama raia wana haki.

Sasa hao raia wasiwe wabishi, wajaribu kuzungumza nje ya mahakama ili waachiwe nyumba zao.

Hali nayoiona hapa, inawezekena hilo eneo ni la asili la huyo bwana, lakini hakuwepo miaka mingi, hivyo kuna watu ambao ni wenyeji wa huko (majirani) wakalivamia na kuanza labda kulima au shughuli mbalimbali.

Baadae, hao wavamizi wenyeji wakaanza kuuza viwanja kwa wageni. Wageni wakanunua bila kujua.

Mmiliki halali wa asili karudi kaanza kudai eneo. Kilichotakiwa hapa ni wavamizi kukubali matokeo wamlipe huyo jamaa kama kweli eneo ni la asili la huyo jamaa.

Kama eneo ni la asili la huyo bwana, atashinda tu mahakamani! Mana anaweza kuleta mashahidi wazee wa miaka hiyo enzi za kijiji ambapo wanamfahamu hadi babu yao. Je, hao wavamizi wakiulizwa hapa alikuwa analima mzee nani watajua?

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
Haya mambo ya ardhi ni mtihani Sana

Nakumbuka huko maeneo ya kerege bagamoyo,wananchi WA pale walivamia maeneo ya watu,tukapewa taarifa maeneo yanauzwa,Mimi na mke wangu na baadhi ya wadau tukajichanganya tukanunua, nakumbuka tulinunua viwanja viwili na wife kama 2,000,000/=

Daah baadae mwenyewe karudi,ikajulikana wananchi wamevamia eti kisa mwenyewe hakuwepo Muda mrefu,hakukuwa na namna zaidi ya kupoteza hela.

Tukafungua kesi dhidi ya waliotuuzia tukaenda nayo,si unajua danadana za mahakama tena,mara jaji kaenda likizo mara kurushwa tarehe,tukaona isiwe tabu tutakuja kulipana katika mahamaka ya Allah
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom