DOKEZO Majembe Auction Mart waiba madirisha Majohe

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

viking

JF-Expert Member
Aug 23, 2012
2,123
1,269
Ndugu zangu kuna mgogoro wa ardhi unaondelea hivi sasa maeneo ya Majoe na mtu anayedai kwemba hilo ni eneo lake. Mwanzoni mwa mwezi huu zaidi ya nyumba 48 wakazi wake walitolewa kwenye nyumba zao kwa amri ya Mahakama ilihali kesi ya msingi bado ipo Mahakamani.

Wananchi wamekosa kabisa ushirikiano toka Serikalini na vyombo vya dola. Muhusika amezungushia mabati kwenye hilo eneo na kuweka walinzi. Cha kushangazi siku 3 zilipopita uongozi wa Majembe kwa kushirikiana na walinzi waliowaweka wameiba madirisha ya aluminium kwenye baadhi ya nyumba.

Polisi walikwenda kwenye eneo la tukio na kuwakuta walinzi lakini hakuna hatua zozote zile zilizochukuliwa. Polisi wanakataa kuwaruhusu wananchi kwenda kwenye nyumba kuangalia uharibifu uliofanywa. Kesi inaunguruma tena kwa hati ya dharura Jumatano wiki ijayo.
 
sajo

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
1,850
2,598
Mwanzoni mwa mwezi huu zaidi ya nyumba 48 wakazi wake walitolewa kwenye nyumba zao kwa amri ya Mahakama ilihali kesi ya msingi bado ipo Mahakamani.
Sasa hapa kuna shida gani ikiwa amri ilitolewa na mahakama? Mna shaka na amri hiyo? Iweke tuione

Kesi inaunguruma tena kwa hati ya dharura Jumatano wiki ijayo.
Ni kesi namba ngapi na ipo mahakama ipi kwa mwenyekiti au jaji nani?
 
njumu za kosovo

JF-Expert Member
Mar 9, 2017
1,049
2,018
Watu wenye nguvu ya fedha wamerudi kwa kasi mno kwenye hii awamu ya sita. Tusubiri tuone mahakama itaamua nini.
Acha kabisa yani mtaani kwetu kuna mmoja anadai eneo lote la mtaa wetu ni lake( ni makazi mapya) enzi za Magu alipoleta za kuleta akazimwa akatulia tuliii, baada ya kifo cha Magu tu alitoka kama umeme kalianzisha upya na wakati mpaka kesi alifuta mwenyewe 😔😔
 
KijanaHuru

JF-Expert Member
Jan 7, 2017
1,825
2,236
Mtu unamiliki eneo haulipii kodi na unajiona kama ardhi ni ya kwako? Walishaambiwa toeni pesa kidogo kidogo niwaachie maeneo maana mmejenga tayari mliuziwa bila kujua wakajifanya kichwa ngumu wakagoma kutoa pesa wakidhani watashinda.

Mwenye eneo hata hajatumia pesa yoyote zaidi ya umiliki halali kabisa, tatizo watanzania tuko hivi ukiwa unaona upo na nafasi hakuna anayekugusa unavimba sana hata kama haki si ya kwako, ukishaguswa pabaya ndio unajikuta sasa unajua kuitafuta haki kwelikweli.

Serikali sio bibi ya mtu mwenye eneo analipia kodi ya ardhi hata kabla hilo eneo watu hamjaanza kujenda
Kama madirisha hayapo ni eneo lake wala hajaiba ni haki yake kuuza au kubomoa au kufanya lolote ndio maana waliambiwa tokeni na vyombo vyenu tu.

Mbona ambao walitoa pesa na kumpa mwenye eneo mbona hawakuondolewa?

Lingine watanzania tujifunze kufuata kanuni tunapofanya manunuzi hasa ardhi sio ununue kienyeji tu hakikisha ardhi wamekuja kupima na kusajili eneo lako.

Unapozidi kukwepa gharama ndogondogo ndio unavyojiumiza zaidi nk
 
KijanaHuru

JF-Expert Member
Jan 7, 2017
1,825
2,236
Sasa hapa kuna shida gani ikiwa amri ilitolewa na mahakama? Mna shaka na amri hiyo? Iweke tuione

Ni kesi namba ngapi na ipo mahakama ipi kwa mwenyekiti au jaji nani?
Acha wakome walijua watashinda kesi wakati hata ardhi huko hawatambulikani, yaani mtu una hati uchwara umeandikishana na mwenyekiti sijui na mwenzako analipa kodi ya ardhi toka miaka hiyo na unategemea ushinde kesi kweli?
 
Mpetde

JF-Expert Member
Sep 5, 2022
1,081
1,267
Acha kabisa yani mtaani kwetu kuna mmoja anadai eneo lote la mtaa wetu ni lake( ni makazi mapya) enzi za Magu alipoleta za kuleta akazimwa akatulia tuliii, baada ya kifo cha Magu tu alitoka kama umeme kalianzisha upya na wakati mpaka kesi alifuta mwenyewe 😔😔
Na soon mnaenda kuporwa hilo eneo, si ushasikia mnapenda bure? Sasa yeye ataenda kutandaza vibunda kuanzia mlinzi wa mahakama hadi hakimu, mna chenu hapo? Ridhimoko naibu wa land mtaporwa hadi mfe, yule Jamaa alieporwa ghorofa kariakoo umemsahau?

Kuna wale wameporwa eneo la msikiti Mwenge ukavunjwa yakajengwa maduka frem za Biashara unamkumbuka?
 
Mpetde

JF-Expert Member
Sep 5, 2022
1,081
1,267
mtu unamiliki eneo haulipii kodi na unajiona kama ardhi ni ya kwako?
Walishaambiwa toeni pesa kidogo kidogo niwaachie maeneo maana mmejenga tayari mliuziwa bila kujua wakajifanya kichwa ngumu wakagoma kutoa pesa wakidhani watashinda,
Mwenye eneo hata hajatumia pesa yoyote zaidi ya umiliki halali kabisa,
Tatizo watanzania tuko hivi ukiwa unaona upo na nafasi hakuna anayekugusa unavimba sana hata kama haki si ya kwako,
Ukishaguswa pabaya ndio unajikuta sasa unajua kuitafuta haki kwelikweli
Serikali sio bibi ya mtu mwenye eneo analipia kodi ya ardhi hata kabla hilo eneo watu hamjaanza kujenda
Kama madirisha hayapo ni eneo lake wala hajaiba ni haki yake kuuza au kubomoa au kufanya lolote ndio maana waliambiwa tokeni na vyombo vyenu tu.

mbona ambao walitoa pesa na kumpa mwenye eneo mbona hawakuondolewa?

Lingine watanzani tujifunze kufuata kanuni tunapofanya manunuzi hasa ardhi sio ununue kienyeji tu hakikisha ardhi wamekuja kupima na kusajili eneo lako,
Unapozidi kukwepa garama ndogondogo ndio unavyojiumiza zaidi nk
Hilo eneo lipo mpigi magoe au majoe? Unajua mleta mada anachanganya hakuna mpigi majoe ila kuna majoe ya pugu
 
KijanaHuru

JF-Expert Member
Jan 7, 2017
1,825
2,236
*************
Hilo eneo lipo mpigi magoe au majoe? Unajua mleta mada anachanganya hakuna mpigi majoe ila kuna majoe ya pugu
Majoe ni kama unaenda viwege njiani
Ukifika pugu sekondari unapoenda chanika unachepuka kushoto na moja kwa moja unaenda huko
 
mapesa yamejaa

JF-Expert Member
Dec 29, 2021
667
1,539
Wananchi mkishirikiana huyo mmiliki uchwara hatawafanya lokote.Tumieni hata nguvu kumuondoa.haiwezekani mtaa mzima auhamishe na kwa nini mwanzo hakuwazuia?serikali ya huyu bibi imekuwa ya hovyo sana,wananchi tujiokoe na tuchukue hatua wenyewe
 
ETUGRUL BEY

JF-Expert Member
Aug 6, 2020
1,650
2,695
Mtu unamiliki eneo haulipii kodi na unajiona kama ardhi ni ya kwako? Walishaambiwa toeni pesa kidogo kidogo niwaachie maeneo maana mmejenga tayari mliuziwa bila kujua wakajifanya kichwa ngumu wakagoma kutoa pesa wakidhani watashinda.

Mwenye eneo hata hajatumia pesa yoyote zaidi ya umiliki halali kabisa, tatizo watanzania tuko hivi ukiwa unaona upo na nafasi hakuna anayekugusa unavimba sana hata kama haki si ya kwako, ukishaguswa pabaya ndio unajikuta sasa unajua kuitafuta haki kwelikweli.

Serikali sio bibi ya mtu mwenye eneo analipia kodi ya ardhi hata kabla hilo eneo watu hamjaanza kujenda
Kama madirisha hayapo ni eneo lake wala hajaiba ni haki yake kuuza au kubomoa au kufanya lolote ndio maana waliambiwa tokeni na vyombo vyenu tu.

Mbona ambao walitoa pesa na kumpa mwenye eneo mbona hawakuondolewa?

Lingine watanzania tujifunze kufuata kanuni tunapofanya manunuzi hasa ardhi sio ununue kienyeji tu hakikisha ardhi wamekuja kupima na kusajili eneo lako.

Unapozidi kukwepa gharama ndogondogo ndio unavyojiumiza zaidi nk
Kama unayosema haya ni sahihi basi mwenye eneo alikuwa fair sana,kile kitendo cha kuwapa Mda wamlipe hela kidogo kidogo alionyesha big love Kwa wadau.

Ingawa wadau wakajifanya kukomaa wakati eneo sio Lao.

Anyways kubwa ni huyo bwana aendelee kuwa fair awape Mda maalum walipe,then kama mtu hatatimiza Hilo automatically waondolewe
 
macho_mdiliko

JF-Expert Member
Mar 10, 2008
17,177
26,454
Watu wenye nguvu ya fedha wamerudi kwa kasi mno kwenye hii awamu ya sita. Tusubiri tuone mahakama itaamua nini.
Haki ya nani nchi ina raia wa ajabu kweli kweli. Tumezoea kufanyiwa kila kitu. Nchi inaporwa na na mafisadi kila kona halafu raia tunasema ''tusubiri mahakama''. Tutasubiri sana. Yaani hata siku moja hatujisikii kutetea haki zetu jamani? Badala yake tunataka kufanyiwa kila kitu wakati sisi tumekaa kama mawe? Hizi mahakama mnazijua?
 
KijanaHuru

JF-Expert Member
Jan 7, 2017
1,825
2,236
Kama unayosema haya ni sahihi basi mwenye eneo alikuwa fair sana,kile kitendo cha kuwapa Mda wamlipe hela kidogo kidogo alionyesha big love Kwa wadau.

Ingawa wadau wakajifanya kukomaa wakati eneo sio Lao.

Anyways kubwa ni huyo bwana aendelee kuwa fair awape Mda maalum walipe,then kama mtu hatatimiza Hilo automatically waondolewe
Aliwapa muda walileta kichwa ngumu wachache sana ambao walitoa kidogo hata kama hawakumaliza kawaachia maeneo kabisa,
na shida ya hawa ambao walikuwa hawalipi ndio waliuwa kidedea kukomaa na mahakama wakajua sijui sheria inaonea watu huruma
 
Umkonto

JF-Expert Member
Dec 27, 2018
1,126
1,757
Aliwapa muda walileta kichwa ngumu wachache sana ambao walitoa kidogo hata kama hawakumaliza kawaachia maeneo kabisa,
na shida ya hawa ambao walikuwa hawalipi ndio waliuwa kidedea kukomaa na mahakama wakajua sijui sheria inaonea watu huruma
Mimi nachojua, ukiwa na mgogoro wa ardhi na mtu binafai, inawezekena kuzungumza nje ya mahakama. Ni serikali tu ndio huwa inatumia nguvu kubomoa nyumba za watu hata kama kesi ipo mahakamani, au hata kama raia wana haki.

Sasa hao raia wasiwe wabishi, wajaribu kuzungumza nje ya mahakama ili waachiwe nyumba zao.

Hali nayoiona hapa, inawezekena hilo eneo ni la asili la huyo bwana, lakini hakuwepo miaka mingi, hivyo kuna watu ambao ni wenyeji wa huko (majirani) wakalivamia na kuanza labda kulima au shughuli mbalimbali.

Baadae, hao wavamizi wenyeji wakaanza kuuza viwanja kwa wageni. Wageni wakanunua bila kujua.

Mmiliki halali wa asili karudi kaanza kudai eneo. Kilichotakiwa hapa ni wavamizi kukubali matokeo wamlipe huyo jamaa kama kweli eneo ni la asili la huyo jamaa.

Kama eneo ni la asili la huyo bwana, atashinda tu mahakamani! Mana anaweza kuleta mashahidi wazee wa miaka hiyo enzi za kijiji ambapo wanamfahamu hadi babu yao. Je, hao wavamizi wakiulizwa hapa alikuwa analima mzee nani watajua?

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
2 Reactions
Reply
Top Bottom