Majaribio ya mbegu

maxmhozya

Member
Dec 26, 2019
20
34
Habari wana JF,

Nimekuwa nikijaribu sana kuweza kuotesha mazao mbalimbali katika bustani yangu Salasala hii yote ni kutaka kujifunza zaidi kwasababu ni kazi nayoipenda sana.

Zoezi 1
Nilijaribu kuotesha mbegu mbalimbali za machungwa, chenza na limao kupitia machungwa tunayokula na pia nikafanikisha miche ikakua sana mingine nikauza mpaka sasa nyumbani kwenye bustani yangu na miche mingi sana karibuni.

Zoezi 2
Nilichukua viazi mviringo ambayo tayari niliviandaa nikavipanda nikafaulu vimeota sana na sasahivi nakaribia kula viazi.

Zoezi 3
Nilichukua tangawizi nikapanda sasa hivi zimekuwa sana nakaribia kuvuna tangawizi hizo kwa ardhi yetu hii hii.

Zoezi 4
Nilichukua mbegu za tende nilizipata kutoka Zanzibar nikazipanda katika bustani yangu pia zoezi hili nimefaulu zimekuwa sana kama unahitaji miche ya tende karibu takuelimisha jinsi ya kutunza mpaka utavuna.

Kwa mawasiliano 0657709912
 
Back
Top Bottom