Hii ni stori ya maisha yangu. Nini ushauri wako kwangu?

mbuyake

Senior Member
Feb 20, 2013
190
235
Wanajamvi naomba nipate ushauri wenu kwa hili.

Kwa sasa nipo kweye 35 kasoro sikni nimepata ujuzi katika fani kama tatu hivi hapa namanisha elimu ya diploma ya utawala biashara lengo kuu tangu awali niwe mjasiriamali lakini baada ya masomo nikajiegesha kwenye kampuni fulani ya ulinzi ili nipate mtaji karibia miaka mitatu nikaona mwishowe nitalowea humo nikajichomoa kajisenti nilikokapata nikavutiwa na kilimo cha kitunguuumuma, Kilosa, Morogoro.

Nikaenda ili nikalime lakini nilichelewa eneo la kulima maana wanakodi kabla ya msimu wa kulima hivyo nikabakia pale kama miezi miwili kama kibarua lengo nipate elimu na ujuzi jinsi ya kusia mbegu kupanda pia uzalishaji wa mbegu hilo nikalifanikisha.

Baada ya hapo nikachukua jukumu la kusafiri hadi mikoa ya magharib kulima hicho kilimo, nilikodi heka mbili na kununua mashine aina ya jd ya kumwagilia maji,nikatafuta vijana watatu tukaanza kazi hatukupata changamoto nyingi wakati wa uendeshaji basi baada ya msimu da!! tulikuja kuambulia debe tatu tu za vitunguu.

Basi sikukata tamaa niliuza mashine yangu nikawalipa vijana nusu ya makubaliano yetu kilichobaki nikaanza kilimo cha nyanya miche elf 5 nikakomaa mwenyewe baada ya msimu pamoja na changamoto lukuki nikaambulia tenga saba tu.

Nilipoziuza nikapata 100k nikaingia kwenye kilimo cha mahindi ya kiangazi nusu heka nikakomaa nayo hadi nakaribia kuivisha mvua za maska zikaanza eneo lilikuwa bondeni, maji yakaingia mashina yakaanza kuoza hatimae nikakosa kabisa, mpaka kufikia hapo ikanilazimu niombe nitumiwe nauli nirudi kwetu lakini ndugu waliona si busara nikakae nyumbani hivyo wakanitaka mawazo yangu nikawambia nataka nikasome afya

Basi wakaniambia nitafute chuo nikafanya hivyo baada ya wiki nikatumiwa nauli ada wakasema naweza nisiende chuo hivyo wakamtumia mpwa wangu ambaye alikuwepo eneo hilo anasoma chuo pia yeye ndo akanilipie kwani mimi siaminik tena, na kwa kuwa hata simu yangu niliyoendanayo huko enzi hizo LG ya kama 400 hivi nilishiwa nikaiuza 56 elfu na laini nikaweka kwa jirani wa kike hivyo waliamini huko nimeoa tayarini

Nilitumiwa 250 ya maandalizi yangu basi nikasema kabla sjaenda ngoja 200 ninunue miwa jaruba moja la miwa niikate kwa pamoja na kukodi trekta nikapeleka munadani kwa mategemeo ya kupata faida mara mbili lakini baada ya siku ya pili kumaliza mauzo nilikata 60 hatimae nikasaliwa 190 nikaona hilo litanighalimu hata nauli nitaishiwa tena basi nikaianza safari na kuanza masomo baada ya muda wangu wa kozi ndo kikafika kipindi cha JPM hakuna ajira,niliamua kujiajiri kwenye field hiyo.

Nilipata kamtaji nikaanza maabara yangu sehemu baada ya muda miaka kama miwili nilianza kupata jina sehemu hiyo nilishangaa kupata ugonjwa wa ajabu kuna kitu kilikalia kwenye koo nilijalibu kutafuta ufumbuzi hospitals nyingi skufanikiwa nilijaribu kuangalia upande wa tiba jadi baasi nikapata ufumbuzi nao walidai ni matatizo ya kutoka upinzani wa kibiashara basi kwa jinsi nilivyotaabika na hilo gonjwa niliacha kutoa huduma za tiba kwa haraka haraka nikafikiria je nitasavive vp kwenye haya mazingira basi likaja wazo kuwa nikiwa dalasa la 3 huko nyuma nilikuwa najifunza ufundi radio hivyo nilipenda sana kujifunza kwa fundi maarufu katika eneo nilipokuwepo mpaka ikatishia kusitisha masomo ili niwe nashinda kujinikaij

Nikaijiwa na wazo kwanini nisijaribu kufanya nikaan, nikaanza ndani ya wiki mbili nikaanza kupata wateja na wengi wakiwa wa simu nikashangaa naimudu kwa haraka zaidi hasa simu nikajikuta nakuwa fundi wa simu na radio, nilianza kupata mafanikio kidogo tofauti na kazi ya awali basi kwa wengi eneo nililokuwepo walipenda kunishauri kwann nisirudi kutibu kuliko kuwa fundi simu radio ila skutaka kabisa kurudi huko.

Nikalazimika kujifunza tiba mbadala ili niweze kutibu kwa kutumia miti shamba ambapo baada ya mafunzo ya waganga zaidi ya tisa wa magonjwa mbali mbali dhumuni ilikuwa baada ya kuzijua dawa za miti shamba niandike vitabu na kusambaza vya tiba mbadala basi nilianza kusaga miti yote niliyoelekezwa kwa kila gonjwa nikapaki katika package zangu, nikafuatilia cheti kutoka baraza la tiba mbadala na kupata, nilianza kuzungusha dawa nyumba kwa nyumba mkoa mzima nilipo na pia mikoa ya jirani hata nilidhubutu kuingia nchi jirani ya drc kwa ajiri ya hayo.

Kwa kila pakage niliweka mawasiliano hivyo wengi walihitaji niwapelekee mwendelezo wa dawa basi baada ya zoezi la kuzunguka,niliugua hata mwili ukashindwa kufanya lolote yaani nikiongea dakika tatu hadi nipumzike kwanza kwa muda kutembea nikawa natingishika hata kusimama hadi supot ya kushika kbas.

Basi baada ya vipimo bugando nikambiwa nimepiga kazi over work,hivyo nikapewa dawa sasa naanza mwaka wa tatu natumia daily mwili upo sawa japo bado kidogo sana ambapo hapaonyeshi inability yoyote hata tatizo limebakia kwenye feeling. kutokana na jinsi nilivyosumbuliwa na hali ya afya nililazimika kurudi kwenye huduma ya kutibu na sasa naendelea kazi yangu ila ni kazi ambayo nafanya lakini nahisi haitanifanya niwe navyotaka japo 20k per day ndo kipato changu,lakini naona hakuna mabadiko kama ambapo niliyoyapata kwenye fundi radio simu kwa kuwa sasa kuna chuo kinatoa ufundi simu nina mpango mwezi ujao nikajiuswa.

Swali langu: je, huo ufundi unaweza kuwa ndo kipaji changu kwa wale wajuvi wa mambo ya vipaji au maana mimi kwa sasa napenda niishi kwa maisha ya kipaji ila sjaujua nini kipaji changu
 
mkuu hivi wewe binafsi unajua unahitaji nini kwenye maisha yako ?

embu check,
kilimo cha kitunguu wewe
kilimo cha nyanya wewe
kilimo cha miwa wewe
maabara wewe
kuuza dawa za hasili (mitishamba) wewe
fundi redio na simu ni wewe mwenyewe

na hapo movie haijaisha ujue! ningependa kujua utafanya vitu gani vingine baada ya miaka kama mitano hivi
 
Ni vizuri kujua vitu vingi lakin ni vizur zaidi kujua vichache kwa undani mkuu.
Hapo ushafanya mambo mengi mno na hayajatiki kama ulivyotarajia.
Na mengi kama sio yote umeafanya kwa muda mchache tu, kila kilimo umetumia msimu mmoja tu.

Nahisi wewe ni moja ya wale watu ambao wakisikia kitu hiki kinalipa basi wanaenda kukifanya bila tafiti za kujiridhisha.

Mi nakushauri ustick hapo kwenye afya au ufundi simu. Hiyo donoa donoa haisaidii
 
Chagua kile kimoja ambacho wewe unakipenda kutoka moyoni na hata unapokuwa unakifanya huwa unapata prestige....komaa nacho hicho..kati ya kilimo,Afya au ufundi simu..
 
Shida moja ya wewe unajikita kutafuta hela na sio kutafuta fani.

Kuna mwenzako mmoja alihitimu chuo kikuu akawa anajichanganya kwenye vibarua vya seremala yumo, Plumbing yumo, umeme yumo , ujenzi yumo , kuweka mageti yumo mwisho kajakujikuta hakuna anachokijua kwasababu alijikita kutafuta hela tu na sio kujua fani.

Kuja kustuka umri umeenda ajira hazitoki.

Tukamshauri ashike fani moja anayoimudu, akachagua kujikita kwenye mabomba, kwasasa ni Fundi mzuri tu.

Na wewe shika moja unaloliweza.
 
Shikilia hapa narudia tena shikilia hapa lasivyo utakuwa na mwisho mbaya sana na uk abv 34 tafadhali chagua kitu kimoja komaa nacho in any means mpaka uone mafanikio aiseee acha kabisa kutangatanga loss mara 1 tu na kuacha.

Anyway afya umesoma coz gani
 
Una familia au una watoto tujue itajitoa VIP kwa icho kipato cha 20k daily
 
Mungu amekuandaa uwe fundi redio na simu! Niamini mimi, ndani ya miaka miwili tu utakuwa umeshanunua kiwanja na kujenga kibanda chako kidogo cha kuishi.

Karibu sana mtaani fundi wetu mahiri. Kuhusu hizo fani nyingine, naona zinakupoteza tu muda wako.
 
wakuu kwa upande wa kilimo nilijiweka pembeni tangu 2014 sjawahi na skutaka tena kuingeji huko niliachana napo kabisa labda huko mbeleni kama itatokea sawa,kwa upande mwingine Elimu ya afya ni taaluma niliyoipata dalasani hivyo natekeleza majukumu yangu ila ufundi nahisi ni kipaji changu maana kwa maelezo ya wengi kuwa kipaji unaweza ukakifanya hata bila elimu husika na ukateleza kwa ufanisi lakini pia unakifanya kwa ubunifu mkubwa hivyo huku sjioni kama moyo unanituma kufanya ubunifu nilionao ndani ya moyo sababu nafanya kwa guidline suala kubwa ambalo ninyi mtanitoa kwenye huu mkwamo ni hapa,ni kweli kuna uwezekano wa kuiacha taaluma na ku deal na upande ambao nahisi ni kipaji changu?,karibuni
 
Shikilia hapa narudia tena shikilia hapa lasivyo utakuwa na mwisho mbaya sana na uk abv 34 tafadhali chagua kitu kimoja komaa nacho in any means mpaka uone mafanikio aiseee acha kabisa kutangatanga loss mara 1 tu na kuacha.

Anyway afya umesoma coz gani
medical lab
 
mkuu hivi wewe binafsi unajua unahitaji nini kwenye maisha yako ?

embu check,
kilimo cha kitunguu wewe
kilimo cha nyanya wewe
kilimo cha miwa wewe
maabara wewe
kuuza dawa za hasili (mitishamba) wewe
fundi redio na simu ni wewe mwenyewe

na hapo movie haijaisha ujue! ningependa kujua utafanya vitu gani vingine baada ya miaka kama mitano hivi
mkuu ni ngumu kujua nitafanya
nini kwa kipindi ulichokitaja japoo target yangu kuu tangu awali naanza maisha ilikuwa ni biashara gani itanipa time freedom then nipate financial freedom kabla ya 40 hilo ndo kusudio langu kuu la uwepo wangu duniani,hvyo kwayote ninayoyafanya si kwa tamaa ya kuwa na mengi bali nifikieje kwenye lengo langu.
 
Chagua kati ya ufundi simu au maabara, stick kwenye hicho kimoja, kuwa karibu na Mungu upate ulinzi wake, piga kazi
 
Wewe ni Jack of all trades, master of none. Unaenda kwa upepo wala sio kipaji kama unavyosema. Hakuna mtu mwenye kipaji cha ufundi kisha akawa na kipaji ya kulima, kisha akawa na uuguzi. Yani ukishakuwa na kipaji kinajitenga chenyewe na viujuzi vingine. Komaa na vitu vichache uvimudu.

Unajifunza kilimo cha vitunguu msimu mzima kisha unalima msimu mmoja? Hauko serious
 
"A rolling stone gathers no moss. Jack of all trades, master of none." Kama suala ni kurogwa hata kwenye ufundi simu utalogwa pia. Endelea ni huduma ya tiba, utazeeka nayo, hiyo mambo ya simu teknolojia itakupindua, haraka ndani ya miaka mitano, ijayo.
 

Similar Discussions

7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom