Dawa ya kuotesha nywele kichwani

Tutor B

JF-Expert Member
Jun 11, 2011
9,025
6,554
DAWA YA KUOTESHA NYWELE KICHWANI

Heroic Shampoo

(Imetengenezwa kwa virutubisho asilia kwa ajili ya ubora wa nywele)
Hakuna kitu kinavutia zaidi kama kuwa na nywele nzuri za kutosha na zenye afya yake ya asili. Hata hivyo tatizo la kupotea kwa nywele au upara ni tatizo kubwa linalowapata watu wengi kila pembe ya dunia.

Kuna sababu nyingi zinazoweza kupelekea kupotea kwa nywele kama vile:

a)Sababu za kimazingira,

b)Kuzeeka,

c)Msongo wa mawazo (stress),

d)Kuvuta sigara kupita kiasi,

e)Lishe duni,

f)Homoni kutokuwa sawa,

g) Kurithi

h) Maambukizi kwenye ngozi ya kichwa

i)Matumizi yasiyo sahihi ya vipodozi vya nywele

j)Baadhi ya dawa za hospitali

k)Matatizo katika kinga ya mwili

l)Upungufu wa madini chuma

m)Na magonjwa mengine sugu

Ni jambo la kawaida kupotea nywele 50 mpaka 100 kwa siku lakini unapoanza kupoteza zaidi ya hapo kwa siku ni muda muafaka kwako kuchukua hatua kurudishia kiasi hicho cha nywele kinachopotea.

Leo nimekuletea hapa orodha ya dawa za asili 6 zinazoweza kuotesha na kuzipa afya upya nywele zako ambazo zimeanza kupotea na hivyo kuondoa huo upara bila gharama sana.

Uvumilivu unahitajika zaidi kwani ni tiba inayochukua muda mrefu kwa kawaida.



Dawa za asili 7 zinazootesha nywele na kuondoa upara



1. Uwatu


Uwatu unajulikana kwa miaka mingi kwa kutibu tatizo la kupotea kwa nywele kichwani. Mbegu za uwatu zina homoni mhimu ijulikanayo kwa kitaalamu kama ‘antecedents’ ambayo huhamasisha kukuwa kwa nywele na kuamsha upya vinyweleo vya nywele.

Mbegu hizi pia zina protini na asidi amino nyingine iitwayo kwa kitaalamu kama ‘nicotinic‘ ambayo huhamsisha kukuwa kwa nywele.

Loweka katika maji kikombe kimoja cha mbegu za uwatu kwa usiku mmoja.

Asubuhi yake zisage upate kama gundi (paste).

Pakaa hiyo gundi kwenye nywele zako na ujifunike na kofia ya kuogea kwa dakika 40.

Fanya zoezi hili kila siku asubuhi kwa mwezi mmoja hivi.

2. Juisi ya kitunguu maji

Juisi ya kitunguu maji husaidia kukuza nywele sababu inayo sulfur nyingi ya kutosha ambayo husaidia kuimarisha mzunguko wa damu kwenda kwenye vinyweleo vya nywele, huvifufua upya vinyweleo vya nywele na kupunguza uvimbe.

Kitunguu maji huua bakteria wabaya kitendo kinachosadia kuua vimelea na wadudu wa magonjwa kwenye ngozi ya kichwa vitu ambavyo huweza kupelekea kupotea kwa nywele (upara).

Utafiti unaonyesha juisi ya kitunguu kuwa na uwezo mkubwa kutibu tatizo la kupotea kwa nywele kwa mjibu wa utafiti uliofanywa na Jarida la Dermatology mwaka 2002 huku wakitoa majibu ya zaidi ya asilimia 74 ya washiriki wa utafiti huo kupata kurejeshewa nywele zao zilizokuwa zimeanza kupotea.

  • Chukua juisi ya kitunguu maji kimoja na uipake moja kwa moja sehemu ambayo nywele zimeanza kupotea na uache kwa dakika 30 kisha jioshe baadaye na shampoo
  • Au changanya pamoja vijiko vikubwa vitatu vya chakula vya juisi ya kitunguu maji na vijiko vikubwa vingine viwili vya jeli ya aloe vera. Unaweza pia kuongeza kijiko kikubwa kimoja cha mafuta ya zeituni na upake mchanganyiko huo kichwani sehemu ambayo nywele zimeanza kupotea. Acha kwa dakika 30 ujisafishe na shampoo baadaye.
Rudia zoezi hili mara 2 mpaka 3 kwa wiki kwa wiki kadhaa.

3. Aloe Vera (mshubiri)

Mmea wa Aloe vera una vimeng’enya ambavyo huhamasisha ukuwaji wa nywele. Ina sifa pia ya kuweka sawa usawa wa asidi na alkalini (pH) ya nywele jambo linaloweza kupelekea kuhamasisha kuota kwa nywele.

Ukiacha hilo la kuotesha nywele aloe vera pia hutibu mba kichwani.

Chukua majimaji ya mshubiri fresh (jeli) na upakae kichwani sehemu ambayo nywele zinanyonyoka na uache kwa masaa kadhaa na ujisafishe na maji ya uvuguvugu.

Fanya zoezi hili mara 3 mpaka 4 kwa wiki.

Unaweza pia kunywa juisi fresh ya mshubiri kikombe kimoja kila siku asubuhi tumbo likiwa tupu kuongeza ufanisi wa ukuwaji wa nywele zako na afya yako kwa ujumla.

4. Juisi ya Kiazisukari. (Beetroot)

Juisi ya kiazisukari ina wanga, protini, potasiamu, , phosphorus, calcium na vitamini B na C. Viinilishe hivi vyote ni mhimu sana kwa ajili ya kukua na kuota kwa nywele na afya ya nywele kwa ujumla.

  • Mara kwa mara kunywa juisi fresh ya kiazisukari pia juisi ya karoti fresh ili kuongeza afya ya nywele zako.
  • Au twanga majani kadhaa ya kiazisukari na uyachemshe kwenye moto kidogo ukichanganya na hina na upake mchanganyiko huo kichwani sehemu ambayo nywele hazioti. Acha kwa dakika 15 na ujisafishe na maji safi. Rudia tendo hili mara kadhaa katika wiki.
5. Tui la Nazi

Tui la nazi lina kiasi kingi cha protini na mafuta mengine mhimu ambavyo huhamasisha kukuwa na kuota kwa nywele na hivyo kuzuia upara. Likitumiwa kwa ajili ya kazi hii tui la nazi halikawii kuleta matokeo mazuri.

  • Tengeneza tui lako zito kidogo ukitumia nazi, ili kupata tui zito na jingi nakushauri kisha kukuna nazi yako iweke kwenye blenda na maji kidogo kwa mbali kisha iblendi kwa dakika kadhaa ndipo ukamuwe upate tui zito kabisa na jingi.
  • Mimina tui hilo kwenye sufuria na uweke kwenye moto kama dakika 3 au 4 hivi kisha ipua
  • Subiri tui hilo lipowe na mwisho pakaa kichwani kichwa chote au sehemu ambayo nywele zimepotea na uache hivyo kama dakika 20 kisha safisha kichwa na shampoo ya aloe vera (mshubiri).
  • Kufanya dawa iwe na nguvu zaidi unaweza kuongeza ndani ya tui la nazi nusu kijiko cha achai cha unga wa pilipili manga nyeusi na kiasi hicho hicho cha unga wa mbegu za uwatu.
6. Mafuta ya habbat soda

Moja ya matumizi makubwa ya mafuta haya ni kuotesha nywele. Bidhaa nyingi sokoni zinazotumika kwa ajili ya kuotesha nywele zinaacha madhara makubwa zaidi kwa mtumiaji kuliko faida zake. Kwahiyo kwa wale wenye tatizo la upala, nywele zisizokuwa na kwa wale ambao nywele zao hazina afya mnashauriwa kuchagua mafuta haya kwa matatizo haya yote.

Ingawa haieleweki ni kwa namna gani mafuta haya yanakuza nywele lakini wanasayansi wanaamini haya yanaweza kuwa ni matokeo ya uwezo wake mkubwa wa kuondoa sumu na protini nyingi ndani yake.

Mafuta ya habbat soda kwa ajili ya nywele yenyewe ni meusi kabisa na huwa mazito kidogo.

Matumizi: Sugulia kipande cha limao fresh eneo ambalo nywele zimenyonyoka na kisha pakaa kijiko kikubwa kimoja cha mafuta ya habbat soda ya nywele na uache kama dakika 15 hadi 20, unaweza kuacha hivyo hivyo au ujisafishe na maji safi, unaweza kufanya kutwa mara 1 au 2 kwa muda wa mwezi mmoja hadi miwili.



7. Tumia mlonge kukuza na kuotesha nywele


Nywele inawezekana ndiyo kitu cha kwanza hasa linapokuja suala la urembo hasa kwa wasichana, wadada na wamama kwa ujumla. Hii inamaanisha nywele zinaangaliwa zaidi na watu kuliko hata nguo, dhahabu au hata viatu.

Nywele ndiyo taji, fahari na kung’aa kwa utukufu wa mwanadamu katika ulinzi na kujiamini.

Ingawa katika zama hizi za vyombo vingi vya habari, wanawake wamekuwa wakishinikizwa na kupewa presha juu ya kuwa aina fulani ya muonekano wa nywele kwa maana ya urefu, rangi, ulaini wake au staili yake.

Namna nywele zako zinavyoonekana isitokee kuwa ni kizuizi cha wewe kutokujisikia vizuri bali unahitaji zaidi kujipenda, kujiamini na kujikubali hivyo ulivyo.

Nywele zako ni kitu pekee na cha thamani

Haijalishi ikiwa wewe ni mwafrika, ni mzungu, ni mchina au mhindi, vile Mungu amekuumba na kukupa hizo nywele wewe ni mrembo na ni wa pekee hivyo ulivyo.

Tofauti ya nywele mara nyingi ni matokeo ya asili ya ki-DNA. Nywele zinaweza kuwa ni kiwakilishi cha utamaduni, sanaa, siasa au namna ya kuwasilisha hisia.

Hakuna kiwango maalumu cha urembo au uzuri wa nywele kwa watu wa utamaduni wowote! Vyombo vya sasa vya habari vinatuchanganya tuwe bize na urembo wa nje ya mwili huku tukijisahau kushughurika na urembo wa ndani ya mwili.

1 Petro 3 : 3 – 4

3. Kujipamba kwenu, kusiwe kujipamba kwa nje, yaani, kusuka nywele; na kujitia dhahabu, na kuvalia mavazi;
4. bali kuwe utu wa moyoni usioonekana, katika mapambo yasiyoharibika; yaani, roho ya upole na utulivu, iliyo ya thamani kuu mbele za Mungu.

Ingawa katika mbio hizi za urembo wa nywele (na hakuna ubaya wowote katika hili) mti wa ajabu wa mlonge una umhimu mkubwa ambao hujawahi kuambiwa na mtu katika kutunza, kukuza na kuweka vema afya ya nywele kwa ujumla.

Unaweza kuniuliza KIVIPI?

Kabla ya yote ngoja tujifunze ni viinilishe vipi, vitamini zipi na madini yapi ambayo ni MHIMU kwa kuotesha, kukuza na kuboresha afya ya nywele kwa ujumla.

Vile vile yakupasa utambuwe kuwa ubora wa afya yako kwa ujumla unaweza kutambulika kwa kuangalia muonekano wa nywele zako tu! Nywele zako zinaonyesha afya yako ilivyo.

Kama mwili wako ni mzima, una viinilishe vyote mhimu na nywele zako zitaonekana kuwa zina furaha pia. Ikiwa kuna shida mahali popote kwenye mwili wako nywele zako zitatuonyesha hilo.

Utumiaji wa kila siku wa vitamini na madini mhimu na asidi amino ni mhimu katika kutunza nywele zetu zibaki na afya na zenye furaha. Baadhi ya vitamini, madini na asidi amino ni mhimu kwa ajili ya uundwaji wa ‘keratin’ ambayo hufahamika kama umeng’enywaji wa nywele ( hair metabolism).

Siri kubwa nyuma ya pazia la ukuwaji wa nywele …

Kwahiyo, kwa ubora kabisa wa kukua kwa nywele, vinyweleo vya nywele lazima viwe na kiasi cha kutosha cha viinilishe na oksijeni katika mfumo wa mwili ili kuotesha na kukuza nywele.

Kumbuka mti huu wa ajabu wa mlonge umebarikiwa kuwa na vitamini na madini kwa wingi kuliko mti au mmea wowote chini ya jua. Mlonge una viinilishe 92 vya madini na vitamini mbalimbali huku ukiwa na viondoa sumu mwilini 46!

Kama tunavyoweza kuona mlonge ni kitu maalumu mno na cha ajabu, una viinilishe vingi mno kwa ajili ya afya ambavyo siyo rahisi kuvieleza vyote katika makala hii lakini nitajaribu kuvigusia baadhi kati ya hivyo mhimu kwa ajili ya nywele.

Mlonge una vitamini C mara 7 zaidi ya ile ya kwenye machungwa, una madini ya chuma mara 25 zaidi ya yale yaliyomo kwenye spinachi na mara 17 zaidi ya kalsiamu zaidi ya ile iliyomo kwenye maziwa na mara 4 zaidi ya vitamini A iliyomo kwenye karoti na vitu vingine vingi.

Vitamini A ndiyo vitamini mhimu zaidi katika kutengeneza afya bora ya tishu na seli mabalimbali katika mwili jambo linalopunguza kupotea au kunyonyoka kwa nywele. Mlonge ni mti tajiri wa vitamini A na utachangia kwa sehemu kubwa katika ukuwaji wa nywele zako.

Madini ya Zinki ambayo yanapatikana kwa wingi katika mlonge yanahamasisha ukuwaji wa nywele na kuimarisha kinga yako ya mwili.

Kiasi cha kutosha cha madini ya zinki na vitamini A pia kunazuia kuzibika kwa tezi mafuta ya nywele katika ngozi ya kichwa. Sababu namba 1 ya watu wengi kusumbuliwa na tatizo la kunyonyoka kwa nywele au upara ni matokeo ya kushuka kwa madini ya zinki mwilini.

Ikiwa una upungufu wa madini ya zinki mwilini kutatokea kupungua au udhaifu katika vinyweleo vya nywele ambavyo vina uhusiano wa moja kwa moja na usanisi na DNA ya nywele, wakati zinki ina ushawishi mkubwa katika uundwaji wa asidi nyukilia.

Kingine mhimu kilichomo kwenye mlonge kinachohusika na afya ya nywele ni uwepo wa viatmini nyingi za kundi B kama B1, B2, B3, B4, B6, B7, B12 ,B14, na B17. Hivyo afya mbovu ya nywele inaweza kutokea ikiwa lishe yako ina upungufu wa kiasi cha kutosha cha vitamini za kundi B hasa hasa vitamini B6 na folic asidi.

Vitamini E ambayo huondoa sumu mwilini ni mojawapo ya kiinilishe mhimu katika mlonge ambacho ni cha lazima katika ukuwaji wa nywele sababu huongeza msukumo wa damu kwenye ngozi ya kichwa.

Kuongezeka kwa msukumo wa damu kwenye ngozi ya kichwa (scalp) kunatengeneza upatikanajai wa viinilishe mhimu kwa ajili ya vinyweleo vya nywele jambo linaloleta afya bora ya nywele na nywele kuwa ndefu.

Kwa kuongezea vitamini C kwenye mlonge inaunda msukumo wa damu katika ngozi ya kichwa na vinyweleo vya nywele.

Madini ya Potasiamu madini mengine mhimu katika mlonge yanazipa nywele zako uwezo wa kuchukua viinilishe katika chakula vinavyohitajika ili kuwa na nywele nzito, nyingi na za kuvutia.

Kwenye mlonge pia kuna kiondoa sumu chenye nguvu sana kijulikanacho kitaalamu kama ‘Zeatin’. Tafiti za wazi zimethibitisha kwamba mlonge una kiasi kingi kisicho cha kawaida cha homoni za mimea zijulikanazo ‘cytokinins’ kama vile zeatin.

Katika kuangalia zaidi katika kemikali hii majaribio mbalimbali yamehitimisha kuwa cytokinins kama zeatin zina kazi kubwa katika kukuzuia usizeeke. Namna hili linatokea ni kuwa Zeatin inachelewesha mgawanyiko wa seli (cell division) na kuondoa sumu mwilini.

Madini, Mlonge na Ukuwaji wa nywele …

Salfa ya asili iliyomo kwenye mlonge ni madini mengine mhimu kwa ukuwaji wa nywele.

Sulfur ya asili ambayo ni tofauti na ile ya kutengenezwa ni kitu kilichopo karibu katika kila vyakula tunavyokula hasa matunda na mboga za majani.

Sulfur inashikilia jina la utani (a.k.a) la ‘madini urembo’ kwa sababu hii. Ndiyo madini yanayokuza nywele, kucha, kung’arisha ngozi na hivyo kukufanya uonekane kijana.

Madini mengine yaliyomo kwenye mlonge kama vile manganizi, kalsiamu na shaba yanaweza kuhamasisha kukua na kuripea nywele.

Usisahau pia kupendelea kula vyakula vingi ambavyo havijapikwa (staili ya kachumbali nk). Vyakula vingi vya kwenye migahawa si salama kwa ukuwaji wa nywele zako.

Vyakula feki kama vile vyenye sukari nyingi kupitiliza, vinywaji baridi, keki, utumiaji uliozidi wa nyama nyekundu, nyama ya nguruwe (kitimoto) vinachangia kupotea kwa nywele.

Ili kuotesha au kukuza nywele zako ukitumia unga wa majani ya mlonge anza na kutumia kijiko kidogo kimoja cha chai cha unga wa majani ya mlonge kutwa mara 1 ukitumia kwenye juisi ya matunda uliyotengeneza mwenyewe nyumbani au katika uji au kwenye mtindi au kwenye asali.

Pole pole unaweza kuongeza kiasi mpaka kijiko kikubwa cha chakula kimoja kwa siku kutegemea na afya yako inavyoitika. Wasiliana pia na daktari wako wa karibu kabla ya kuanza kutumia mlonge ikiwa wewe ni mjamzito au una shinikizo la chini la damu.

Mpendwa msomaji, wakati ukiwa bize ukitumia mlonge kukuza nywele zako usisahau pia kutumia mlonge siyo tu kutakusaidia kuwa na nywele nzuri bali pia utakuwa ukiusaidia mwili wako katika kuongeza kinga ya mwili, kusafisha damu yako, kudhibiti uzito wako, kuweka sawa sukari katika mwili wako, kuongeza nguvu za mwili na faida nyingine nyingi za kiafya bila idadi.

Kwa mahitaji ya unga wa mlonge, shampoo kwa ajili ya kuboresha nywele zako wasiliana nasi kwa simu nambari 0655 533 543; E-mail: jnb14enterprises@gmail.com.

MZIGO TUNAKUTUMIA POPOTE ULIPO.
 
Back
Top Bottom