Majambazi zaidi ya 20 yafanya kweli Masaki | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Majambazi zaidi ya 20 yafanya kweli Masaki

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kanyagio, Feb 26, 2010.

 1. kanyagio

  kanyagio JF-Expert Member

  #1
  Feb 26, 2010
  Joined: Dec 10, 2009
  Messages: 985
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 45
  habari ifuatayo ni tetezi, bado nafuatilia kujua kama ni ya kweli. hasa kufahamu ni kampuni gani imekumbwa na maswahiba haya.

  "majambazi yamevamia ofisi za kampuni mpya ya simu jana mahira ya saa 3.30 usiku huko maeneo ya masaki karibu na coco beach . kwa habaaari zenye uhakika ni kwamba majambaz hayo yalikuja na gari ya security comapn na kujifanya yamekuja kupakua mzigo ndipo yalipofunguliwa mlango yaliingia ndan na kuwatyt walinzi na kuingia panapo ofisi kuu. waliingia watu kama ishirin wakiwa na uniform za ultimate security na walipoingia ofisi za juu waliwafunga kamba waliokuwa shift ivo walifanikiwa kupora simu za watu hao na fedha pia na kama tulivyozoea wafanyakaz wengi wa maofisin wanaachaga lap top zao oficn walizichukua takriban laptop 56 na shelf la pesa na vitu vingine visivyo na idadi"
   
 2. kanyagio

  kanyagio JF-Expert Member

  #2
  Feb 26, 2010
  Joined: Dec 10, 2009
  Messages: 985
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 45
  hiyo habari ilitumwa na mdau mmoja, naendelea kufuatilia habari zaidi
   
 3. Masaki

  Masaki JF-Expert Member

  #3
  Feb 26, 2010
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,468
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 160
  Kampuni iliyopo Masaki karibu na Coco Beach ni sasatel.
   
 4. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #4
  Feb 26, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,834
  Likes Received: 249
  Trophy Points: 180

  Wakuu wa Polisi wapo kwenye SEMINA (elekezi!)
   
 5. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #5
  Feb 26, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 368
  Trophy Points: 180
  leteni uthibitisho
   
 6. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #6
  Feb 26, 2010
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 99
  Trophy Points: 145


  Hao ni majambazi au kundi la vibaka au ni kundi la waasi wezinduka na kufanya huo uhalifu ???? watu 20 jamani??

  Hii nchi sasa inahitaji viongozi ambano ni ma dictator period ndio tutasonga mbele nao sasa huu uhuru si uhuru tena ni kunyanyasana ndani ya uhuru na kuutumia vibaya

   
 7. M

  Mwanazuoni Member

  #7
  Feb 26, 2010
  Joined: Nov 12, 2008
  Messages: 69
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kinachosigitisha zaidi kuhusu ulinzi ni kuwa polisi wetu msaada wao ni mdogo sana. Tuliopata taarifa mapema baada ya kupigiwa na waliokua zamu wezi walipoondoka, tulijaribu kupiga emmergency number za polisi na za makamanda ikiwemo number ya saidi mwema lakini cha kusigitisha ni kuwa hakuna mtu aliyekua anapokeo hizo simu. Hivyo wezi walichukua walivyotaka kwa raha zao na kuondoka bila preasure yeyote ile. Sijui watanzani wategemee ulininzi toka wapi. Polisi wamefika pale zaidi ya nusu saa tangu uhalifu ulipotokea. Mmoja wetu aliyepigiwa simu akiwa tabata ndiye aliyekimbia hadi osterbay kutoa taarifa...sasa waweza kuelewa mtu atoke tabata na hii foleni ya dar eti ndio akawahi wezi waliokwisha kuiba na kutoka.

  Hiini setback kubwa sana kwa kampuni hii ambayo ndio kwanza haijafikisha hata mwaka tangu ianze operation mwaka jana. Polisi walipofika pale hakuna hata la maana walilokua nalo zaidi ya kuwatukana nakuwagombeza wale walinzi waliopigwa na kuumizwa kisha kufungwa na kamba. Wezi walituibia hadi pete za ndoa mikono ikiwa pamoja na simu na pesa tulizokua nazo mikononi.

  Ashukuruwe Mungu kuwa wafanyakazi hawakuumizwa
   
 8. M

  Mwanazuoni Member

  #8
  Feb 26, 2010
  Joined: Nov 12, 2008
  Messages: 69
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Unataka uthibitisho gani? huelewi nini...Sasatel imevamiwa jana na majambazi waliongia na Hiace...waliwahadaa walinzi kuwa wanaingiza mali za kampuni toka bandarini zilikochelewa. Walinzi kwa uzembe nao wakawafungulia geti bila kuthibitisha ukweli. Kibaya zaidi wale walinzi ndio ilikua mara yao ya kwanza kupangiwa ulinzi sasatel.

  Pia nimhahihishe mmoja laiyesema walikuwa wamevaa uniform za altimate security...baadhi yao kama watano walikua wamevaa uniform za Knight Support ambao ndio wanalinda pale. Tulikuta wameacha shati moja na kofia za kampuni hiyo nje ya jengo.
   
 9. M

  Mwanazuoni Member

  #9
  Feb 26, 2010
  Joined: Nov 12, 2008
  Messages: 69
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sio tetesi ndugu yangu...wezi wamevamia sasatel majira ya saa tatu na nusu...wengi kama 20 hivi...hawakuua zaidi ya kuumiza walinzi...wakaingia ndani na kuwafunga staff waliokua zamu na kuwapora kila walichokua nacho...waliiba kila kilichowafaa ikiwa ni pamoja na kuvunja store na kuiba safe ya kampuni kama ilivyo pamoja na uzito wake wote.
   
 10. W

  Watanzania JF-Expert Member

  #10
  Feb 26, 2010
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 727
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Habari ilivyo inatoa picha kuwa wakusika wa wizi huo ni wafanyakazi wa Sasatel
   
 11. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #11
  Feb 26, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 80,463
  Likes Received: 117,261
  Trophy Points: 280
  Mkuu Jethro, Kiongozi wa nchi juzi tu alitangaza Tanzania iko shwari. Polisi wako busy na kesi ya Jerry Muro.
   
 12. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #12
  Feb 26, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Kama ulikuwepo,kila siku ni semina elekezi,sijui wataelekezwa mpaka lini.
   
 13. M

  Msharika JF-Expert Member

  #13
  Feb 26, 2010
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 937
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Kweli polisi wetu vilaza jamani. Tusiwalaumu polisi ila tuangalie na wanaofanya selection ya watu wanaoomba kusomea upolisi. Hakuna mtu wa Division I, II au hat III anaye apply upolisi. Sasa inteligency system utaitrain vipi? walishakuwa wagumu wa kuelewa tangu wakiwa wadogo, hawafundishiki.
   
 14. k

  kanda2 JF-Expert Member

  #14
  Feb 26, 2010
  Joined: Apr 22, 2007
  Messages: 1,318
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  poleni sana ndugu zanguni.
   
 15. Hebrew

  Hebrew JF-Expert Member

  #15
  Feb 26, 2010
  Joined: Jul 3, 2008
  Messages: 520
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 45
  mkuu, una uthibitisho kuhusu hii? Kama unao basi karipoti polisi
   
 16. J

  JokaKuu Platinum Member

  #16
  Feb 26, 2010
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 13,572
  Likes Received: 6,705
  Trophy Points: 280
  ..poleni!! hii nchi sijuwi inakwenda wapi. ujambazi unaotokea ni dalili za matatizo makubwa zaidi ktk jamii yetu.
   
 17. Hassani

  Hassani JF-Expert Member

  #17
  Feb 26, 2010
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 276
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  Si kweli kuwa Police hawaajiri watu wenye hizo division,wanaajiri sana tu,tena hata bachelors holders wengi tu.Tatizo la police ni bad manpower utilization,viongozi wa police wameshindwa kabisa kuwamotivate hao watu,kuna jamaa yangu Aliajiriwa na Bachelor ya Public Administration and French Language,Kazi alizokuwa anapewa ni kukaa counter(CRO) na malindo ya usiku,tena kwa kumkomoa kisa anajifanya msomi.Mara nyingi utakuta tangu wakiwa CCP wanatukanwa na matusi kama,"ungekuwa msomi usingeingia polisi".Vitengo muhimu kama Intelligencia na CID wanapewa watoto wa wakubwa ambao wengi ni vilaza.Tangu alipoingi Mwema angalau kabadlisha system mtu mwenye degree anaanza na mshahara wa 250,000/=,sasa hapo kutakuwa na utendaji wa kazi kwa dhamira.JESHI LA POLISI KWA TZ NI BADO SANA.
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...