Majambazi Arusha: Mabomu, Bunduki, Risasi, Bastola - Hii ni Kashfa JWTZ

Nd. Mwanakijiji,
Umejuaje kama matundu ya risasi kwenye miili ya hawa jamaa yanaashiria CLOSE RANGE? Unless kama umeona forensic report!
hata hivyo kama polisi walitumia SMG ( bila shaka walitumia), unategemea kweli matundu yake yatakuwa sawa na yale ya pistol??(ambayo unaweza ku-judge kirahisi kama ni close range kind of shooting au la)

Brutus, mbona taarifa hiyo imetoka tangu juzi na Polisi wetu hawajakanusha. Jamani, mauaji ya bunduki yanachunguzika kiurahisi sana na ni rahisi kujua hata umbali wa mtu alikokuwa na hata angle ya risasi iliingiaje. Brutus, kwa vile naona umepitwa kidogo mambo yanayojulikana hadi hivi sasa publicly:

a. Walipigwa risasi kifuani
b. Walipigwa risasi kichwani
c. Walipigwa risasi wengine wakiwa wamegeuka nyuma (from behind)
d. Walipigwa risasi kwa ukaribu

Hayo yote manne yanajulikana na Polisi wetu na wa Kenya. Hayajakanushwa, kwani wakikanusha tu, miili bado haijazikwa mtaalamu yeyote yule anaweza kwenda kuiangalia na kuamua!
 
Wizi ulikuwa utokee lini? Jinsi nilivyosoma ulikuwa ufanyike siku ya pili, huenda una more information za ndani lakini haya ndio maswali ambayo kamanda wa polisi alitakiwa kujibu ulipohojiana naye - Kwa nini hukumuuliza maswali magumu?

Kweli huenda makosa yametendeka lakini wewe na mimi tupo kambi ya Tanzania hatuwezi kuwasupport The EA Standard na baadhi ya Kenyans hivi sasa wakati tupo kwenye hili ambalo kwanza lina divert our attention kwenye maswala yetu ya ndani. Vile vile lazima ukumbuke kwamba yalipotokea mauaji Dar kuliundwa tume, tume ni pesa na ushahidi mwingi hapa hawa walikuwa ni wezi yule aliye na beef aende kufungua kesi lakini sidhani kama sisi Tanzania tuna pesa za kuchezea kwa wezi wanaotembea na silaha za kivita. Hapa naona serikali imelala usingizi wa pono hadi mambo kama haya yanatokea kwenye barabara zetu. Hebu fikiria wangelipua mabomu waliyokuwa nayo kwenye umati wa watu ingekuwaje?
 
Hizi ulipoziangalia zile silaha ulijua kama zilitumika? HIvi unajua magazine moja inachukua kama risasi 30 hivi na hizo AK 47 tatu tukiassume zote zilikuwa loaded ina maana zilikuwa na risasi 90 ukiongeza na hizo ambazo hazikutumika kulikuwa na magazine nyingine mbili. (assuming kuwa haikupigwa hata moja).

Kama ilipigwa hata risasi moja ina maana polisi wanaushahidi wa maganda wa kuonesha ni risasi ngapi zilipigwa na majambazi hao. Naweza kufundisha mambo ya POlisi kidogo lakini elewa ndugu yangu mambo sivyo kama mnavyosoma kwenye picha, ndio maana kunakitu kinaitwa forensic science.
 
Brutus, mbona taarifa hiyo imetoka tangu juzi na Polisi wetu hawajakanusha. Jamani, mauaji ya bunduki yanachunguzika kiurahisi sana na ni rahisi kujua hata umbali wa mtu alikokuwa na hata angle ya risasi iliingiaje. Brutus, kwa vile naona umepitwa kidogo mambo yanayojulikana hadi hivi sasa publicly:

a. Walipigwa risasi kifuani
b. Walipigwa risasi kichwani
c. Walipigwa risasi wengine wakiwa wamegeuka nyuma (from behind)
d. Walipigwa risasi kwa ukaribu

Hayo yote manne yanajulikana na Polisi wetu na wa Kenya. Hayajakanushwa, kwani wakikanusha tu, miili bado haijazikwa mtaalamu yeyote yule anaweza kwenda kuiangalia na kuamua!

Vyote ulivyoorodhesha vinaweza kutokea katika mapambano ya silaha... hasa yanayohusisha silaha nzito.. unless ungependelea wapigwe risasi za miguuni!
Labda nikuulize hili swali...
Unafikiri polisi waliwanyemelea wakawa-execute kimya kimya..na hizi ripoti ni kiini macho?
 
keep thinking my dear Brutus...sikiliza mahojiano yangu na Kamanda Lukas, read all the initial report up to know.. pole pole utaanza kupata picha ya kwanini nauliza maswali..
 
....hapo hakuna jambazi wala silaha ni scam tuu ya hao majangili polisi yaliyonyimwa rushwa
 
W
izi ulikuwa utokee lini? Jinsi nilivyosoma ulikuwa ufanyike siku ya pili, huenda una more information za ndani lakini haya ndio maswali ambayo kamanda wa polisi alitakiwa kujibu ulipohojiana naye - Kwa nini hukumuuliza maswali magumu?

Ulikuwa ufanyike siku ya pili... halafu wakauawa wakiwa wanaenda kuiba benki?

halafu naelewa wewe unaangalia suala hili kiuzalendo na kitaifa kuwa waliouawa ni Wakenya so, no need to even look at the numerous possibilities.... that might lie behind the curtain..
 
Hizi ulipoziangalia zile silaha ulijua kama zilitumika? HIvi unajua magazine moja inachukua kama risasi 30 hivi na hizo AK 47 tatu tukiassume zote zilikuwa loaded ina maana zilikuwa na risasi 90 ukiongeza na hizo ambazo hazikutumika kulikuwa na magazine nyingine mbili. (assuming kuwa haikupigwa hata moja).

Kama ilipigwa hata risasi moja ina maana polisi wanaushahidi wa maganda wa kuonesha ni risasi ngapi zilipigwa na majambazi hao. Naweza kufundisha mambo ya POlisi kidogo lakini elewa ndugu yangu mambo sivyo kama mnavyosoma kwenye picha, ndio maana kunakitu kinaitwa forensic science.

Kwa nini hukumuuliza kamanda wa polisi maswali haya? Unafahamu unatoa tuhuma nzito sana, unaweza kutupa ushahidi wa hizi tuhuma.

Hebu tupe ukweli vile vile wa ule wizi wa ubungo ambako askari polisi alipambana nao saa nee asubuhi?
 
na angalia maneno yangu nayachagua vizuri sana.... Ukiacha kuliangalia hili macho ya "mtanzania" na kuliangalia kwa macho ya "utawala wa sheria na haki"... you'll get closer to where I am. And I know, nikianza kuangalia kwa macho ya "nchi yangu, Tanzania, majambazi wa Kenya".. I'll get closer to where you are..
 
Hivi unapomuhoji kwa mfano kamanda wa polisi huwa unachaguliwa maswali? Kama huchaguliwi kwa nini hukutoa dukuduku zako - ulikuwa unamuonea soni? Mimi siafiki utumbo huu unaouleta hawa ni majangiri - PERIOD WANISHI KWA BUNDUKI WATAKUFA KWA RISASI.
 
Kwa nini hukumuuliza kamanda wa polisi maswali haya? Unafahamu unatoa tuhuma nzito sana, unaweza kutupa ushahidi wa hizi tuhuma

Dua... sasa hivi natamani ningemuuliza maswali hayo yote, lakini maswali hayo yote hayakuwa formed kwenye akili zangu kwani sikuwa na habari zote zinazokingana, na nimechukua muda kupiece up information. tatizo ni kuwa nikimuuliza hata hivi sasa tutapata majibu tofauti. KUmbuka habari hii iliporipotiwa hapa mara ya kwanza ilikuwa ni kuhusu jaribio la kwenda kuwaokoa wenzao toka gerezani. NIlipomuuliza juu ya hilo alikana.. lakini sasa hivi wameliongezea... (sidhani wakati anazungumza na mimi alikuwa amesikia tetesi hizo)...!

Anyway, nimejenga maswali makubwa manne ambayo sikupata kumuuliza Kamanda, na nitayauliza kwenye makala yangu kesho na ni matumaini yangu itasababisha majibu ya uhakika siyo ya kupuuzia. Wakitoa majibu ya kuridhisha na yasiyokingana watawanyamazisha WAkenye, na watawanyamazisha watanzania ambao nao wanahoji juu ya mauaji hayo. In that case watakaokuwa wameshinda na kujijengea credibility zaidi ni wao. Kinyume cha hayo... you can just imagine...
 
Mwanakijiji,
Mimi nakuamini sana katika mambo mengi unayoyawekea mashaka, AC ilikuwa mojawapo na pili lile swala la wanafunzi wetu huko Urusi. Inaonyesha unazo data lakini kutokana na mazingira yenyewe umetumia akili ya kuzaliwa... una deal na isuue kulingana na mazingira! hiyo akili mjomba wala sintakupinga hata kidogo. Lakini pamoja na yote hayo, mbona unazidi kutupa wasiwasi na Polisi wetu.
Nimeuliza kama motive ilikuwa zile billioni zilisemekana kuibiwa ktk benki mojawapo huko huko Moshi siku za nyuma..Umeniacha nje.
Nimeuliza kama zile silaha zilikuwa planted.. umeniacha vilevile bali kunambia nichimbe ndani zaidi... duh nachimba mjomba lakini sioni dhahabu wala shaba!
Sasa ebu nitazame kwa jicho lako. Polisi wetu walipewa hint ya kwamba majambazi fulani wanaotakiwa Kenya wapo sehemu fulani (kama alivyosema mkuu wa kituo).. Kwa kuelewa hivyo walijipanga na ku wafuata pale walipo (i.e Hotelini) wakachukuliwa hadi sehemu njia panda na kuwapa somo (mateso) kisha walipoona hakuna kitu waliamua kuwamaliza. Kuna uwezekano jeshi letu la Taifa TPDF walijumuika ktk kutoa AK47 na hand granade maanake kituop cha Polisi hawana silaha hizi...
Sasa yote haya yalipangwa ktk muda gani?.. questiuon mark. OK hawa Majambazi walikuwa ktk msafara kama madai ya Polisi wetu na walikuwa silaha zile ndani ya gari..Hawakuzitumia hata kidogo kwani waliposimamishwa walijisalimisha.
Polisi wetu kama walivyofanya Polisi wa Kenya waliwalaza chini wengine wakiwa bado wamesimama waliamua kuwawasha. baadhi yao walijaribu kukimbia ndio maana walipigwa risasi za nyuma!..
Kuua watu 14 execution style ina maana kulikuwepo na askari wetu zaidi ya mmoja. Hivi kweli askari wetu wote wanaweza kulala usingizi kwa kufahamu wameua Majambazi wakiwemo na raia ambao hawakuhusika kabisa!.
Je, tuna ushahidi gani zaidi wa kudhihirisha maelezo haya?.. hatuna isipokuwa tunatumia maneno ya Polisi na kuyatoa makosa wakati sisi wenyewe hatuna theory ya kile kilichotokea.
Je, tukifanya uchunguzi kwa theory hii yetu ya kubahatisha ina mantiki?.. sidhani bado fumbo ni kubwa zaidi ktk Polisi kufanya Unyama...Tusubiri ukweli tutakuja jua.
 
Mwanakijiji,
Mimi nakuamini sana katika mambo mengi unayoyawekea mashaka, AC ilikuwa mojawapo na pili lile swala la wanafunzi wetu huko Urusi. Inaonyesha unazo data lakini kutokana na mazingira yenyewe umetumia akili ya kuzaliwa... una deal na isuue kulingana na mazingira! hiyo akili mjomba wala sintakupinga hata kidogo. Lakini pamoja na yote hayo, mbona unazidi kutupa wasiwasi na Polisi wetu.

my dear friend.. siyo kusudio langu kuwatia wasiwasi.. lakini historia iko nyuma yangu zaidi na hii inanifanya niwe skeptic. Sababu serikali huwa hazitoi habari kwa hiari hasa hii ya kwetu.

Nimeuliza kama motive ilikuwa zile billioni zilisemekana kuibiwa ktk benki mojawapo huko huko Moshi siku za nyuma..Umeniacha nje.

Motive ya nani? kwa upande wa hao washukiwa inawezekana kabisa walikuwa wanakuja kujihusisha na vitendo vya ujambazi (hilo siyo ninaloulizia). Kwa upande wa polisi motive ilikuwa ni kuhakikisha kuwa wote washukiwa hawatapa nafasi ya kusimama hadharani kuelezea upande wao, hata Sadam jamani alipewa nafasi ya kusimama kujitetea, ingawa walimnyonga!

Nimeuliza kama zile silaha zilikuwa planted.. umeniacha vilevile bali kunambia nichimbe ndani zaidi... duh nachimba mjomba lakini sioni dhahabu wala shaba!

Mkandara, silaha walizikuta wapi?

a. Kama walizikuta mikononi mwa washukiwa ina maana washukiwa walikuwa tayari wamejiandaa kwa mapambano na hivyo hawakushtukizwa. Kama walikuwa wamejiandaa kwa mapambano na walikuwa njiani bila ya shaka walikuwa wanakwenda kupora benki. Tatizo ni kuwa hiyo ilikuwa saa moja na nusu usiku! Benki zinafunguliwa kesho yake....

b. Polisi waliwafuatilia hawa jamaa tangu mpakani (that is my original theory) which will explain ilikuwaje rahisi sana kuwapata waliko ndani ya siku mbili tangu waingie nchini. Walijua wapi wamefikia na jana yake walimfuatilia mwanamama alipoenda benki. Je, yawezekana silaha zilikutwa kwenye nyumba waliyofikia na siyo eneo la tukio? absolutely, that will explain kwanini hawakuwa wamevaa vests zile na kwanini silaha zilikuwa bado intact (maganda ya risasi maganda ya risasi)

NOw,

Sasa ebu nitazame kwa jicho lako. Polisi wetu walipewa hint ya kwamba majambazi fulani wanaotakiwa Kenya wapo sehemu fulani (kama alivyosema mkuu wa kituo).
.

almost!, lakini fikiria nyuma kidogo.. walipewa hint kuwa kuna majambazi yamevuka mpaka wenu na wako hivi na hivi.. tumewapa pasi za kusafiria hizi na hizi... wanapopita mpakani.. hawachunguzwi sana wanaweza kupitisha silaha zote...! the first set up.

Kwa kuelewa hivyo walijipanga na ku wafuata pale walipo (i.e Hotelini)

very close.. fikiria toka mpakani...
wakachukuliwa hadi sehemu njia panda na kuwapa somo (mateso) kisha walipoona hakuna kitu waliamua kuwamaliza.

very good! hawakuuawa kwenye nyumba waliyofikia bali barabarani.. wakienda wapi? waliweza vipi kuteremka watu wote 14 kwenye vitara au magari mengine.. wale wengine walirushiana risasi kwa muda gani na je magari yale "yaliyokimbia" yalipatwa na risasi?
Kuna uwezekano jeshi letu la Taifa TPDF walijumuika ktk kutoa AK47 na hand granade maanake kituop cha Polisi hawana silaha hizi...

may be not.. kumbuka sihoji kama walikuwa ni majambazi au la... inawezekana kutokana rekodi zao kuwa walikuwa ni majambazi kweli...

Sasa yote haya yalipangwa ktk muda gani?.. questiuon mark. OK

hawa Majambazi walikuwa ktk msafara kama madai ya Polisi wetu na walikuwa silaha zile ndani ya gari..Hawakuzitumia hata kidogo kwani waliposimamishwa walijisalimisha.

hilo swali kwa upande wangu ni rahisi, kwani aliyeongoza mapambano hayo.. ni mtu ambaye nina data zake... na one of the best cops Tanzania ever produced in field operation!

Polisi wetu kama walivyofanya Polisi wa Kenya waliwalaza chini wengine wakiwa bado wamesimama waliamua kuwawasha. baadhi yao walijaribu kukimbia ndio maana walipigwa risasi za nyuma!..
Kuua watu 14 execution style ina maana kulikuwepo na askari wetu zaidi ya mmoja. Hivi kweli askari wetu wote wanaweza kulala usingizi kwa kufahamu wameua Majambazi wakiwemo na raia ambao hawakuhusika kabisa!.
Je, tuna ushahidi gani zaidi wa kudhihirisha maelezo haya?.. hatuna isipokuwa tunatumia maneno ya Polisi na kuyatoa makosa wakati sisi wenyewe hatuna theory ya kile kilichotokea.
Je, tukifanya uchunguzi kwa theory hii yetu ya kubahatisha ina mantiki?.. sidhani bado fumbo ni kubwa zaidi ktk Polisi kufanya Unyama...Tusubiri ukweli tutakuja jua.

now hayo maelezo ya mwisho na mtiririko wa matukio only independent investigation itaonesha. Na kama watu wanawazulia mabaya POlisi will be vindicated na sisi sote tutaona fahari!
 
Hii issue inachanganya, Kwa taarifa tulizosoma ni

1.kuwa hawajamaa walikuwa wanajiandaa kufanya uhalifu kesho yake sasa hapo hamna mantiki ya kuvaa makoti ya kuzuia risasi leo wakati kazi ni kesho.

2. Polisi waliwafuatilia na walifanya ambushi eneo la maili sita daraja mbili na hii ni kupunguza madhara ambayo yangeweza kutokea kama wangesubiri hadi wakati wa kurob bank, Polisi walijifunza kutokana na tukio la Arusa la kupambana na majambazi wawili kwa masaa kadhaa.

3.Taarifa zilizopatikana kutoka polisi wa Kenya ni kuwa baadhi yao walikuwa wahalifu sugu wa kutisha, je hao watu wema walitoka wapi na wahalifu hao?

4. Je taarifa ya polisi ni kuwa polisi walikuwa wamejipanga na hatujui idadi ya polisi na hii inawezekana kustukizia huko ndio kulirahisisha kazi ya kuwauwa hao jamaa.

5. Polisi wanadai walishambuliwa na magari mengine yalifanikiwa kutoroka. Kama ni kweli tunajua magari yaliyotoroka yaliondoka na sila za aina gani na ngapi?

6. Inawezekana kabisa silaha zilizokamatwa na polisi hazikutumika kwani inawezekana washambuliaji walifanikiwa kutoroka na silaha hizo zilizofyatua risasi kwenye hayo magari mawili yaliyoondoka.

7. Polisi imesema wawili kati ya waliotoroka wamepata taarifa zao na majina, umri na sehemu wanazotoka zilitajwa kama kweli si wahalifu si wajitokeze waseme kilichotokea?
 
mtoto wa mjini nakupa homework, angalia maelezo yako halafu anza kujibu moja baada ya jingine objections zinazoweza kutokea dhidi ya hoja zako. Halafu ukiona moja inazidi hoja yako ya kwanza ifute.. halafu uone utabakiwa na maswali gani au swali gani muhimu zaidi. Nitarudi baada ya muda...
 
Mwanakijiji
Nadhani skepticism zako hazitii shaka. Mimi mwenyewe ningependa kujua watu wa uhamiaji/usalama kwanini waliwaruhusu hawa watu waingie Tanzania kama lead ilikuwa imetolewa kutoka Kenya? Walitaka wafanye demage kwanza halafu ndio washughulikiwe? Inakuwaje silaha zinapitishwa kirahisi sana mpakani wakati walikuwa tayari wameambiwa? Hapa siwezi ku-conclude kitu lakini ninachoweza kusema ni kuwa, kuna uwezekano polisi wa Kenya walitaka hawa jamaa wauawe Tanzania na authorities Tanzania ziliafiki hilo, na kuna uwezekano kuwa labda kuna mazingahombwe yaliyofanyika ambayo sisi tunafumbwa. Lakini hata hivi Polisi walioko on the ground bado nitawasifu sana, they have been taking bullets kwa ajili ya kazi yao lakini wanalipwa hela kidogo sana ukilinganisha na kazi zao
 
Bongolander, unafikiri vipi kama Rais Kikwete akitoa leseni ya "ukishukiwa jambazi na ukikutwa na silaha uuawe"? Unafikiri hiyo itawafanya watu wawe na amani zaidi?
 
Bongolander, unafikiri vipi kama Rais Kikwete akitoa leseni ya "ukishukiwa jambazi na ukikutwa na silaha uuawe"? Unafikiri hiyo itawafanya watu wawe na amani zaidi?

Nadhani mfano wako hapo juu auendani kabisa na hii kesi , tukubali tusikubali kuna kujirudia kwa makosa hapa . Ni majambazi toka Kenya walipambana na polisi kama miezi miwili iliyopita huko Arusha na kuiba mamilioni ya shilingi kwenye benki. Inawezekana labda polisi awakuact accordingly lakini kama kweli hawa watu ni majambazi na walikuwa na hizo silaha , na Nchi yao inakiri ya kuwa ni most wanted then sidhani kama kuna haja ya kusumbua mahakama ... Polisi wawaue , najua itasound vibaya lakini usipofanya hivyo watakumaliza wewe.

Jamani tusitake kuwa kama wamarekani na hizi rule za engagement , mpaka vita vinawashinda huko Iraq .
 
Rufiji, demokrasia ina gharama na gharama mojawapo ni kuheshimu utawala wa sheria. Kwa maneno yako unataka tuhalalishe raia kuchukua sheria mikononi. Naomba nirudie tena, sibishanii kama walikuwa majambazi au la....nahoji jinsi walivyouawa...
 
Back
Top Bottom