Majambazi Arusha: Mabomu, Bunduki, Risasi, Bastola - Hii ni Kashfa JWTZ

Ninyi wengine mnachangia humu inaelekea hamuwajui majambazi. Sisi tunaoishi Arusha hasa maeneo ya Sakina, Esso, Unga, tunawajua majambazi kwa sura na majina, na tunapishana nao barabarani, tunakunywa nao katika baa na tunasali nao makanisani! Tusichokiweza ni kuwakamata. Siku jambazi "anapokutembelea", unamwona vizuri sura yake, pengine unamfahamu tangu kabla. Anafanya vitu vyake usiku huo, anaondoka anakuacha amekujeruhi kidogo (kuzima resistance tu), ubaki na nguvu ya kutafuta hela zingine aje kuchukua tena. Na majambazi wengine wakikujua ni mtoaji wa hela bila ubishi, wanakutajia tu bwana kama unataka amani, sisi tunataka sh milioni 4, tuwekee tutakuja kuchukua jioni. Ukiwapa kweli, hakuna shida. Ukienda kushitaki, inaripotiwa tu polisi wanakuambia watafuatilia, inaisha hivihivi unawaona wanadunda mitaani kama kawa. Tena wakikuona wanakuonya "usijifanye mjanja, utajuta!". Na ukiwawekea "resistance" watakayoona inaweza kuwazuia kutimiza lengo lao, hapo ndio wanakuua.

Na hakuna hata siku moja majambazi wanakamatwa kwenye tukio, lakini waathirika wa matukio haya wanawafahamu. Matukio yote aliyofanya Nyari na wenzake ni ya kweli na watu wa Arusha wanayafahamu. Siku hizi katajirika, kwa hiyo huwa haendi tena binafsi "kufanyiza", lakini "vijana" wake wanajulikana. Mambo ya Alex Massawe ndio huwa yanasimuliwa Arusha kama vile sinema za "Rambo", hakuna asiyemjua. Wako majambazi walio-specialize wizi wa magari, na wanajulikana kwa majina na sura zao. Wavunjaji wa mabenki (hawa ndio hatari, huwa hawahurumii mtu katika suala la mauaji), nao wanafahamika, na biashara zao walizozianza baada ya kupata pesa za ujambazi zinajulikana. Kama kuna waandishi wa habari wenye skills za investigative journalism, nawachagiza waende tu Arusha wakatafute data, watashangaa, majambazi wote wanajulikana na data watazipata nyingi mno. Wanunuzi wa vitu vya wizi pale Arusha, wanajulikana, kuanzia wale middlemen wanaovinunua kwa bei ya jumla, hadi wale wanaovifanyia "alteration" na kuvirudisha madukani kuuzwa upya. Majambazi wa Arusha huwa wanaenda kuvunja nyumba wakiwa na "orders" tayari ya mahali pa kupeleka watakavyoviiba, na ni usiku huohuo wanapokea hela yao. Barons wengine wa ujambazi huwa wanatoa "advance payments", wanamalizia pale bidhaa inapoletwa.

Mie leo hii nina orodha ya majambazi ambao nikisikia wameuawa sitauliza mazingira ya kufa kwao yalikuwaje, nitashangilia tu! Mtu anakuvamia, anakuumiza anaishia, unaendelea kumuona mtaani anapita kibabe, wala haoni aibu yoyote! Sasa huyo hata nikipewa nafasi ya kumvizia barabarani nimmalize ningefanya hivyo, lakini bahati mbaya wao wana nyenzo zaidi, kwa hiyo tunabaki kusononeka tu na "kumwachia Mungu"!

Waacheni polisi wawaue majambazi. Tena ingewezekana wasisubiri kuwakamata kwenye tukio, wale wanaojulikana wawavizie tu na kuwamaliza, basi! Wananchi wanawajua majambazi, na siku akiuawa ambae sio utaona malalamiko. Na polisi wanawafahamu pia, wote. Labda hawajapewa ruhusa rasmi ya kuwaua, au sijui kuna nini. Mnakumbuka ile kesi ya Zombe, aliyekuwa kaimu RPC Dar? Kwa nini wananchi walilalamika? Kwa sababu wale waliouawa hawakuwa majambazi na wananchi wana uhakika huo, na hata uchunguzi ulipofanywa ilithibitishwa hivyo. Kumbuka kila mara tumesikia polisi wakiua majambazi lakini hatukusikia malalamiko hayo. Kumbe wananchi tunazo taarifa za kutosha sana za ujambazi, lakini kwa bahati mbaya kinachotumika mahakamani kumtia hatiani jambazi si ukweli (facts), bali ni sheria (ambazo wanasheria wanazichezea watakavyo) na nguvu ya ushahidi (ambao pia wanasheria wanaudhoofisha hadi hatua ya kuitwa ushahidi "dhaifu"), kisha jambazi anaachiwa. Unakwenda kutoa ushahidi dhidi ya jambazi ambaye siku unaibiwa ndiye aliyekuelekezea bastola kichwani ukamkabidhi ufunguo wa gari yako akaondoka nayo. Unamkumbuka kwa uhakika kabisa! Basi wakili wake anakuyumbisha pale na maswali ya maudhi, mwishoni inaonekana kwamba ushahidi wako ni "dhaifu", mtu aliyekunyang'anya ki-baluni chako anaachiwa hivihivi! Utajisikiaje? Na hapo kwa mwalimu wa sekondari, bei ya "ki-baluni" second hand ni sawa na kulimbikiza mishahara ya miaka 3 mfululizo, ukiwa unalishwa na mkeo (mwalimu wa primary, anaongezea na tuisheni sh 100 kwa siku, na mnalima mchicha na kufuga kuku wa kienyeji), kwa mategemeo kuwa hiyo gari ungefanza teksi ukusanye 12,000 kwa siku, ijilipe in 2 years ndipo uanze kukusanya kafaida ka kupeleka wanao sekondari. Na bado majambazi tunawajua, tunawaona mitaani, lakini hatuna "ubavu" wa kuwadhibiti!

Acheni polisi wawaue majambazi. Tena kwa kufanya hivyo wanatupa moyo wananchi kuwa serikali ipo, na tunajipa moyo kuwa hata hao ambao bado hawajakamatwa siku yao ipo. Nakuhakikishia kuwa nikisikia kuna mchango wa kuunda kikundi cha "hitmen" wa kutafuta jambazi mmojammoja na kuwatungua, (angalao wale ninaowajua mimi), ningetoa huo mchango tufanye hiyo kazi wenyewe. Polisi wafanye hiyo kazi maana viginevyo wananchi tukiingilia kati itakuwa fujo, hadi sasa tumechoshwa kabisa tunaishi kwa hofu!

Hongereni polisi kwa kuua majambazi, endelezeni mapambano.
 
Muzic 4 Peace

[media]http://youtube.com/watch?v=5BHNMwzwb-A[/media]

Afro Moses Live

[media]http://youtube.com/watch?v=rFH01BtMCIA[/media]

African Music

[media]http://youtube.com/user/motomuzic[/media]

Yap
 
Hii ni nyeti best,

Niko Arusha today I will try to do something on this issue. So touching man
 
Back
Top Bottom