Polisi wamewazoesha raia mabomu na risasi sasa raia hawaogopi tena na polisi sasa hawako salama

Tulimumu

JF-Expert Member
Mar 11, 2013
13,188
2,000
Polisi waliua zaidi ya raia 23 waliokuwa wakiandamana kwa amani Zanzibar wakati wa maandamano ya amanii ya CUF kupinga matokeo ya uchaguzi. Hakukuwa na sababu ya askari kutumia silaha za moto katika maandamano yale.


Polisi waliua watu watatu kule Arusha wakati wa maandamano ya amani ya CHADEMA. Hakukuwa na sababu ya polisi kutumia risasi katika maandamano yale


Polisi wanadaiwa kumuua mwananchi mmoja kule Morogoro wakati wa mkutano wa CHADEMA. Hakukuwa na sababu kwa polisi kuzuia mkutano na maandamano yale na kusababisha mauaji yale


Mwandishi wa habari Daud Mwangosi aliuawa na bomu kule Iringa wakati akiripoti mkutano wa ndani wa CHADEMA. Hakukuwa na sababu ya kutumia nguvu na silaha na katika hali ya kushangaza zaidi aliyeratibu na kusimamia mauaji yale akapandishwa cheo!


Polisi wanatuhumiwa kutesa, kujeruhi na kuua watu huko Mtwara kutokana na upinzani wa gesi kupelekwa Dar.

Polisi wamelipua mabomu, kuwapiga na kuwajeruhi wanafunzi wa vyuo vikuu wanaoandamana kudai mikopo. Hakukuwa na sababu

Polisi wameua watu kule Ruvuma kisa eti walikuwa wanaandamana kwenda kwa mkuu wa mkoa kumtaka akomeshe mauaji. Maandamano yalikuwa ya amani lakini polisi wakayatawanya kwa risasi watu wakafa


Polisi wamelipua mabomu katika mkusanyiko wa maombolezo ya CHADEMA kule Arusha bila sababu.


Mifano yote ya matukio niliyoyatoa hapo juu yanathibisha hoja yangu kuwa matumizi ya mabomu, risasi na virungu katika mikusanyiko ya amani ya wananchi imewafikisha mahali sasa hawaziogopi tena silaha hizo na sasa umefika wakati raia wameanza kuwa sugu na kutoogopa tena milipuko ya mabomu na milio ya risasi hivyo wako tayari kupambana na mtu yeyote awe askari au kiongozi mwenye silaha . wameshajua jua kuwa katika kudai haki silaha haziwezi kuzuia kwani risasi zikiisha mwenye silaha anakuwa kama mbwa asiye mna meno.


Ndipo tunaposhuhudia sasa raia wakivamia vituo vya polisi na kuvichoma moto pamoja na polisi kuwatishia kwa risasi na kuwaua lakini wananchi hawaogopi tena. Wanajua kuwa watakufa lakini wanajua kuwa wengine watabaki na kufanikiwa kushughulikia makatili. Tumeona Mwanza kigogo alidhani bastoa ndio jibu la ukubwa wake. Aliua lakini nae aliuawa kwa mawe kama kibaka


Sasa hivi hali ni mbaya zaidi kwani matukio ya raia sasa kupambana na polisi wenye silaha na watu wenye silaha yanatangazwa sana kwenye vyombo vya habari kiasi kwamba wananchi wa sehemu nyingine nao wanajifunza kutoka kwa wenzao. Hii yote ni kwasababu ya ukosefu wa busara wa jeshi la polisi kufikiri wakiwa na silaha wanaweza kuwadhibiti raia wenye kiu ya haki. Polisi sasa wavae mabomu na wazunguke na silaha lakini hiyo sasa haiwahakikishi wao wenyewe usalama kwasababu wameshawazoesha wananchi silaha hizi kwa kuzitumia katika shughuli za amani kijamii. Hivi nani atakubali kufyata mkia anapoona mwanae, babake au jirani yake anauawa mbele yake bila sababu halafu akae kimya kama kondoo? Lazima atalipiza na kama naye atakufa wengine watakuja kumsaidia na hatimaye mwenye silaha naye atakufa tu.Lakini ni lini polisi walikuwa wanapambana na majambazi na kuwaua halafu wananchi wakawavamia polisi? Hawawavamii kwasababu wanaona silaha imetumika kuwalinda na sio kuwaua wao wasiokuwa na hatia kama nilivyoeleza hapo juu.


Hivyo matukio tunayoyasikia sasa kutoka Mwanza, Morogoro na kwingineko ni ishara ya raia sasa kuwa sugu kwa silaha za moto kwani zimeshatumika kuangamiza raia wasiokuwa na hatia hivyo hawaogopi tena kupambana nazo wanapoona haki haitendeki. Hivi kama watu wanaandamana kwa amani kwanini wasiachwe wakisha maliza ndipo viongozi husika waitwe polisi kujieleza na wasipotekeleza wito wakamtwe kisha washitakiwe badala ya kuwapiga, kuwajeruhi na kuwaua raia wasiokuwa na hatia waliokuja kusikiliza au kuangalia mikutano. Ukijumlisha yote utagundua polisi wetu wamefunzwa kutumia nguvu tu kwa kila kitu hivyo suala la busara ni kiyunani kwao. Utakuta watu katika mikutano wameshasalimu amri wamenyoosha mikono juu lakini bado polisi wanawapiga virungu. Mtu atakuwa amekubali kukamatwa lakini hawaridhiki lazima wamburute na kumpiga virungu wakiamini bila hivyo
 

m4cjb

JF-Expert Member
Jul 23, 2012
7,374
2,000
Rock city tunayatumia mawe yetu vizuri na kwa vile MUNGU alitujalia milima mingi ya mawe,insallah tutayatendea haki! hatutaki upuuzi wa mizigo kwa sasa.kama noma na iwe noma!
 

m4cjb

JF-Expert Member
Jul 23, 2012
7,374
2,000
Na mimi nasema,WAPIGENI TU WOTE WANAOWADHURUMU HAKI ZENU IKIWEMO HII YA KUANDIKISHWA NA KUPIGA KURA! CC PINDA
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom