Abuu Said
JF-Expert Member
- Jul 5, 2015
- 4,009
- 4,776
Unafikiri Magufuli hatagombea 2020. Hao wasubiriage 2025 na pia inawezekana wasiwe wao akatokea mwingine kwani mlijua kama Magu atakuwa president .alikuwa Hana wanaomuunga mkono mpaka sehemu zingine fomu alienda masokoni, vijinini. Yeye mwenyewe anakuambia ni Mungu Tu ndio alijua hata yeye hakujua. Akina Membe ,Sitta, Lowass,, Mwandosya,Rose migiro Hadi akina January, mwigulu walimzidi mh Magu Kwa uungwaji mkono mwisho wa siku aliibuka mshindi bila watu kutokujua kinachoendelea mpaka anaapishwa Kuwa president.Hawa ndio Wahusika wakuu wa 2020
1. Kasim Majaliwa
2. Dkt. Hussein Mwinyi
3. January Makamba
Mark my words!
Sent using Jamii Forums mobile app
Hivyo havina faida, wanasiasa huangalia akili za watu na kutumia makundi ya dini kufanikisha malengo yao.Nafikiri ukristo, uislamu na upagani hakuna faida yoyote. Bora hekima aliyoiomba nabii Suleiman. Kwani sasa ukristo unatudaidia nini sasa?! Zaidi ya [emoji40] [emoji87]
Sent using Jamii Forums mobile app
Unafikiri Magufuli hatagombea 2020. Hao wasubiriage 2025 na pia inawezekana wasiwe wao akatokea mwingine kwani mlijua kama Magu atakuwa president .alikuwa Hana wanaomuunga mkono mpaka sehemu zingine fomu alienda masokoni, vijinini. Yeye mwenyewe anakuambia ni Mungu Tu ndio alijua hata yeye hakujua. Akina Membe ,Sitta, Lowass,, Mwandosya,Rose migiro Hadi akina January, mwigulu walimzidi mh Magu Kwa uungwaji mkono mwisho wa siku aliibuka mshindi bila watu kutokujua kinachoendelea mpaka anaapishwa Kuwa president.
Sent using Jamii Forums mobile app
Kabisa kama ilivyotokea 2015, hakuna aliyedhani yangetokea yaliyotokea
SGR,Bomberdier,Stiegles,,Heshima mitaani,Mafisadi,heshima kwa wafanyakazi wa Umma..nk.nk..Watanzania wana macho na wanashuhudia pamoja na juhudi zenu za kupinga maendeleo.
2020 Makonda anaweza akagombea ubunge alafu akachaguliwa kuwa waziri mkuu, nyota ya Majaliwa ikaanza kufifia haya yote yanaweza tokeaHakuna kitu cha maana kitajiri hivi karibuni, mpaka karibia na uchaguzi wa 2020, kutakuwa na purukushani za uchaguzi. Uchaguzi wa 2020 mtawala ni mwenyekiti, atajipitisha. Tutarajie mabadiliko na uasi mkubwa dhidi ya utawala karibia na 2025.
hakuna waziri mkuu aliyewahi kuwa rais..
Mmiliki mkubwa wa chama ni mwenyekiti na yeye anaweza kuja na majina mfukoni au akabadilisha katiba ya chama mapema kabla ya 2025 ili amchague anaemtaka wote wanamuogopa jiwe.Jina lilitoka mfukoni. Utaratibu wa kutoa mtu kusikojulikana na kumpa dhamana kubwa ya Urais sasa hivi kila mtu hata ndani ya CCM wanauogopa. Achana na hawa vijana wa humu wanaotumwa kuja kumuunga mkono kwa malipo kidogo. Naongelea wamiliki wa Chama, tena sio watu kama Polepole, huyo sio mmiliki, huyo amewekwa tu kupiga kelele.
Pamoja na kwamba Majaliwa hapendi mambo mengi ya ajabu anayofanya mtawala, lakini mtu pekee ambaye atajaribu kufunika uovu wa mtawala wa sasa kwa kadri atakavyoweza ni Majaliwa. Tayari mikakati rasmi ya ndani ya kambi kadhaa za KiCCM zinazowania kwa udi na uvumba nafasi ya Urais 2025 zimeshajipambanua. Majaliwa anakubalika kwa kiasi fulani na kambi zote na zipo tayari kumpisha iwapo mambo yatakuwa magumu pande zao.
Watu wanaojaribu kujenga haiba au wenye haiba ya kuukwaa Urais 2025 ni:
1. January Makamba (Hapiti)
2. Majaliwa Kasimu
3. Dk. Augustine Mahiga
4. Khamis Kigwangallah (Hapiti)
5. Dr. Ali Mohamed Shein
6. Huyu nani Muhammed Seif Khatib?
7. Samia Suluhu
8. Balozi Amina Salum Ali
9. Balozi Ali Karume
10. Hussein Mwinyi
Watu wengine ambao walikuwa ni potential candidates (kwa kiwango cha akili ya CCM) lakini wamepotezwa ni pamoja na
1. Prof. Sospeter Muhongo
2. Dk. Asha Rose Migiro
3. Bernard Membe
4. Dk. Mohamed Gharib Bilal
Kuna watu kama Peter Nyalali, Prof Mark Mwandosya, Hassy Kitine, Dk. Harrison Mwakyembe (unafiki mwingi), hata mtu hujui usemeje kuhusu wao!
Kuna watu kama Mwigulu Nchemba ambao ndoto zao zimekufa kibudu, huyu kuna mtu hataki hata kumsikia.
Pia kuna watu waliofia kusikojulikana kama Lazaro Nyalandu.
Utawala huu hautaki kabisa mgombea ambaye ataonekana kurudisha uongozi wa kidemokrasia, mfano retired Chief Justice Augustino Ramadhani, kwa nia ya kuogopa kumulikwa matendo yao. Pia iwapo kamari ya Majaliwa (anaweza kumgeuka) haitawezekana Rais ajaye anaweza kutokea Jeshini kwa matakwa binafsi (mfukoni kwenye koti la mtu).
Pamoja na hizo orodha hapo juu, Rais ajaye ni mwanaume na ni Mwislamu.
Awamu ya 2025 mtu kuibuka au kuibuliwa kusikojulikana na kugombea Urais kama ilivyotokea kipindi cha nyuma hakutatokea.
Kuna watu ambao umri huenda ikawa ni kikwazo kwao (wamezeeka). Ndani ya CCM kuna kambi nyingi, lakini zote zinaangukia katika makundi makuu 3:
1. Kambi zenye utawala wa mrengo wa kidemokrasia
2. Kambi zenye utawala wa mrengo wa kibabe
3. Kambi zenye mrengo wa utawala wa katiba mpya hasa inayomwajibisha na kumpunguzi Rais madaraka
Kati ya ujinga ambao Jiwe hatakiwi kufanya ni kumweka Mkonda uwaziri mkuu. Hadi wanaCCM wenye akili watacheka kimoyomoyo, lakini swala hilo litamfanya apate upinzani mkali vibaya mno hasa kuelekea 2025.2020 Makonda anaweza akagombea ubunge alafu akachaguliwa kuwa waziri mkuu, nyota ya Majaliwa ikaanza kufifia haya yote yanaweza tokea
Sent using Jamii Forums mobile app
Huwezi ukaisikia maana ilikuwa ana kwa anaHii qoute sijaisikia hii
Mmiliki mkubwa wa chama ni mwenyekiti na yeye anaweza kuja na majina mfukoni au akabadilisha katiba ya chama mapema kabla ya 2025 ili amchague anaemtaka wote wanamuogopa jiwe.
Sent using Jamii Forums mobile app