Majaliwa Ndio Mgombea wa Urais 2025

The New Bruce Lee

Senior Member
Jul 21, 2018
103
243
Pamoja na kwamba Majaliwa hapendi mambo mengi ya ajabu anayofanya mtawala, lakini mtu pekee ambaye atajaribu kufunika uovu wa mtawala wa sasa kwa kadri atakavyoweza ni Majaliwa. Tayari mikakati rasmi ya ndani ya kambi kadhaa za KiCCM zinazowania kwa udi na uvumba nafasi ya Urais 2025 zimeshajipambanua. Majaliwa anakubalika kwa kiasi fulani na kambi zote na zipo tayari kumpisha iwapo mambo yatakuwa magumu pande zao.

Watu wanaojaribu kujenga haiba au wenye haiba ya kuukwaa Urais 2025 ni:

1. January Makamba (Hapiti)

2. Majaliwa Kasimu

3. Dk. Augustine Mahiga

4. Khamis Kigwangallah (Hapiti)

5. Dr. Ali Mohamed Shein

6. Huyu nani Muhammed Seif Khatib?

7. Samia Suluhu
8. Balozi Amina Salum Ali
9. Balozi Ali Karume
10. Hussein Mwinyi
11. SULEIMAN JAFFO

Watu wengine ambao walikuwa ni potential candidates (kwa kiwango cha akili ya CCM) lakini wamepotezwa ni pamoja na

1. Prof. Sospeter Muhongo
2. Dk. Asha Rose Migiro
3. Bernard Membe
4. Dk. Mohamed Gharib Bilal

Kuna watu kama Peter Nyalali, Prof Mark Mwandosya, Hassy Kitine, Dk. Harrison Mwakyembe (unafiki mwingi), hata mtu hujui usemeje kuhusu wao!

Kuna watu kama Mwigulu Nchemba ambao ndoto zao zimekufa kibudu, huyu kuna mtu hataki hata kumsikia.

Pia kuna watu waliofia kusikojulikana kama Lazaro Nyalandu.

Utawala huu hautaki kabisa mgombea ambaye ataonekana kurudisha uongozi wa kidemokrasia, mfano retired Chief Justice Augustino Ramadhani, kwa nia ya kuogopa kumulikwa matendo yao. Pia iwapo kamari ya Majaliwa (anaweza kumgeuka) haitawezekana Rais ajaye anaweza kutokea Jeshini kwa matakwa binafsi (mfukoni kwenye koti la mtu).

Pamoja na hizo orodha hapo juu, Rais ajaye ni mwanaume na ni Mwislamu.

Awamu ya 2025 mtu kuibuka au kuibuliwa kusikojulikana na kugombea Urais kama ilivyotokea kipindi cha nyuma hakutatokea.

Kuna watu ambao umri huenda ikawa ni kikwazo kwao (wamezeeka). Ndani ya CCM kuna kambi nyingi, lakini zote zinaangukia katika makundi makuu 3:

1. Kambi zenye utawala wa mrengo wa kidemokrasia
2. Kambi zenye utawala wa mrengo wa kibabe
3. Kambi zenye mrengo wa utawala wa katiba mpya hasa inayomwajibisha na kumpunguzi Rais madaraka
 
2025 tukipitisha tena ccm tena. Kuna haja ya kupima watu akili mana badala ya watu wa 4 kuna kichaa mmoja yaeza kuwa baada ya mtu mmoja kuna kichaa mmoja. Hata kama wataiba

2025 ndipo umafia wa hali ya juu utatumika kuipitisha CCM.
 
Majaliwa hapana, January Makamba na Mwandosya wanafaa sana nikiangalia CCM nzima na wote uliyowaorodhesha.

January Makamba sahau, ana mrengo wa utawala wa zamani (wa Kikwete), mbabe wa sasa hivi hatakubaliana na hilo kwa sababu hizo tawala mbili zinahasimiana. January will be thrown in the same basket like Membe.
 
January Makamba sahau, ana mrengo wa utawala wa zamani (wa Kikwete), mbabe wa sasa hivi hatakubaliana na hilo kwa sababu hizo tawala mbili zinahasimiana. January will be thrown in the same basket like Membe.
Nakubaliana na wewe Chief, ila kwa ustawi wa Taifa hili, namuona January anafaa sana...kama ulivyosema kupata hiyo nafasi ni ngumu sana, lakini inawezekana, AJIPANGE.
 
Kuna watu umewasahau wapo kimya wataibuka kipindi hicho na kushinda. Unafikiri Ridhiwani hatagombea, mwigulu , Dr Tulia, Bashe, Nape, Hussein Mwinyi ,Jafo, Kabudi n.k. watu kibao Ila kuna watu umewataja age Yao haitawaruhusu walioabove 60 Kwasasa kipindi hicho watakuwa 70+. Mawaziri wakuu wote wastaafu ulikuwa ngumu kuupata Urais eg kawawa,sokoine,Salim,warioba,msuya,malecela, lowasa,sumae,pinda etc. Nafasi ya kassim inaweza Kuwa ngumu. In general hatajulikana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
11 Reactions
Reply
Back
Top Bottom