Chizi Maarifa
JF-Expert Member
- Jul 29, 2013
- 14,695
- 32,273
Ok. Nlidhani ni Ziwa JipyaSorry. Ni ziwa Nyasa
Ok. Nlidhani ni Ziwa JipyaSorry. Ni ziwa Nyasa
Ni kweli kaka ukimpoteza mzazi ambaye ni rafiki. Hakika lazima uyumbe kidogoPolee Sana..
I can Feel your pain Through Narrative Words..
Polee sana..
Umenikumbusha Nilivompoteza baba Yangu..
Maumivu ya kupoteza mzazi ambaye pia ni Rafiki yako na anayekuelewa Nayajua vizuri..
Maumivu hayo yalinichukua Muda sana kukaa In Normal States. Sikuwa naamini Kuwa Dunia ni Kitu halisia nilihisi Ni Illusion tu..
Nilikosa huruma,Nilipoteza Muelekeo Ilinichukua Miaka minne Kurealise kwamba Kila kitu Kinapangwa na kinatokea kwa Sababu..
Through nakukumbuka Mzee wangu ila umenifunza Vingi sana Baada ya kifo chako..
Uendelee kupumzika kwa Amani
Ok. Nlidhani ni Ziwa Jipya
Hebu straight tueleze ulipoharibu maisha yako. Pole kwa kuondokewa na mama.Habari wanaJF, bila shaka kila anayesoma hapa ni mzima na afya, na kama sio Mungu akupe lililo hitaji la moyo wako [emoji1488]
Mimi ni kijana wa miaka 30. Nimezaliwa mkoa wa mwanza, nimepata elimu yangu ya msingi huko mkoani mwanza. Nilimaliza kwa ufaulu wa kawaida lakini nilifanikiwa kuchaguliwa na kuendelea na elimu ya sekondari huko huko mkoani mwanza.
Mimi ni mtoto wa 2 kati ya 3 ambao tumelelewa kwa pamoja, japo nna dada zangu wengine wawili ambao hatukukua pamoja muda mwingi (Baba alikua na watoto wawili kabla hajaoa) so jumla yetu tuko watano (5)
Maisha ya nyumbani yalikua ya kawaida tu sio matajiri na sio masikini. Na nimekua kwenye malezi ya maadili ya kiafrika kabisa.
To cut it short
Kwenye kukua kwetu hatukuwa tukiomba hela kwa baba maana tulikua tunamwogopa, mzee alikua mkali balaa so kila kitu tulikua tukiongea na mama. Mama alikua mtu mwenye upendo sana kwa wanae na alipambana kwa namna yoyote kuhakikisha watoto wake tunasoma na kuwa vijana bora. Pesa ya kula shule, nauli, madaftari na kila kitu tulikua tukipewa na mama. Sio kwamba Baba hakua anatoa chochote kabisa lakini najaribu tu kuonyesha kwamba Mama ndo alikua rafiki yetu sana kuliko mzee. Japo fimbo na vibao vingi tumepigwa na mama kuliko mzee.
Nilipomaliza darasa sa saba, Kaka yangu alikua form 2 kwa wakati huo na alikua akisoma shule ya private. Kwa upande wangu matokeo ya darasa la saba sikuweza kuchaguliwa first selection. (Sikua na alama za kutosha) kama nilivyosema hapo juu nilifaulu kawaida ntafafanua mbele.
Mama alinipeleka shule ya private ambayo kaka yangu anasoma kwa wakati huo na nilifanya interview na kupewa majibu ndani ya siku 2 kuwa nimefaulu naweza kujiunga na shule hiyo ili kuendelea na elimu ya sekondari.
Nakumbuka baada ya mwezi hivi (sina uhakika sana) second selection ilitoka na nilikua nimechaguliwa shule flani iko wilaya ya ilemela (Jina nahifadhi). Ilikua ni shule mpya kabisaa kwa kipindi hicho zilkua na jina maarufu zikiitwa shule za kata. So nilichaguliwa shule ya kata.
Mama alisema niendelee kusoma kwenye shule hiyo ya private lakini niliona kama hayuko sahihi maana hali yake ya uchumi haikua nzuri hata ada najua alikopa. Ila kwa umri ule nisingeweza kumshauri kitu zaidi ya kusema sawa mama. Na maisha yaliendelea.
Mama yangu alikua mtu wa upendo sana na mchakarikaji. Niseme tu nilikua nampenda sana mama na nilikua ni yule mtoto wa mama (mamaz boy). Ilipita wiki kadhaa na mama alianza kuumwa serious. Alikua akilalamika siku za nyuma lakini wakati huu alisisitiza kuwa hajisikii vizuri hivyo alituaga na kuondoka kwenda hospital kwa matibabu.
Aliondoka majira kama ya saa sita nakumbuka na aliahidi angerejea baada ya matibabu.
Kuna hospital moja ipo Mwanza kwa kipindi hicho ilikua ikiitwa Mission, iko maeneo ya Ghana kama sikosei, sina hakika kama bado iko pale hadi leo.
Taarifa za mama kuumwa hazikua nzuri kwangu maana Mama hakufanikiwa kurejea nyumbani siku hiyo.
Mimi (Nijiite Amani…Sio jina halisi) nilikua yule mtoto ambaye hata mama akitoka ikifika saa 3 usiku hajarudi basi wasiwasi na uoga ulikua unakua mwingi.
Sasa hii siku mama hakurudi kabisa na nilikua na wasiwasi sana hadi hapo mama mdogo alipokuja home majira ya jioni ya kutupa habari kuwa mama amelazwa katika hospital hiyo ya Mission. Kama kumbukumbu zangu ziko vizuri ilikua ni weekend.
Maisha yaliendelea na tulikua tukienda kumwona mama. Jumatatu tulienda shule kama kawaida, nilikua nikiondoka na kaka yangu kwani alikua ananizidi madarasa 2 hivyo alikua ananiongoza vyema tu. Kaka yangu aliwahi sana kujitambua hivyo hakuwa msumbufu sana kwa mama kama mimi.
Mimi nilikua hata nikitoka shule sina muda wa kusoma, ni michezo hadi usiku so hata maendeleo yangu shule hayakua mazuri sana ukiringanisha na kaka yangu.
Mama aliendelea kupatiwa matibabu kama siku 3 hivi lakini hakuonyesha nafuu hivyo alipewa rufaa kwenda Hospital ya Bugando.
Nilikua na ratiba kila nikitoka shule naunga moja kwa moja hadi Bugando kwenda kumsalimia mama. Nilikua natoka shule saa nane na nusu hvyo hadi kufika saa kumi muda wa kuona nilikua nimeshafika pale Hospital.
Kuna muda nilikua nazuiliwa na walinzi maana kwa kipindi hicho walikua na utaratibu wa kuzuia watoto kwenda kuona wagonjwa. Sasa mimi na umbo langu dogo dogo nilikua naonekana mdogo so kuna muda sikua nafanikiwa kuingia hadi niwe na mtu mzima
Hali ya mama haikua nzuri kwakweli maana baada ya kama siku kumi hivi, Nakumbuka hiyo siku nilienda kumwona mama nikakuta amewekewa mashine ya Oxygen, ndo ilikua mara yangu ya kwanza naona mtu kawekewa ile mirija puani.
Nakumbuka nilianza kulia pale na mama mdogo alinitoa nje maana nilikua nalia alafu mama ananiangali wakati huo alikua hawezi hata kutoa sauti ukaisikia so alikua ananiangalia na nilikua naona kabisa anaumia kuona nalia.
Tulirudi nyumbani siku hiyo na usingizi ulikua wa shida sana nawaza mama amekuwaje. Hali ya home pia haikua nzuri kwani kwa kipindi chote hicho mama hakuwepo nyumbani.
Pale nyumbani tulikua na kiduka ambacho kilikua kinaendeshwa na mama na ndipo hapo tulikua tukipata hela ya nauli pamoja na ile ya kula shule. So wakati wote ambao mama hakuwepo hata mapato dukani yalipungua kwani bidhaa nyingi zilikua zimeisha usimamizi hakua mzuri.
Ni baada ya kama siku 2 tu nikiwa nimetoka hospital kumwona mama. Wakati huo sikua naruhusiwa tena kwenda kumwona kutokana na kile kitendo cha kulia.
Hii siku nilitoka shule nikaenda moja kwa moja home lakini ilipofika jioni baadhi wa watu waliotoka hospital walinipa taarifa kuwa hali ya mama bado si nzuri.
Usiku wake baba alipigiwa simu akiambiwa mama hali yake ni mbaya na alienda moja kwa moja hospital.
Baaba ya masaa kama mawili nilishtuka kwa kelele za vilio kutoka kwa mama zangu wadogo.
Mama alikua amefariki tayari
NITAENDELEA… Leo Leo
Usiku wake baba alipigiwa simu akiambiwa mama hali yake ni mbaya na alienda moja kwa moja hospital.
Baaba ya masaa kama mawili nilishtuka kwa kelele za vilio kutoka kwa mama zangu wadogo.
Mama alikua amefariki tayari
Bado kipande kirefu kidogo kufika huko.. Tuwe wavumilivu mkuuHebu straight tueleze ulipoharibu maisha yako. Pole kwa kuondokewa na mama.
Sema dogo na dkt mmemsema sana mpaka amehitimisha ki bongo moviePole sana Tumetoka kwa Uzi wa Dogo na Dkt huku kumewaka tena
Yule Dogo kiazi sana yaaniSema dogo na dkt mmemsema sana mpaka amehitimisha ki bongo movie
Haya tuendeleeBado kipande kirefu kidogo kufika huko.. Tuwe wavumilivu mkuu
😂😂😂 ulitupwa Lufilyo kaka mkubwa, mpaka miaka ya 2015 mi naenda kule barabara zilikua mbovu sijui hiyo 2010 hali ilikuaje aisee.SEHEMU YA SABA (7)
Tulipoishia…
Asubuhi niliondoka na Clara alisubiri hadi bus liondoke ndo akaondoka ila alikua na maumivu makali mno na hata tembea yake haikua kawaida.
Wakati niko njiani tulikua tukichat na alinijulisha kuwa anaumwa sana, amepata hadi homa. Nilimpa pole nyingi na kumwambia ajikaze home wasijue.
Kwa upande wa Jane baada ya kumaliza form 4 alienda Dar kwa mpenzi wake baadae akaenda mwanza kwa dada yake (niliambiwa na mwenzake) lakini taarifa niliyokuwa nayo wakati naenda Advance ni kuwa Jane tayari ana mimba kubwa tu.
Tunaendelea….
Nilifika dar majira ya saa tano usiku, na hii ndo ilikua mara yangu ya kwanza kuja Dar. Aunt alituma mtu aje kunipokea na joto ndo lilinipokea vizuri.
Aunt wa Dar ana maisha yake mazuri tu na sitotaka kuongelea chochote kuhusu maisha ya kwa Aunt ila kwa ufupi sana ni maisha poa na kila mtu na time zake, mtakutana jioni muda wa kuangalia habari na kula labda
Kesho yake kuna Dada yangu alinipeleka Mwenge na Kariakoo kununua vitu vya Shule. Nilikaa Dar kama siku 4 then safari ya Mbey ikaanza.
Wakati natoka Dar nilikua na kila kitu cha shuleni. Aunt wa Dar alininunulia ( aunt wa Dar tumwite B. Mkubwa ili kutofautisha na wa Bukoba)
Account yangu ya CRDB iliwekwa laki 2 na B. mkubwa kama Pocket money ya shule then nikapewa nauli na pesa ya kula njiani. Nilinunuliwa counter Book 12, vitabu 6 na kila hitaji nilipewa. Mzee mwanza pia alinipa hela ila nilikula bata yote nilivyofika Dar ikiwemo kununua nguo mpya.
Safari ya Mbeya ilikua safi tu na nilifika Mbeya Tukuyu majira ya saa nne na nusu hivi usiku. Wakati niko njiani kuna mbaba nilikaa nae alikua ni doctor huko Kyela na alitokea kunikubali sana na tulibadilishana namba.
Changamoto ilikuja pale nilipofika Tukuyu na kujikuta nimebaki na Cash kama elfu 17 tu. Sasa nikauliza bank iko wapi, Dreva tax alinijibu “huku hakuna CRDB, kuwa linakuja gari (Mobile Bank) sijui kama niko sahihi linavyoitwa. Hilo gari huwa linakuja siku ya jumatatu tu na linatoa huduma na kuondoka”. Asee nilichanganyikiwa na sikuwa na mwenyeji yoyote Mbeya kwa wakati huo. Niliomba dreva Tax anipeleke lodge yoyote ya bei ndogo. Jamaa alinifanyia uhuni, Lodge ilikua sehemu ya kutembea kwa dak 2 tu ila jamaa akanizungusha njia ya mbali na akanipela hapo Lodge nikampa buku 3. Pale Lodge nililipa elfu 10 nikalala huku nikiwaza asubuhi naendaje Mbeya mjini maana nilikua mgeni kabisa na mfukoni nna kama elfu 4 tu.
Niliamka asubuhi nikajiandaa then nikaenda mapokezi nikamwomba jamaa aniangalizie mizigo yangu.
Nilipanda costa za Tukuyu - Mbeya nauli ilikua buku 3 kama sikosei. Safari ikaanza nami macho yangu yote yalikua barabarani nikijisemea ntakapoona ATM ya CRDB basi nashukua.
Nilishuka Mwanjelwa pale baada ya kuona ATM then nikatoa pesa kama laki hivi. Nilinunua godoro, blanketi na koti jeusi. Ile shule tulikua tunavaa full black… Yani shati white, suruali black na koti Black… suit kabisa yani.
Nikarudi Tukuyu na kubeba vitu vyangu tayari kwenda shule. Yule dreva tax nilichukua namba yake na tulikuja kuwa washkaji baadae. Alinipeleka hadi stand ya kwenda huko ndani ndani (Mbambo, Itete hadi shuleni penyewe)
Sasa pake stand nilikutana na wanafunzi kibao wanaoenda shuleni ila cha kushangaza usafiri ulikua Canter na sio mabasi… Yani mnaning’inia huko juu kwenye canter.. wanawake ndo wanakaa chini. Asee niliishiwa nguvu baada ya kusikia hivyo.
Canter inajaza balaa na mizigo ni mingi mnoo kwani watu huja Tukuyu kununua mahitaji mengi na wengi ni wafanyabiashara kule kijijini.
Safari ilianza kama baada ya masaa mawili hivi na wanafunzi tulikua tunapiga story nyingi mnoo na swali kubwa ilikua ni kuulizana we umetokea wapi. Peke yangu ndo nilikua natoka Bukoba.
Ile safari ilikua ya mateso sana. Barabara ni vumbi, madaraja ya mbao alafu barabara ina milima na kona balaa (watu wa Mbeya hususani Tukuyu wananielewa vizuri hapa)
Ilikua Gari ikilalia upande wetu nasali sana maana ukiachia zile bomba ndo uko chini hivyo
Nilianza kujuta kwanini sikusoma Bukoba tu. Baada ya masaa matatu na nusu hivi tulifika shuleni… Asee nilihisi kuna kitu kimenikaba kooni kama nataka kulia kama nimebanwa (hii hali mnaijua wengi) kwa ufupi ningekua mtoto ningelia
Shule ilikua mwisho kabisa. Yani kata ya mwisho kabisaa baada ya hapo kuna Mlima Living stone so hakuna namna utaenda kokote.
Tulipokelewa shuleni tukaonyeshwa mabweni then tukaenda kula mtaani siku hiyo maana tulifika watu washapewa chakula cha jioni shuleni pale.
Nilifanikiwa kupata marafiki wengi na maisha ya kuishi mbali na wazazi yakaanza rasmi
Tuishie hapa kwa leo
See you kesho
Ooh safi sana. Linaitwaje ili nitafute muda nikalitembelee... Limeanzishwa lini?Jipya lipo kijijini kwenu
Hiyo ni Lufilyo, ingekua mwakaleli angeshukia katumba na sio tukuyu.Najaribu kufikiria shule iliyo chini ya safu ya milima ya Livingston ni Luteba Mwakaleli
Mlikua mnaenda kucheza disco lupata sec, aisee life la kule bna. Ni bush ila unakamatika na starehe za wanyakyusa wa kule.SEHEMU YA NANE (8)
Tulipoishia….
Tulipokelewa shuleni tukaonyeshwa mabweni then tukaenda kula mtaani siku hiyo maana tulifika watu washapewa chakula cha jioni shuleni pale.
Nilifanikiwa kupata marafiki wengi na maisha ya kuishi mbali na wazazi yakaanza rasmi
Tunaendelea sasa….
Maisha ya shule hayakua na changamoto sana, ile shule tulikua tunakula sembe suoer kabisaaa, maharage ya shule mnayajua vizuri, nyama ilikua ni jumapili mchana tu na Wali tulikula mara 2 kwa wiki.
Matunda kule Mbeya yapo ya kutosha ilikua ni pesa yako tu.
Nilianza tabia mpya ambazo sasa nyingine sijaacha hadi leo. Kwanza niwafahamishe tu pale shuleni nilikua mtu wa Kanisani sana mwanzoni. Kuna wakati hadi jina langu lilipendekezwa nigombee uongozi wa UKWATA.
Nilikua nikiimba kwaya pia. Tatizo lilianza baada ya kwaya mistress kuonyesha kunielewa (kunipenda) na mimi nilikua nampenda.
Niwarudishe nyuma kidogo….
Wakati nimemaliza form 4 kule Bukoba. Kuna wakati pale kwa aunt kulikua na maandalizi ya harusi ya mtoto wa aunt mkubwa (wa kike) . Sasa zikiwa zimebaki siku 3 hivi kuelekea sendoff, wageni kutoka kijijini na wengine mikoani walianza kuwasili pale home.
Kuna Baba mdogo (Mungu ampumzishe mahali pema peponi amen) alikua anatengeneza pombe ya kienyeji kule kijijini na alikuja na dumu la lita 20 kwenye hiyo sendOff. Hii pombe ni ile pure imetengenezwa na ndizi, ilikua nyeupe kama Kvant or Konyagi.
Sasa kuna bro flani nae ni ndugu upande wa kina uncle alikua rafiki yangu sana. Tulikubaliana na yule bro tuibe kiasi cha pombe tukafiche chumbani.
Nakumbuka tulichukua Kidumu cha lita 5 kile. Tukamimina kama nusu na zaidi (almost kijae) tukaficha chumbani.
Kila usiku tulikua tunapiga kale ka pombe asee, kumbuka tuna siku 3 mbele kuelekea sendoff.
Siku ya kwanza nilikunywa usiku na yule bro, nikalewa ila asubuhi niliamka poa na hakuna aliyejua. Siku ya pili hivyo hivyo. Sasa siku ya tatu ndo ilikua sendoff. Tulijiandaa hao tukaenda kwenye sendoff. Usiku tuliporudi tukasema tulewe then tulale.
Asee hii siku tulikunywa mimi nikazidisha kipimo maana sikua mzoefu wa pombe, sikumbuki kilichotokea baada ya hapo maana nilizima mle chumbani na bro usiku kucha alikua akihangaika na mimi. Kuna wakati alitamani kuita watu maana anasema hali yangu ilikua mbaya sana.
Nilitapika sana asee, nilishtuka saa 11 asubuhu ndo nikajigundua nimelewa sana. Nilikua nimekabiza Boxer tu, kitanda kizima kinanuka pombe. Bro alinipa maji yenye sukari na majani flani ya kienyeji (alidai inakata pombe lakini sikumaliza hata dak 5 nikazima tena. Bro anadai kuna muda uncle alikuja mlangoni pale chumbani kwetu na kuuliza kama tuko sawa na bro alimjibu tuko sawa.
Asubuhi niliamka nikiwa naumwa kichwa na hangover za kutosha. Sasa pale kwa aunt kuna nyumba 2, moja tulikua tunatumia kama jiko, sehemu ya kula na stoo alafu nyumba kubwa ni sitting room na vyumba vya kulala. Bro alikuja kunishtua kuwa naitwa tukanywe chai, wakati huo Aunt alushakuja room (anaishiaga mlangoni anatoa maelekezo na kuondoka) na kunambia nijiandae leo ntaenda mimi kwenye biashara zake, Yeye bado anaweka mambo sawa home kwani wageni walikuwa wengi.
Nilimjibu kwamba sijisikii vizuri, akahisi numegoma kwenda sababu ya wageni pale home (kampani ilikua kubwa) hakusema kitu ila niliona hakufurahishwa na nilichosema
Nilinyanyuka kwenda nyumba ndogo niungane ma wengine kwenye breakfast. Nimefika nikasalimia na kuketi, kulikua na supu ya samaki na vitafunwa vingine. Kitendo cha mimi kusikia harufu ya supu ile nikahisi kizunguzungu na kichefuchefu, nikanyanyuka ili niende nyumba kubwa nisije kuharibu pale. Sikufanikiwa kufika nyumba kubwa, nilianguka mara tu baada ya kufika mlangoni, nnachokumbuka baada ya hapo nilishtuka saa 12 jioni nikiwa hospital ya mkoa (wanaiita Government, watu wa Bukoba watanielewa hapa) nilikua wodini na aunt alikua pembeni yangu, sura yake ilionyesha kuwa na wasiwasi sana.
Aliniuliza naendeleaje nikamwambia kichwa kinauma sana. Basi alikuja doctor pale na kunicheck tena then akaoder nurse waniongezee drip kadhaa, aunt hakusema chochote kuhusu pombe na wala hakuwahi niuliza hadi hii leo. Kesho yake asubuhi nilishtuka baada ya kujishika pua na kugundua nilikua na uchafu wa damu iliyoganda puani.
Mazingira ya hospital sikuyapenda kabisa kwani ilikua mara yangu ya kwanza kuona mtu akiwa katika hatua za mwisho za kukata robo ( kile kitanda nilicholazwa, niliambiwa na mgonjwa mwingine kuwa juzi yake kuna mtu alikua kalala pale na alifariki).
Zile siku 3 nilizokaa pale hospital nilishuhudia watu 2 wakifa (nurses walikua wanaweka zile screen ili mtu asione ila tulikua tunasikia kabisaa mtu anahangaika na baada ya dak kadhaa anaondolewa pale kama maiti) Hii hali ilinitesa ila nashukuru siku ya 3 niliruhusiwa kurudi home na huko homr nilisimuliwa namna hali yangu ilikua mbaya. Nikajiapia moyoni kuwa sinywi tena pombe.
Sasa tuendelee na maisha ya shule kule Mbeya. Sasa yule kwaya misstress (tumwite Gift) alikua na tabia ya kuniita popote atakaponiona. Nikaanza tabia ya kwenda kusomea olevel usiku, ule muda wa Prep. Naomba kufafanua ile shule ilikua na O level na Advance…wanafunzi wa kike wa olevel walikua wengi wanakaa bweni..(kulikua na mabweni ya wadada kwa O-level)
Sasa uliwekwa utaratibu, madarasa ya advance yalikua nyuma huko na tulikua tunaruhusiwa kukutana na O-level wa bweni kwenye vipindi vya dini tu. Na vipindi vya dini ilikua ni kila siku jioni saa 1 hafi 1:30 then wote mnatawanyika kwenda Prep.
Yule Gift alikua na mwalimu ambaye ni uncle wake pale shuleni(mtoto wa mwalimu) Mimi na baadhi ya wenzangu tulikua kila usiku hatwendi kusoma kwenye madarasa ya advance… tukawa tunakomaa huko huko O level. Tulikua na agenda zetu, mostly mahusiano hahaha….
Nilikua napata wasaa wa kukaa na Gift na kupiga story kila usiku after kipindi cha dini.
Kuna wakati kulikua na shida ya maji, hivyo tulitakiwa kuwa tunafata maji sehemu moja inaitwa irrigation (kulikua na mradi wa kilimo cha umwagiliaji)
Mimi na Gift tuliona ule ndo wakati wa kupata faragha na tulipanga siku hiyo tukitoka kipindi cha dini, mimi nitangulie, yeye atakuja kule, tuzuge tunafuata maji, ila tulikua na jambo letu hopefully mmenielewa
Ile shule ilikua na uhuru flani hasa kwa Advance (tulikua tunatumia hadi simu bwenini na hakuna mwalimu angemind, weekend tulikua tunatembea na simu zetu bila shida kabisaa) Walimu waliruhusu hii kutokana na mazingira ya kule, simu ziliturahisishia hata kutumiwa miamala kutoka home. Kwa upande wa O-level wadada walikaziwa mambo ya simu (Narudia tena hii shule ilikua na O-level mixer ila wadada ndo walikua wanakaa bwenini then wakaka wanaenda kwao)
Mimi na Gift tulikutana irrigation huko, tukachill chimbo flani na story zikaendelea baadae tukashiriki tendo bhana. Wakati tukiendelea asee tulishtuka kuna scout wawili wanakuja upande wetu, ilikua usiku ila kulikua na mwanga wa mwezi.
Tulichomoka pale kila mtu na njia yake, bahati nzuri hawakujua kama ni sisi.
Mahudhurio yangu katika vipindi vya dini yakafa maana niliona sasa namchezea MUNGU, natenda dhambi humo humo kanisani sio vizuri. Nikaanza kubadilika taratibu, nikawa mtu wa madem madem (sorry kutumia lugha hii)
Nikawa mtu wa kutoroka shule usiku tunaenda disco vumbi kila jumatano kama sijasahau.
Nikawa siendi darasani asubuhi, wala siku naenda assemble…(mimi na wenzangu wengine) Tukawa tunasubiri muda wa uji saa nne, tunanunua na mihogo na maparachichi na ndizi mbivu. Zote tunachanganya kwenye kontena la uji then haooo tunaenda porini huko kusoma.
Tabia ya kwenda porini ikakua na tukaanza kucheza kamali kule. Tulikua tukicheza kamali ya karata na dau nakumbuka lilikua 100 au siku nyingine 200. Ilikua pesa nyingi kwa maisha ya shule kwani ukipigwa kama elfu 3 hivi basi wiki nzima utakunywa uji mkavu…
Nikawa na ukaribu wa mdada flani (tumwite Tina) alikua mwanafunzi wa O-level… Asee kumbe yule dada kuna mwalimu anamtaka…. Hapa nikawa nimeyatimba
TUTAENDELEA….
Kaangalie kwenye AtlasOoh safi sana. Linaitwaje ili nitafute muda nikalitembelee... Limeanzishwa lini?