Maisha Yana Maana Gani Hasa?

Maisha ni matamu iwapo una resources. Changamoto ni resources, haya mambo ya uchumi, nchi, pesa sijui ulinzi ni uhaba wa resources otherwise maisha ni matamu mno.
Kuna watu wana hzo resources zote unazozijua ila cha ajabu chakula chake anachotakiwa kula kina maelekezo ya daktari na hata kule kitandani hana uwezo wa kumshughlikia mke wake ipasavyo japo anamtamani na ana kila kitu...amezongwa na stress muda wote na wengi katika hawa ni watu wa kujificha mida mwingi,hata akiwa street gari yake lazima iwe full tinted,hana amani hana furaha,uani kwake kapaki gari za kifahari za kutosha na ana investments za maana....shida zake wewe huwez kuzibeba hta kwa dk 10...
Mungu hawezi kusema uongo upuuzi wa hii Dunia..
kikubwa tumuabudu yeye tu yapo maisha ya ukweli na uhakika yenye utamu usiokatishwa,amewaandalia maisha hayo watendao mema kwa ajili yake.
 
Mkuu maisha ni matamu, ukishaweka utajiri tayari ni tatizo sababu utajiri ni uwezo wa kutunza resources. But imagine, ondoa concept ya utajiri na umasikini, kuwepo tu na resources. Ukitaka chakula simple effort unakipata, ukitaka matibabu simple effort unayapata, ukitaka safari simple effort unaipata, una ndugu, jamaa na marafiki wa kuzeeka nao pamoja. Hapo ubaya wa maisha upo wapi? Ni utamu tu mpaka siku unaondoka ndo utawaachia wengine huzuni unless uwe na tatizo la saikolojia.
 
Kaka nimekwambia kuna wana hzo resources zote unazozijua,ila ndani ya maisha yake kuna changamoto moja au mbili ime/zimemganda na hzo changamoto anajikuta hana raha ya haya maisha.
Wapo watu yeye kila kitu anapress tu kinafanyika/kinakuja ila ndani mke wake anaempenda ni changamoto mnoo na kumuacha hawezi,ana watoto ila kuna tetesi anaziskia nje kwa watu kwamb watoto wako wanafanya mpango wakuue warithi kitu flani,au mtu ana kila kitu ila ana kisukari na presha,chuma hakisimami,mwingine halali usingizi mpaka ameze dawa....hizo raha umazosema unazipata wapi hapo?
Hakuna utamu wa moja kwa moja Duniani,utamu pekee upo kule alipoandaa Mungu mahali ambapo Mungu ameumba maalum kwa ajili ya utamu,huwezi kupata utamu mahali ambapo Muumbaji kapatengeneza kama chumba cha majaribu kwa watu.
 
Reactions: Tsh
Nikiwa mdogo niliwahi kujiuliza swali kama hilo. Miaka kadhaa baadae nilipompokea Yesu ndipo nilipoanza Safari ya kupata majibu toshelevu!. No more worries now. Just stress-free life!

YOHANA 14
1 Msifadhaike mioyoni mwenu; mnamwamini Mungu, niaminini na mimi.

2 Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambia; maana naenda kuwaandalia mahali.

3 Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi mwepo.
 
Kaka nimekwambia kuna wana hzo resources zote unazozijua,ila ndani ya maisha yake kuna changamoto moja au mbili ime/zimemganda na hzo changamoto anajikuta hana raha ya haya maisha.
Mkuu, nini maana ya kuwa na resources kama bado una changamoto zilizokuganda? Nikisema resources simaanishi financial resources, namaanisha Empowering the capacity to meet every need that ensures your happiness.
 
Mkuu, nini maana ya kuwa na resources kama bado una changamoto zilizokuganda? Nikisema resources simaanishi financial resources, namaanisha Empowering the capacity to meet every need that ensures your happiness.
Hapa Duniani hakuna mtu yeyote aliyezaliwa na mwanamke anayepata hiyo happimess kwa masaa yote,masiku yote.Happiness anayoipata mtu yeyote aliyejitosheleza ni ya VIPINDI VIPINDI SI ILE YA MOJA KWA MOJA,happiness za binadamu zimejaa interruption nyingi sababu kubwa ikiwa ni kwamba hii Dunia haijaumbwa spacific kwa ajili ya raha....hii Dunia shida na karaha ni pipa starehe ni kisoda.
"Haikuwa hii Dunia ila ni starehe na udanganyifu mtupu"
Aliye design na kuunda hii Dunia ndo anakwambia hivyo unao uwezo wa kumpinga?
HEbu pita pita uliza hao unaodhani wana resources zote watakwambia how they feel hiyo hapoiness kama wanaipata muda wote,masaa yote.
Hata wale watalii wa kizungu tunaowaona usidhani wapo kuinjoy maisha,kuna wengine yupo katika utalii ila kamkimbia mke ulaya kwa sababu ana vituko vingi vinamchosha,wapo wengine wanaambiwa na madaktari/wana saikojia wao kwamba kwa tatizo lako hili hebu toka safiri kdg nenda huko katembee nje ya nchi ukaishangae Dunia kdg ukirudi tatizo lako litakuwa limepungua...wakija hapa ww unawaona wana enjoy sana kumbe wamebeba mizigo mingi kwenye mioyo yao huku utalii ukiwasaidia kurefresh mind japo nayo ni kwa kipindi tu.
Mtoa mada yupo sahihi sana kutafakari na akagundua hapa Duniani ni kama tambara bovu ni kama hapaeleweki hivi,na kiukweli Hili eneo tulipo halina UHAKIKA WA 100% WA HIYO HAPPINESS tusijidanganye,unapataje hapiness ya moja kwa moja huku kukiwa na tishio lenye uhakika la KIFO?...HAPINESS iko vifundo vifundo sana,inakatika katika no consistance,happiness ya uongo...Hapiness ya Uhakika ni ile aliyotuambia Mungu ipo kule baada ya kufa, starehe za Uhakika, Mitume wanatuambia "Hakuna jicho limewahi kuona na hakuna akili imewahi kuwaza" na hazikatiki,ni daima milele.
 
Hapa duniani hakuna unlimited resources.
 
Hapa duniani hakuna unlimited resources.
Sawa,ila ukumbuke pia hakuna mtu/binadamu anaeweza kuwa na hzo resources zote 100%,...Hii Dunia iko designed kwa changamoto kaka,siyo starehe,ndiyo unaona kuna watu wanajaribu kwenda kwenye space kutafuta possibility ya kutengeneza maisha mengine kule japo nina uhakika hata huko changamoto zitakuwepo na huenda zikawa kubwa zaidi ya hizi.
Usibishane na Engeneer wa hili jengo kaka,Founder na Engeneer wa hili jengo (Mungu Muumbaji) anakwambia "Hii Dunia ni pumbao na upuuzi mtupu"...Hakuna binadamu anaweza badili haya maneno.
Tumuabudu yeye ili akatuzawadie maisha ya uhakika baada ya kufa...unafikaje huko? hapa sasa ndo unakutana na kitu kinaitwa IMANI.
Imani ya aina gani itakayokuingiza huko? Hili sasa ni somo jingine.
 
Reactions: Tsh
Ok mkuu
 
Pole,life is living and living is pain,kuishi kwetu ni mpango wa Mungu,na kifo hakikuwa mpango wake ila mawenge ya Eva ndio yametufikisha hapa,ambapo Mungu alibadili gia na kusema hakika tutakufa.Kwahiyo endelea kuishi tu ila hakikisha kuwa unakuwa na mwisho mwema,hilo swala la kutafuta pesa na mali ni hiari tu....
 
Alitetuumba anasema kupitia Quran tukufu
(87:16:17)
"Bal tu'thiruunal-hayaatad-dunyaa.Wal-aakhiratu khayrun wa abqaa."

Maana:
“Bali nyinyi mnapendelea maisha ya dunia, hali ya kuwa Akhera ni bora na inadumu zaidi.”
Akhera unaijua wewe? Au unafatilia tu maandiko
 
Ni vitu vya kujitungia tu na watu wanaamini kama ukweli, ambao usipo fanya hivyo inakwenda motoni
 
Kwamba maisha ya duniani ni upuuzi?
. Je ukifa si ndio unafutika kabisa na historia yako unapotea mazima?

Mimi naona hakuna maana halisi ya maisha na ukifa ndo imeisha hiyo, maana maana ya yote uliyo ya fanya inafika ukomo
 
Maisha ni matamu iwapo una resources. Changamoto ni resources, haya mambo ya uchumi, nchi, pesa sijui ulinzi ni uhaba wa resources otherwise maisha ni matamu mno.
Una point usikilizwe.. Kama unaamka na kupata kila kitu, bila magonjwa..,bila kuwaza kuhusu kesho yako..

Hakika sisi wenyewe labda ndo tunaya complicate maisha!
 
Reactions: Tsh
Ndio.maana nimeridhika na maisha yangu ya chini nichukulie serious kitu ambacho kina tamati
 
Hakika mkuu, as simple as that..

Maisha ambayo unajua hauna stress ule wapi, uishi wapi, ufanye nini ili u survive anakuwa bora na unaweza kutafuta maana ukiwa na comfort..

Ila maana haipo, ni kuzaliwa kuishi na kufa tu
 
Reactions: Tsh
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…