Hahaaaa kuna hiii nimesahau, ni wachache sana geto wanaandaa maji ya kunawa, weng wetu tunanawa kwenye sufuria ya ugali, mimi nilikua naenda mbali zaid njaa ikikaza, maswala ya kuchota maji sijui kwenye bakuli huku nina ubao, utashangaa tu paap mikono imetua kwenye ndoo yoyote ya maji iliyowazi na karbu hata kama imejaa, baadae nikishashba ndo najiuliza hv nimefanya nini? Kaz nilizokua nazichukia zaid,
1. Kuosha vyombo
2. Kuchomoa net, kaz niliyokua naifanya bila hata kupanga nashangaa tu nimeifanya ni kuosha mwiko, hii ni kutokana na malez, kwa bimkubwa ilikua sahau vyote ila si mwiko wa ugali baada tu ya kuepua. Yoote hilo tu ndo naweza kujisifu 100%