Maisha ya ndoa ni magumu

Maisha ya ndoa ni magumu

nyuzi kama hizi mabachela wakizisikia unafikiri inakuwaje
 
Habari yenu,

Nipo kwenye ndoa miaka mitatu. Sijawahi kuona furaha ya ndoa hata watoto sina.

Nina mpango wa kudai talaka.

Naombeni Ushauri.

Au nimtoroke?

Kabla ya kukupa ushauri wowote naomba nikuulize maswali yafuatayo:
1. Ulikuwa na mategemeo gani juu ya hiyo ndoa kabla ya kufunga?
2. Ni kitu gani kinachokufanya usione furaha katika ndoa?
3. Kwa nini unataka kudai talaka?
 
Ujue Firstlady1 mwenzako amedata na hayo matatizo sasa mm nimecheka jinsi wewe unavyomwambia just aondoke easily bila hata kutaka kumdadisi matatizo yake ni nn na vitu kama hivyo...

hahaha yaani watu tunachanganyikiwa na mengi
 
Habari yenu,

Nipo kwenye ndoa miaka mitatu. Sijawahi kuona furaha ya ndoa hata watoto sina.

Nina mpango wa kudai talaka.

Naombeni Ushauri.

Au nimtoroke?
Uwiiii jamani ndoa sio lelemama kama ulicho tegemea sicho jaribu kukaa chini uone ni wapi ulikosea, pole sana
 
Kwanzaa unaonekana unatabia za kibabe ugomvi ugomvi lazima yakushinde unataka ushindane na mwanaume

Ndo maana unajiita pantheraleo Latin name means simba kwa kiswahili sasa mwanamke unajiita simba we hufai
Kwani simba ni madume tu hakuna majike?
 
Labda pia na kukosa mtoto kwa huo muda kwa familia za kiafrika zilivyo kelele zimezidi, mwanaume ndani halali tena dah kama ni mwanamke pole sana
Upo sawa kabisa, wakati wengine miaka zaidi ya 15 lakini kama wameoana jana, maneno ya ndugu tupa huko
 
Pole sana, unajua wenye kuijua dini wanasema unapotafuta mchumba hata kama ni mlokole angalia mchakarikaji sio mshinda kanisani tu bila kufanya kazi nyingine bora uolewe na mpagani utamsaidia wewe mwenyewe na atakuelewa lakini mvivu wafwa, endelea kumwambia na kumuombea Mungu hana upendeleo iko siku atakusikia
Pole sana hizo changamoto wanakutana na tunakutana nazo sana kiukweli hata mimi nina mwaka toka nimeolewa lakin siifurahii ndoa yangu hata kidogo nilikuwa ni mtu wakujitafutia kipato changu na nilikuwa mwenye bidii sana na kile nilichokipata nilijitahidi kukitumia vizuri ikiwa ni pamoja na kuwasomesha wadogo zangu na kuwajengea wazazi wangu nyumba.Lakini toka nimeingia kwenye ndoa hayo mambo yamekuwa ni ndoto mume wangu yaan furaha yake ni kuona nafanya kazi isiyoeleweka ambayo mda wowote tunaweza kuachishwa kazi.Nilipata kazi mgodini akanigomea akidai kuwa watu wa mgodini ni wahuni na wengi ni wachawi hivyo huko hakunifai nikapata kazi sehem moja hivi ni shirika kubwa tu sema lilikuwa liko mbali na nyumbani ila walikuwa wana utaratibu wa kuwa wiki mbili nyumbani wiki mbili kazini nakwenyewe akagoma.yeye ni mchungaji tena mwenye imani kali ya kuamini kuwa anaweza kupata utajiri pasipokufanya kazi anapenda kulala hakuna mfano yaan mda wa kuamka ni saa tatu asubuhi akinywa chai basi anapitiwa na usingiz akizinduka anakuambia alikuwa anazungumza na Yesu hapendi kuumiza kichwa juu ya kitu chochote kinachohusu future umri wake ni miaka 35 ukimshauri anakuwa mbishi tena anaona unamtoa rohoni mkipishana kauli hakuna kukaa ndani kujadiliana anayapeleka nje utashangaa tu mnakuja kukalishwa kikao ataongea uongo humohumo ukweli humohumo kiukweli hayo ni baadhi tu ya mambo ambayo yananifanya nisiifurahie ndoa yangu hata kidogo na hapo bado hatujapata mtoto
 
Ifike mahali watu wa ustawi wa jamii waanze kutoa elimu kwa uma juu ya mahusiano ya ndoa, maana inapokuja kuachana licha ya dini za kila mmoja kabla ya kufika kuchukua talaka mahakamani lazima muanzie ofisi za ustawi wa jamii.

Tangu watoto waelimishwa kwanini uingie kwenye ndoa na ukiingia ujue hiki na hiki na hiki ukitarajie na hiki na hiki unaweza usikipate na hakuna kufanana na kadhalika na kadhalika. Yaani iwe suala la kujiandaa kisaikolojia zaidi ili wanaokataa ndoa waikatae tangu wadogo.

Sio waingie kichwa kichwa halafu baada ya miezi, mwaka au miaka kadhaa wanasema ndoa haina maana.Siwalaumu maana sijui wanayokutana nayo huko, sina uzoefu ila ni swali la kujiuliza, kwanini uingie kwenye ndoa? na uingie na nani?....

Walioko kwenye ndoa pia wana jukumu kubwa kuwaelimisha uzao wao kuhusu masuala haya haswa kipindi hiki cha utandawazi.

Watu wanaingia kutoa nuksi tu. Huwa nacheka sana.

Na kwa huu upepo wa kisulisuli kuoa bila kuwa na dalili tutashuhudia sana kuyumba kwa hii taasisi.
 
Back
Top Bottom