Maisha ya ndoa ni magumu

Maisha ya ndoa ni magumu

Habari yenu,

Nipo kwenye ndoa miaka mitatu. Sijawahi kuona furaha ya ndoa hata watoto sina.

Nina mpango wa kudai talaka.

Naombeni Ushauri.

Au nimtoroke?
Jombaa,kaza buti akimwacha huyo itakuwa ni sawa na kuruka mkojo ukakanyaga mavi.Jifanyieni matengenezo wenyewe.
 
Fanya utakachokiona sahihi kwako ili baadae usije juta.
 
Nina miaka 25 tu kaishanifanya kama bibi kwa jinsi nilivyochoka na wala hilo haoni ukimwambia aisee kwa mwendo huu hatufiki yaan sina mtoto niko hivi tukipata watoto je itakuwaje nyumba yenyewe ya kupanga kodi yenyewe hamna na mpaka hivi ninavyoongea mwenye nyumba kaishamtafuta alichobakiza ni kuanzakutafutatafuta mapungufu ya nyumba tunayokaa na angali alishasema tokea mwanzo kuwa hayo tutayarekebisha wenyewe haina shida sasa kajikuta hamna kodi anatoa visingizio
Sorry dada ushaachana na mumeo?
 
Pole sana, unajua wenye kuijua dini wanasema unapotafuta mchumba hata kama ni mlokole angalia mchakarikaji sio mshinda kanisani tu bila kufanya kazi nyingine bora uolewe na mpagani utamsaidia wewe mwenyewe na atakuelewa lakini mvivu wafwa, endelea kumwambia na kumuombea Mungu hana upendeleo iko siku atakusikia
Yaan ananishangaza sana kipind tukiwa wachumba alikuwa mbunifu sana wa vitu ambavyo anavijua yeye tu mwingine hawez kuiga mpaka amuulize lakin toka tumeingia kwenye ndoa hataki kuumiza kichwa kabisa anachoweza kulala,kuchat na video basi
 
Taasis ya ndoa Ni rahis Sana na Ni ngumu Sana na weng tunaingia kufuata mkubwa katika ndoa Kuna meng Sana mengne sent from heaven
 
Ifike mahali watu wa ustawi wa jamii waanze kutoa elimu kwa uma juu ya mahusiano ya ndoa, maana inapokuja kuachana licha ya dini za kila mmoja kabla ya kufika kuchukua talaka mahakamani lazima muanzie ofisi za ustawi wa jamii.

Tangu watoto waelimishwa kwanini uingie kwenye ndoa na ukiingia ujue hiki na hiki na hiki ukitarajie na hiki na hiki unaweza usikipate na hakuna kufanana na kadhalika na kadhalika. Yaani iwe suala la kujiandaa kisaikolojia zaidi ili wanaokataa ndoa waikatae tangu wadogo.

Sio waingie kichwa kichwa halafu baada ya miezi, mwaka au miaka kadhaa wanasema ndoa haina maana.Siwalaumu maana sijui wanayokutana nayo huko, sina uzoefu ila ni swali la kujiuliza, kwanini uingie kwenye ndoa? na uingie na nani?....

Walioko kwenye ndoa pia wana jukumu kubwa kuwaelimisha uzao wao kuhusu masuala haya haswa kipindi hiki cha utandawazi.
Mkuu masuala ya migogoro ya ndoa ni mapana sana hata kama umeelimishwa vipi kuyahusu ukishaingia ile elimu inaweza isisaidie kitu chochote.

Hivyo pamoja na elimu ndoa inaweza ikashindikana mapema. Hao ustawi wa jamii unaosema waelimishe watu unakuta wengine wao ndoa ziliwashinda mapema kabisa pamoja na kuwa na ma-degree ya elimu jamii ikiwemo ndoa na mahusiano.

Kuishi na mtu ni kazi inayotegemea zaidi moyo wa mtu kuliko elimu yake.
 
Ndoa ni gereza na nisehemu pekee maadui wanalala gereza moja(kitanda) so tafuta adui unae weza kuhendo..ili uishi gerezani kwa unafuu..ila zaidi ya familia mi sionagi mana ya ndoa kabisa.
Hitimisho lako lina bainisha kuwa una matatizo makaubwa kwenye mitazamoyako kuhusu watu wengine linaweza kuwa limesababishwa na makuzi ,malezi yako,au ulitendwa au ...mengine yanayofanana na hayo ! Bado uana muda wa kuyatibu hayo ili usiishe kweney utumwa huu maisha yako yote!
Ni PM nikupe mwanaga wa kujitibu kama ukitaka!
 
Furaha haiji bila kuwa na amani, sasa muulize kuna amani?
Je uliweka matarajio makubwa au kudanganyana kabla ya ndoa....?
Kukimbia sio dawa....
Habari yenu,

Nipo kwenye ndoa miaka mitatu. Sijawahi kuona furaha ya ndoa hata watoto sina.

Nina mpango wa kudai talaka.

Naombeni Ushauri.

Au nimtoroke?
 
Back
Top Bottom