mtani wewe wengi tunajua kuolewa ni kugegedana na kulala
Kwa mwanamume mkamilifu na mtimilifu....hakuna jambo la aibu na la fedheha kama kuomba........
Kuomba ni jambo linalomfedhehesha sana mwanamume kiasi kwamba linamuathiri sana kisaikolojia.......
Na mwanamume yeyote ili kuepukana na kadhia hiyo ya fedheha....hana budi kupambana na kuhangaika kwa namna yoyote ili kukidhi mahitaji yake na ya wale wategemezi wake......ndio maana mwanamume hufikia hatua mpaka ana hatarisha maisha yake yote ni katika harakati za kukidhi mahitaji yake......
Katika taswira ya kawaida kumuona mwanamume amekaa na huku anaomba msaada kwa watu wanaovuja jasho kama yeye si jambo la kawaida.....ni jambo litakalompelekea mwanamke mwenye akili timamu akajiuliza kuwa nimeolewa na mwanamume wa aina gani...!!??
Kuomba msaada ni jambo la kawaida kwenye maisha kwani kati yetu hakuna aliyejikamilisha....unaweza ukawa na hiki na ukapungukiwa hiki....lakini kuna mazingira yake ya kuomba msaada na staha zake.....
Kwa mfano huyo kijana kama angeanzisha kajimradi ambako kangekuwa kanaendesha familia yake....ambako pengine baba mkwe angeona juhudi zake na kumuongezea mtaji na kukuza mradi wao....sidhani kama wangekataa ukizingatia unaishi na mtoto wao...na juhudi zinaonekana wazi ni katika kuhakikisha mtoto wao anaishi maisha mazuri.....
Kimsingi hakuna mtu mwenye uvumilivu wa kutoa misaada endelevu isiyo na mwisho.....na hilo ndilo lililotokea kwa huyo kijana.....ameukumbatia umaskini kana kwamba ni sifa nzuri.....anashindwa hata kutoka kutafuta vibarua kwenye masite ya ujenzi.....anashinda nyumbani huku akitumainia familia ya mwanamke itaweka mambo sawa.......
Hili ni tatizo kubwa kwa vijana wa sasa hivi ambapo uvivu na kutojituma ni sehemu ya miasha yao.....wanapenda mambo ya kiwepesi wepesi....mafanikio ya ghafla......hapo pengine aliunganisha dot kuwa nikimuoa huyu binti kwakuwa familia yao inajiweza....basi na mimi nitakula humo humo.......
Mwanamme ukishaingia katika majukumu unatakiwa uwe mpambanaji na sio goi goi....hayo ni majukumu yako....usiposhughulika na majukumu yako hakuna wa kushughulika nayo......usiwatupie watu majukumu yako.....
Jukumu la kumtunza mkeo ni lako haijalishi hali ya maisha ya familia ya mkeo.......