Maisha ya ndoa ni magumu sana

Maisha ya ndoa ni magumu sana

Pole sana huo ndo msalaba wako ubebe tu, huyo kijana ukute hata hakupendi ila alifata mteremko kusikiliza ushauri wa wakubwa huwa muhimu sana kwa kweli. Jikaze tu
 
Pole sana haya maisha yana changamoto sana kuna maswala huwa hayakwepeki mumeo anaweza kuwa na pesa na zikaisha au akawa hana akaja kupata upepo hubadilika!
Cha msingi kuliko mumeo au wewe kuendelea kuomba msaada kwenu haipendezi watawachoka na watawatangaza.kikubwa bora muombe msaada hata wa kitega uchumi au mumeo wamtaftie kazi afanye kuliko kujiombeleza kila mara heshima inapungua.
 
usivunjike moyo hayo ni mapito tu ipo siku mtakuwa vizuri kiuchumi na mambo yatakuwa poa
 
ni ufala kuolewa na mume maskini halafu mkipata shida anakuambia kaombe msaada kwenu
kwani yeye hawezi kusolve mambo ya nyumbani kwake? ndugu zako wapo sawa shida zako na mumeo zinawahusu nini?
ajipange hawezi akurudishe kwenu
Maisha yenyewe yalivo magumu kujipeleka kwa maskini kujitàftia maradhi bure aisee.
 
Maisha yenyewe yalivo magumu kujipeleka kwa maskini kujitàftia maradhi bure aisee.
halafu eti anataka msaada kwenu?
hana marafiki? hana wazazi? hana kazi?
kujipa tu pressure maisha yenyewe haya mwanaume hathaminiki .
 
Kweli kabisa.
ni ufala kuolewa na mume maskini halafu mkipata shida anakuambia kaombe msaada kwenu
kwani yeye hawezi kusolve mambo ya nyumbani kwake? ndugu zako wapo sawa shida zako na mumeo zinawahusu nini?
ajipange hawezi akurudishe kwenu
Mwanaume hatakiwi kumendea msaada toka kwa wakwe hata siku moja.
 
Pole sana dada yangu. Haya ni mapito tu yatapita. Kuna watu watakudharau lkn ipo siku moja watakusalimia kwa heshima.
Mm nilioana na wifi yako tukiwa tunalala kweny godoro tu lkn leo na nyumba yangu. Safi mambo yanaenda. Kikubwa ni uzima na upendo(mapenzi ya dhati kati yako na mume wako)
kuna wengine humu wanatamani waolewe na mgane, au awe mke wa pili, na wengine wanatafuta sperm donor lkn leo hawa humu wanajitapa na kujinadi kuwa kuolewa na mume maskini ni ufala kwann wao wasiowaumbe hao wanaume wanaowapenda mpaka anataka kuwa mke wa pili?
Ktk maisha kuna majaribu mengi sana na ukumbuke siku zote kuna watu wema na wabaya. Kuna watu humu wananuka midomo kila atakachopost ni kinye.si kitupu.
Naomba usikate tamaa huyo ni mume wako. Haya yote yatakwisha in the name of GOD
AMEN
 
halafu eti anataka msaada kwenu?
hana marafiki? hana wazazi? hana kazi?
kujipa tu pressure maisha yenyewe haya mwanaume hathaminiki .
Ushauri wa kubwa huwa muhimu tu kwa sababu wameona mengi, sasa imagine hyo hali anayopitia dunia ya sasa ukijifanya wapenda kapuku walahi utajutraa na stress.
 
Pole sana dada yangu. Haya ni mapito tu yatapita. Kuna watu watakudharau lkn ipo siku moja watakusalimia kwa heshima.
Mm nilioana na wifi yako tukiwa tunalala kweny godoro tu lkn leo na nyumba yangu. Safi mambo yanaenda. Kikubwa ni uzima na upendo(mapenzi ya dhati kati yako na mume wako)
kuna wengine humu wanatamani waolewe na mgane, au awe mke wa pili, na wengine wanatafuta sperm donor lkn leo hawa humu wanajitapa na kujinadi kuwa kuolewa na mume maskini ni ufala kwann wao wasiowaumbe hao wanaume wanaowapenda mpaka anataka kuwa mke wa pili?
Ktk maisha kuna majaribu mengi sana na ukumbuke siku zote kuna watu wema na wabaya. Kuna watu humu wananuka midomo kila atakachopost ni kinye.si kitupu.
Naomba usikate tamaa huyo ni mume wako. Haya yote yatakwisha in the name of GOD
AMEN
Nashukuru kaka huyu mume wangu sijaona kasoro yoyote kwake ni mstaarabu msomi sema maisha yetu bado ni ya chini sanaaa na ndugu hawakubali maisha ninayoishi sasa sijui wanataka nifanyeje
 
wakati mwingine ni vigumu sana kushauri kuhusu ndoa na mahusiano.
 
ni ufala kuolewa na mume maskini halafu mkipata shida anakuambia kaombe msaada kwenu
kwani yeye hawezi kusolve mambo ya nyumbani kwake? ndugu zako wapo sawa shida zako na mumeo zinawahusu nini?
ajipange hawezi akurudishe kwenu
weee bibie wewe hivi kuolewa na mtu asie na kipato ni ufala kweli?? Punguza ukali wa maneno aisee mbona mnakatisha wenzenu tamaa namna hiyo na sisi makabwela tutaoa kweli kwa mienendo kama hiyo yako? Kweli kabisa nàkutana na wewe alafu ndio unaleta dharau kama hizo si nitaishia kupiga mechi za mchangani na kusepa kwingine...mwisho wa siku unabaki kulalama umenipotezea muda kuoa umeoa kwingine ..
 
Nashukuru kaka huyu mume wangu sijaona kasoro yoyote kwake ni mstaarabu msomi sema maisha yetu bado ni ya chini sanaaa na ndugu hawakubali maisha ninayoishi sasa sijui wanataka nifanyeje
Maisha hayana formula, Leo unaweza ukawa na kila kitu kesho ukaamka huna hata moja, ni phase tu ya maisha mnapitia, and kila mtu ana chaguo lake as long as ndo kinachompa furaha na amani. Hukufanya kosa kumchagua mumeo Kwa sababu hana uwezo maybe, but simply because you find so much joy and happiness in him. Sio wote wanaolewa na watu wenye uwezo tayari, wengine wanaanzia chini mno, na Mungu Sio mwanadamu, wengine wanafanikiwa mnooo huko mbeleni. Kuna watu walianza na kila kitu, Leo hawana chochote. Na Kuna wengine pamoja na mahela yote, wamezikimbia ndoa zao kama ambavyo wengine wanakimbia ndoa zao Kwa sababu ya pesa hakuna. As long as hayo ndo maisha yako, please usisikilize "judgement za watu", kila mtu na maisha yake, kila mtu afanye kinachompa amani.

Msupport mumeo, he needs you mnooo Kwa wakati huu. But please and please, pamoja na shida zenu zote, msiwape ndugu sababu ya kuwadharau zaidi. kuweni tu maskini jeuri, vumilieni tu na shida zenu, coz hata mkifanyaje hao ndugu hawatowasaidia chochote. Jitahidini tu kutafuta Kwa bidii + kumwomba Mungu, ipo siku yenu, Mungu atawafungulia milango yenu pia.

Usiache maneno ya watu yakakukatisha tamaa. Usidhani kila anayekucheka ana maisha mazuri kwenye ndoa, karibu kila mtu ana changamoto yake, pesa za muhimu sana but sio the only changamoto kwenye ndoa. Wengine wana changamoto za uaminifu, wengine vipigo, wengine watoto, wengine ulevi, wengine mume asiyejali familia,wengine hakuna maelewano kabisa, wengine wapo tu for the sake of their kids, wengine afya etc. Kama ambavyo wao wanavumilia changamoto zao, na wewe ya kwako ivumilie tu, usiwasikilize kabisa. Shikamana na mumeo, na msikate tamaa, Mungu yupo
 
Ndo mana pande hizi za huku kwetu wanachomaga nyumba au kutanguliza waume zao ,nawaza kwa sauti tuu wakuu japo siungi mkono hoja,
Ingekuwa sio vibaya akifikia steji hiyo unamrostia tu kuku mixer na rat and rat....
 
Unakuta binti unatoka familia ambayo ni bora kidogo unakutana na kijana ambaye kiuchumi yupo chini mnaoana lakini maneno yanakuwa Mengi ndugu hawamuheshimu mume wako wanamdharau wanaona kama ulikosea kuchagua.

Binti unadharaulika kwenye familia yenu kila unachoongea hakina maana, ndugu wanakutenga yaani ni mateso tupu hata ukiwapigia simu wakusaidie wanakuambia mwambie mumeo na wanajua kabisa mume hana kwa muda huo.

Haya ni mapito tu naamini yana mwisho
Waache na dharau zao maisha hayana formula! Ipo siku moja nanyi mtabarikiwa
-heading umekosea kidogo! Hapa cha kulaumiwa sio ndoa
 
Back
Top Bottom