Maisha ya ndoa ni magumu sana

Maisha ya ndoa ni magumu sana

happy123

Member
Joined
Dec 11, 2015
Posts
28
Reaction score
43
Unakuta binti unatoka familia ambayo ni bora kidogo unakutana na kijana ambaye kiuchumi yupo chini mnaoana lakini maneno yanakuwa Mengi ndugu hawamuheshimu mume wako wanamdharau wanaona kama ulikosea kuchagua.

Binti unadharaulika kwenye familia yenu kila unachoongea hakina maana, ndugu wanakutenga yaani ni mateso tupu hata ukiwapigia simu wakusaidie wanakuambia mwambie mumeo na wanajua kabisa mume hana kwa muda huo.

Haya ni mapito tu naamini yana mwisho
 
Unakua bega kwa bega na mmeo, mnasaidiana kutafuta, akizipata anakuona tena wewe falah, anazitumia kama hana akili nzuri anakudharau, vitimbi visivoisha.....
Hapo roho itaning'inia duniani haipo ahera haipo
 
Na hapo ndugu wanarudi kwa kasi
mume anawasikiliza ndugu hao hao waliomdharau kupita mkewe
na ndugu sasa wanasema mke ndo mkorofi....

inaitwa fungu la kukosa....inatokea kwa wengi tu
 
nikuusie kitu kimoja tu. KATIKA HAYO UNAYO PITIA SHETANI NAE HUPENYEZA MAMBO YAKE USIJE SHANGAA LIKAJITOKEZA JITU LENYE MIPESA YAKE NA KUANZA KUKURUBUNI.

ila kwa kuwa umetambua ni mapito please usimsaliti mumeo kwa kisingizio cha kutafuta unafuu kwa kutoka na watu wa aina hiyo.....
 
kuolewa na mume maskini halafu mkipata shida anakuambia kaombe msaada kwenu......kwani yeye hawezi kusolve mambo ya nyumbani kwake? ndugu zako wapo sawa shida zako na mumeo zinawahusu nini?
ajipange hawezi akurudishe kwenu
 
Unakua bega kwa bega na mmeo, mnasaidiana kutafuta, akizipata anakuona tena wewe falah, anazitumia kama hana akili nzuri anakudharau, vitimbi visivoisha.....
Hapo roho itaning'inia duniani haipo ahera haipo
Ndo mana pande hizi za huku kwetu wanachomaga nyumba au kutanguliza waume zao ,nawaza kwa sauti tuu wakuu japo siungi mkono hoja,
 
Usiwaze sis, haya ni maisha tu,we na mumeo zitafteni kwa nguvu tu mtapata na heshima itakuwepo,ndugu wa ukweli ni wanao uliozaa mwenyewe hao wengine ni midabwa midabwa tu,ondoa mawazo ya kusaidiwa utafanikiwa zaidi
 
Back
Top Bottom