Kipilipili
JF-Expert Member
- May 25, 2010
- 2,272
- 1,898
simama mbele ya kioo kisha uambie moyo wako kwa kutamka maneno haya "HILI NI GUMU ,LAKINI NALO LITAPITA,NITAPAMBANA, NINAWEZA KUIBADILISHA HALI HII" .Kisha kaa na mumeo chini muangalie humo ndani mwenu mna kitu gani ambacho hamkitumii au ni redundant , mkishavipata basi hivyo mnaweza kuvigeuza mtaji. na kwa mtaji huo huo mdogo pambaneni kuukuza na kusonga mbele. SAHAU kuhusu neno KUSAIDIWA , pambaneni nyinyi wawili na zidisheni upendo kati yenu.Unakuta binti unatoka familia ambayo ni bora kidogo unakutana na kijana ambaye kiuchumi yupo chini mnaoana lakini maneno yanakuwa Mengi ndugu hawamuheshimu mume wako wanamdharau wanaona kama ulikosea kuchagua.
Binti unadharaulika kwenye familia yenu kila unachoongea hakina maana, ndugu wanakutenga yaani ni mateso tupu hata ukiwapigia simu wakusaidie wanakuambia mwambie mumeo na wanajua kabisa mume hana kwa muda huo.
Haya ni mapito tu naamini yana mwisho