Maisha ya Babu Tale, Fella, hayati Kanumba yana financial freedom kuliko wasomi wengi. Tunakosea wapi?

Wasomi wengi wa bongo elimu inawapumbaza, wanasoma lakini bado wanakua hawajaijua nguvu ya pesa, anaweza akawa amesona sana lakini anakua mtumwa wa hela

Hutakiwi kua mtumwa wa pesa, pesa ndio inatakiwa uitumikishe ikuletee pesa zaidi

Wasomi wengi maisha yao ni yaleyale, mshahara ukiingia wanapay bills basi maisha yanaendlea lakin wanakua hawana maendelo yanaoonekana
 
"Talent is scarce so it must be compensated heavily"

Nilikuwa na mawazo kama yako wakati nipo University, ila baada ya kujisomea vitabu nikakutana na huo msemo ndo hapo nilipobadilisha mtizamo wangu na nikauona ni wa kijinga. Haya mambo unayoyaongelea sijui kina Diamond, Kanumba et al, kaa ukijua walikuwa vijana kama hao maelfu lakini waliofanikiwa ni hao wawili tu mpaka ukaja kuwatolea mfano. Na vitu vingine hivi vinatokea kwa bahati sio kila mwenye talent lazima atafanikiwa pia.

Halafu muachege hayo mawazo ya kuwapa pressure wasomi, kwamba lazima wawe na maisha ya juu, like kama ulivomtolea mfano huyo bro wako sio vizuri kabisa. Kama mtu ulikimbia umande tuliza ball wacha wasomi tuendeshe maisha yetu kwa style tunayoijua sisi. Hivi wewe unadhani kuna siku utajifananisha na huyo kaka yako?? Hujasoma hujasoma tu.. acha wivu kwa wasomi
 
Nyinyi wenye dgree ndio mjikague sisi ni wapambanaji kitambo maisha yanakwenda wala hatuchagii kazi
..Wasomi wengi wanakosea kitu kimoja Kuishi kwa kile walichoaminishwa na makaratasi. na ambao hawakusoma wanaishi kulingana na Mazingira....Hivyo msomi lazima afail kuwa Tajiri kwa sababu anaamini makaratasi na huyu anaamini muda na Mazingira...na wasomi wanatakiwa wajue kuwa huwezi kuwa ndani ya kazi ukilindwa na mshahara alafu utegemee kuja kuwa kama Bakhresa....Toka humo ofisini kwenye kiyoyozi ndiyo Utaitwa TAJIRI...la sivyo baki kuwa bread Winner wa mke na watoto wako hakuna utafanya zaidi ya hivyo.
 
Linapokuja suala la pesa hapo mkuu tutatofautiana sana.

Vipaji na ujuzi vyote vinaweza Kukuletea pesa.

Ila si kila mwenye kipaji au elimu katoka ki maisha.

The way ulivyolinganisha mambo hapo ndo kuna kasoro

Umekompea vipaji na elimu ipi inaweza mfanya mtu Kuwa tajiri

Jibu lake wote wanayo chance, tena wasomi wanachance kubwa sana.

Jiulize nchi hii wangapi wenye vipaji vilivyo watoa ki maisha?

Then rudi angalia wangapi wenye elimu wametoka?


Kuhusu wakati wa kutoka hapo napo pana tatizo

Vipaji ugunduliwa mapema ila Life span yake mara nyingi huwa ni fupi
Yatazame maisha ya vijana wetu wanavyopukutika kila siku.


Elimu uwekezaji wake ni wa muda mrefu, Thank God hata return yake ni Life long ukijaliwa afya njema.


Kuhusu mafanikio hapo ndo tutatofautiana kabisa

Kwako wewe mafanikio ni magali na nyumba na benk balance yenye mamilioni....

Kwa mwingine mafanikio ni kuwa kiongozi wa watu tu au

Kuwa daktari bingwa anayetoa huduma ya kuokoa maisha ya watu na kulejesha furaha kwenye maisha ya watu. .....yaani ile Dr asante kwake ni mafanikio tosha n. K

Back to money mkuu

Hapa ndo huwa nacheka kinoma, ukiwa haujui kuhusu pesa unaweza sema mengi

Hivi unajua watu wanalipa garama kiasi gani kupata utajiri?

Umewahi kuua mtu ili upate pesa?
Umewahi kufanya mapenzi na maiti ili upate pesa?

Umewahi kupiga deal la rushwa na kuhujumu haki za watu ili kuwa tajiri?


Ndg yako mengi tusiyoyajua, linapokuja suala la pesa na utajiri.


Maisha in fumbo complex sana

Hitimisho langu ***

kibongo bongo watu wenye maisha yenye unafuu ni wasomi ukilinganisha na kazi zingine zote kwa ujumla wake.

Elimu haina mbadala, regardless ya changamoto zake.

Amina
 
Mbona wasomi waliotoboa kimaisha wapo kibao tena kuwazidi hata hao uliowataja kwakuwa wasomi wengi sio celebrates ndomana huwajui
 
Labda nianzie hapa,...
Unaposoma unakuwa umejipatia uhakika wa kuish maisha ya kawaida.. maisha haya ya kawaida yanapatikana kwenye ajira..
Ninaposema maisha ya kawaida namaanisha maisha ya kuweza kujimudu kwenye mahitaji muhim, yaani kula, kulala na kuvaa.

Endapo utaamua kutumia elim yako kwa kujiajiri, hii ndo njia pekee ambayo inaweza ikakuletea mafanikio yasiyokuwa na mipaka... hapa ndo unaweza ukaishi hayo maisha ya kina babu tale.

Wasomi wengi wanapofika kwenye njia panda hii.. ya kuchagua kutumia elim yao kuajiriwa au kujiajiri, wengi huwa wanaenda kuajiriwa... hii ni kwasababu

i.mifumo yetu ya elim inatuandaa kuajiriwa na wanajamii kwa ujumla wanaamin sana kwenye kuajiriwa.. yani ukiwa msomi, mafanikio yako ni kupata ajira kwenye kampuni nzuri.
ii. Ukimaliza kusoma... kuajiriwa ni kitu ambacho tayari umekishika mkonon, kwahyo wengi huwa wanapita njia hii kutokana na uraisi.
Hivyo bhas, unapoamua kujiajiri, unakuwa umeamua kupita njia ngum lakin isiyokuwa na mipaka kwenye mafanikio,
Kutokana na hili wasomi wengi huwakuti kwenye kujiajiri, utawakuta wapo kwenye ajira na wanaishi maisha ya kawaida mnoo.

Tugeukie upande kwa kina babu tale,
Hawa jamaa hawajasoma, hivyo bhas, hawana option ya kuajiriwa.. yaani ni lazima wajiajiri... hivyo bhas njia wanayopita hawa jamaa haina mipaka ya mafanikio, na kwakuwa hawana option nyingine, bhas wengi wao huwa wanapigana kufa na kupona, mapigano hayo huwafikisha kwenye mafanikio kwa urahisi.
Na hyo ndo sababu leo hii ukiwaangalia majamaa wengi ambao hawajasoma na wameamua kujiajiri, wana mafanikio makubwa saana ukilinganisha na wasomi wengi.
NB
Unaposoma unakuwa umepata mtaji mkubwa sana.... ambao mtu ambaye hajasoma, huwa hana, ukiamua kuutumia mtaji huu kujiajiri, una uwezekano mkubwa sana wa kufanikiwa na kumzidi mtu ambaye hajasoma.
 
Wasomi wa Tz hawataki ku risk usomi wao wakajiajiri kama Bill Gates alivyofanya hata chuo asimalize. Pili wasomi wa Tz wanajikweza na hawana nidhamu ya kujituma. Hawawezi kuwa kama Wachina ambao hawachagui kazi (hata biashara ya mahindi ya kuchoma wanafanya). Mwisho wasomi wengi hawana nidhamu ya kudunduliza (to save money for future investment). Msomi wa Tz akiwa na mshahara wa milioni anataka akae nyumba 'ya hadhi yake' anataka "atanue" na mabinti warembo. Hiyo milioni haitoshi. Akienda kozi akapata promosheni ya kupata mshahara milioni mbili anaongeza matumizi mara mbili na haweki hela yoyote. Ndio maana mshahara unapochelewa siku mbili hata huku JF mapovu yanaanza kuwatoka watu. Kamwe mshahara hauwezi kumfanya mtu tajiri.
Pamoja Mkuu
 
Shule zote zinafundisha kuajiriwa.....
wasomi wengi wanafundishwa kuajiriwa ..
ukiweza kujiajiri ni freedom kubwa sana
but kwa kila Babu Tale mmoja au Diamond mmoja alieweza
kuna wengine 200 au zaidi wameshindwa na hali zao mbaya kupita maelezo

So kuajiriwa ni nafuu kuliko kushindwa kujiajiri..ingawa kujiajiri ni better ukiweza fika
Upo sahii mkuu
 
Tatizo ni simple ,watu wanasoma ili waajiriwe -a very stupid notion. Unatakiwa usome ili uelimike -kisha utumie ile elimu na ubunifu kujiletea maendeleo uwe umeajiriwa au hujaajiriwa.Halafu wengi wanaonaga wanamfanyia kazi mwajiri kwa hiyo wanakuwa na go slow badala ya kujua unajifanyia kazi mwenyewe kwa hiyo u-hustle major time. Lakini pia sote hatuwezi kuwa matajiri.
 
habari wadau..

nilikuwa natazama kwenye tv kipindi cha arobaini ya mtoto wa babu tale.. hiyo nyumba ya babu tale ni ndoto za wasomi wengi kuimiliki.. ni wasomi wachache sana wanaimiliki tena wengi ya hao wachache ni kwa rushwa, na ufisadi.. sio kwa hela halali..

mahojiano ya fella pia nyumbani kwake mbagala... napo maisha yake yanaonekana yana financial freedom kubwa kuliko hata ya kaka yangu ambaye ni lecture mzumbe kwa miaka mingi na ni mbahili sana huyo bro.. ila hana maisha na vitega uchumi kama vya fella.. na bro ana umri mkubwa kuliko fella na amefanya kazi miaka mingi kama mhadhiri

mwisho kabisa kanumba..

hadi mauti inamkuta alikuwa na miaka 28.. ila aliacha kampuni yake... magari kadhaa ikiwemo lexus, na hiace,, na account yake benki ilikuwa na milion 40 savings... je wasomi wangapi wenye miaka 28 wana uwezo wa kuwa na savings ya milion 40... na huku maisha mengine yanaenda kama kawaida tena maisha ya anasa sio ya kula matembele

sijamtaja diamond sababu kila mtu anajua mchango wake..

naomba tuelezane ukweli wasomi tunakosea wapi kiasi ikifika tarehe 23 tu humu thread za mishahara imechelewa zinakuwa nyingi sana,,, na wengine tunakopa hadi elfu 10 ili zisogeze siku mbele..

tutasema ni vipaji hatuna,, je babu tale au fella wana kipaji gani? mbona hawaimbi, wala hawana studio tuseme ni ma producer.. ila wana maisha mazuri tu... je degree zetu zinatusaidia kweli au zinaturudisha nyuma..

kuna thread ya visa humu..watu wengi wanalalamika kunyimwa visa na balozi hasa wa marekani na canada.. na tena wengi ya wanaolalamika ni wasomi wana elimu kubwa sana.. na wanashangaa kina fella, au babu tale wakipeleka documents tu visa wanapewa na wanasafiri mara nyingi kama JK vile kushangaa dunia.. ila wasomi hatuwezi hata kuweka mazingira ya kumshawishi mzungu akupe visa ukatembelee nchi yake

dick sound mfunga mziki wa magari magomeni.. wengi waliokaa magomeni wanamjua na amewahi kuwauzia maji kwenye madumu ya mkokoteni pale magomeni, anasukuma mkokoteni anauza maji kipindi ametoka kwao iringa... angalia leo alipo ana nyumba kibao mpaka mama yake kamjengea nyumba dar... na angalia gari zake anavyozibadili kila mwaka. angalia umri wa dick hata 35 sizani kama amezidi.. hizi degree zinatusaidia kweli au zinatufelisha?
Unataka hao wasomi nao waingie kwenye biashara ya nganda?
 
Back
Top Bottom