Maisha ya Babu Tale, Fella, hayati Kanumba yana financial freedom kuliko wasomi wengi. Tunakosea wapi?

Wasomi wa Tanzania matajiri wapo wengi tu. Weka Maengineer, mawakili, madaktari bingwa, na watu wa fani mbalimbali waliojiajiri na kuajiriwa. Kiufupi wasomi ndo kundi la watu wenye maisha mazuri kuliko wote hapa nchini.

Maisha mazuri sio tu utajiri uliopindukia ila ni kwamba watu wanajenga, wanasomesha na kumiliki mali kwa kazi zao. Ndio kuna wasomi wanaotoka shule na kupitia wakati mgumu ila hayo ni mapito tu ambayo hata hao wasanii wamepitia. Tukumbuke pia nchi hii mishahara ni midogo. Kuna wasomi nchi zingine wanapata pesa nyingi sana zaidi ya hao wasanii unaowataja hivo huweza waponda wasomi wetu kwa hilo.

Finally sio kila fani mtu anaweza kujiajiri. Na pia kwenye maisha kila mtu ana ndoto yake na kujiajiri sio ndoto ya kila mtu.

Kwenye maisha mafanikio sio kiasi cha fedha ulichotunza benki ila ni kutimiza malengo uliyojiwekea. Sio kila mtu duniani kasoma kwa lengo la kuja kuwa tajiri.
 
habari wadau..

nilikuwa natazama kwenye tv kipindi cha arobaini ya mtoto wa babu tale.. hiyo nyumba ya babu tale ni ndoto za wasomi wengi kuimiliki.. ni wasomi wachache sana wanaimiliki tena wengi ya hao wachache ni kwa rushwa, na ufisadi.. sio kwa hela halali..

mahojiano ya fella pia nyumbani kwake mbagala... napo maisha yake yanaonekana yana financial freedom kubwa kuliko hata ya kaka yangu ambaye ni lecture mzumbe kwa miaka mingi na ni mbahili sana huyo bro.. ila hana maisha na vitega uchumi kama vya fella.. na bro ana umri mkubwa kuliko fella na amefanya kazi miaka mingi kama mhadhiri

mwisho kabisa kanumba..

hadi mauti inamkuta alikuwa na miaka 28.. ila aliacha kampuni yake... magari kadhaa ikiwemo lexus, na hiace,, na account yake benki ilikuwa na milion 40 savings... je wasomi wangapi wenye miaka 28 wana uwezo wa kuwa na savings ya milion 40... na huku maisha mengine yanaenda kama kawaida tena maisha ya anasa sio ya kula matembele

sijamtaja diamond sababu kila mtu anajua mchango wake..

naomba tuelezane ukweli wasomi tunakosea wapi kiasi ikifika tarehe 23 tu humu thread za mishahara imechelewa zinakuwa nyingi sana,,, na wengine tunakopa hadi elfu 10 ili zisogeze siku mbele..

tutasema ni vipaji hatuna,, je babu tale au fella wana kipaji gani? mbona hawaimbi, wala hawana studio tuseme ni ma producer.. ila wana maisha mazuri tu... je degree zetu zinatusaidia kweli au zinaturudisha nyuma..

kuna thread ya visa humu..watu wengi wanalalamika kunyimwa visa na balozi hasa wa marekani na canada.. na tena wengi ya wanaolalamika ni wasomi wana elimu kubwa sana.. na wanashangaa kina fella, au babu tale wakipeleka documents tu visa wanapewa na wanasafiri mara nyingi kama JK vile kushangaa dunia.. ila wasomi hatuwezi hata kuweka mazingira ya kumshawishi mzungu akupe visa ukatembelee nchi yake

dick sound mfunga mziki wa magari magomeni.. wengi waliokaa magomeni wanamjua na amewahi kuwauzia maji kwenye madumu ya mkokoteni pale magomeni, anasukuma mkokoteni anauza maji kipindi ametoka kwao iringa... angalia leo alipo ana nyumba kibao mpaka mama yake kamjengea nyumba dar... na angalia gari zake anavyozibadili kila mwaka. angalia umri wa dick hata 35 sizani kama amezidi.. hizi degree zinatusaidia kweli au zinatufelisha?
zuruma zao unazijua kuliko wasanii wanao show tv
 
Ni wangapi sanaa imewalipa kama babu tale, salaam...fela diamond.?

Hao wote wamefanikiwa sababu ya mtu 1 diamond, kabla hajawa manager wa diamond alikua kawaida tu.

Mwanafa na sanaa yake ila aliamua kusoma aliamini atapata mafanikio kupitia elimu kuliko sanaa..

Uchumi wetu bado upo chini usitegemee msomi akawa na maisha mazuri wakati uchumi hauruhusu labda uwe fisadi, mtu wa deals ofisini ndiyo angalau utakua na mafanikio makubwa.
 
mshahara umejaa makato,biashara mjini imejaa mapato

nikki wa pili
inspiring punchline
 
Sasa mbona hamuwahesabu mamilioni ya wasiosoma wanaoishi kwa dhiki hata hela ya kula ni mtihani. Hii hoja ya kulaumu elimu haina mshiko kabisa. Afadhali hata mngefananisha wafanyabiashara wasiosoma na wasomi wasio na pesa. Pesa za michezo, filamu na muziki ni kwa wachache watu tu walio bora katika fani hizo.
 
Wafanye chochote kitakacho wawezesha kuwa na uhuru wa kifedha.
Asante.

Sasa pendekeza nin kifanyike.
2. Je wapewe magari wote?

Wapewe majumba,

Au madaktari wache kutibu wawe maprojuza,

Walimu waaidundishe wawe diamond

Em brify
 
61 Reactions
Reply
Back
Top Bottom