Wahitimu wa Vyuo mnakwama wapi? Kina Millard Ayo, MC Garab, Babu Tale, Hamissa Mobetto wanakimbiza kutawala fursa za social media

FRESHMAN

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
8,822
33,531
Habari wadau.

Kila mwaka udsm inamwaga vijana graduates wenye degree mbali mbali.

Mzumbe na udom hivyo hivyo.

Ajira ni ngumu wote tunajua, graduates karibu wote wa vyuo hivyo vikuu huwa wanatumia social media mbali mbali.

kizazi cha internet kinatambua kwamba kuna fursa nyingi za kupiga hela na ajira zinapatikana ukiweza kutawala ama kujibrand kwenye mtandao.

1. Vyuoni kuna wadada kibao wana tabia kama za Hamisa mobetto, najiuliza wanakwama wapi kutumia tabia zao hizo hizo Kujibrand na kupiga hela za mtandaoni. Hamisa mobetto form 4 failure anawazidi vipi ujanja dada zetu wenye tabia kama zake waliojaa vyuo vikuu vyetu.

2. Mc Gara B ni mwalimu level ya diploma kasoma zake kigurunyembe teachers college.. kajiongeza kwa kujibrand mtandaoni. Kawa MC mkubwa anapiga hela harusi moja anachaji milioni 4. kwenda kuongea masaa kazaa ukumbini. wasomi wa vyuo vikuu na degree zetu tunakwama wapi kujibrand kwa kutumia elimu zetu tuwe zaidi yake.

3. Millard Ayo na yeye hivyo hivyo. form 4 failure kasoma zake certificate ya journalism tu vyuo vya kienyeji. ila ndie amedominate soko la habari. sababu kuu kajua kujibrand mtandaoni.. udsm inamwaga graduates wenye degree za uandishi wa habari kila mwaka, wanakwama wapi kujibrand kwa kutumia elimu zao wamkimbize millard ayo. maana internet unajibeba mwenyewe kwa content zako

Babu Tale na yeye kajiongeza kadandia umeneja WCB, umembeba mpaka kaenda bungeni, wasomi wa managemet degrees wanamwagwa kila siku na vyuo vikuu vyetu, why hawajiongezi kwenye fursa za ku manage wasanii.

Wasomi tunakwama wapi kutawala ajira za mitandaoni
 
Mwijaku anawawakilisha hao graduates

Mwijaku anajitahidi kuwakilisha kwa kufanyia kazi degree yake ya maigizo.. ila graduates wenzake wanamsema vibaya wanamuona chizi anatia aibu wasomi

pacha wa mwijaku baba levo na yeye ni form failure. wasomi wangekuwa wamechangamka mwijaku angekuwa na pacha msomi mwenzake. ila sababu hayupo baba levo kachukua nafasi
 
Kama degree zenyewe zinazalisha watu wa type ya kina mwijaku unategemea aende akadominate kwenye field ipi mkuu?
 
Elimu tunayosoma, inaondoa ile akili tuliozaliwa nayo(u-genius) na kuwekewa mawazo ya watu wengine kwenye ubongo; na hatimaye kutunukiwa vyeti kwa kuweza kubeba mawazo ya watu wengine vichwani mwetu.
Hawa wengine wamefanikiwa, kwa sababu wanaubeba ule u-genius​
 
Siri ipo kwenye sehemu moja, Uchawi mkuu, uchawi, We nenda na Phd yako ya public administration, msukuma ni darasa la 7 lakini ana Phd ya uchawi na kuloga..uone kwenye utafutaji pesa nani atafanikiwa.

Fanya kazi kuanzia asubuhi mpaka jioni utaishia kupata hela ya kula tu..mwenzio anafanya kazi na analoga, lazima akupige gepu.

Mafanikio/umaarufu ni swala ambalo lipo spiritual.
 
Mwenye kudharau ilmu binfsi huwa namuonea tu huruma!

Msisahau huyo Millard pamoja na hapo alipofika ni wasomi kawaajili wanamfanyia kazi

Anao content developers
Anao graphics designers
Anao sound editors
Anao video producers and video editors

In short anamiliki kampuni iliyokamilika na inayoendeshwa kama inavyotakiwa

Yeye alipata wazo + capital mengine mengi sasa yanayaendelea sio mawazo yake tena Bali ya watu tena wenye taaluma zao walioajiliwa na kampuni.

Sent from my phone
 
Tatizo lao wanasoma ili waje kuajiriwa na serikali walipwe mishahara minono na posho ndefu za uhakika plus kiinua mgongo na pensheni ya uzeeni mpaka kifo. Hawapendi ku scratch from zero ku archieve devolopment zao independent japo wana elimu za kutosha kuanzisha firms zao
 
Back
Top Bottom