Maisha ya Babu Tale, Fella, hayati Kanumba yana financial freedom kuliko wasomi wengi. Tunakosea wapi?

FRESHMAN

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
4,456
2,000
Habari wadau..

Nilikuwa natazama kwenye TV kipindi cha arobaini ya mtoto wa Babu Tale. Hiyo nyumba ya Babu Tale ni ndoto za wasomi wengi kuimiliki. Ni wasomi wachache sana wanaimiliki tena wengi ya hao wachache ni kwa rushwa, na ufisadi, sio kwa hela halali.

Mahojiano ya Fella pia nyumbani kwake Mbagala napo maisha yake yanaonekana yana financial freedom kubwa kuliko hata ya kaka yangu ambaye ni lecturer Mzumbe kwa miaka mingi na ni mbahili sana huyo bro ila hana maisha na vitega uchumi kama vya Fella na bro ana umri mkubwa kuliko Fella na amefanya kazi miaka mingi kama mhadhiri.

Mwisho kabisa Kanumba. Hadi mauti yanamkuta alikuwa na miaka 28 ila aliacha kampuni yake, magari kadhaa ikiwemo Lexus na hiace na account yake benki ilikuwa na milion 40 savings.

Je wasomi wangapi wenye miaka 28 wana uwezo wa kuwa na savings ya milion 40 na huku maisha mengine yanaenda kama kawaida tena maisha ya anasa sio ya kula matembele.

Sijamtaja Diamond sababu kila mtu anajua mchango wake.

Naomba tuelezane ukweli wasomi tunakosea wapi kiasi ikifika tarehe 23 tu humu thread za mishahara imechelewa zinakuwa nyingi sana na wengine tunakopa hadi elfu 10 ili zisogeze siku mbele.

Tutasema ni vipaji hatuna, je Babu Tale au Fella wana kipaji gani? Mbona hawaimbi wala hawana studio tuseme ni ma producer ila wana maisha mazuri tu.

Je degree zetu zinatusaidia kweli au zinaturudisha nyuma?

Kuna thread ya visa humu watu wengi wanalalamika kunyimwa visa na balozi hasa wa Marekani na Canada na tena wengi ya wanaolalamika ni wasomi wana elimu kubwa sana na wanashangaa kina Fella au Babu Tale wakipeleka documents tu visa wanapewa na wanasafiri mara nyingi kama JK vile kushangaa dunia ila wasomi hatuwezi hata kuweka mazingira ya kumshawishi mzungu akupe visa ukatembelee nchi yake.

Dick sound mfunga mziki wa magari Magomeni wengi waliokaa Magomeni wanamjua na amewahi kuwauzia maji kwenye madumu ya mkokoteni pale Magomeni anasukuma mkokoteni anauza maji kipindi ametoka kwao Iringa. Angalia leo alipo ana nyumba kibao mpaka mama yake kamjengea nyumba Dar na angalia gari zake anavyozibadili kila mwaka angalia umri wa dick hata 35 sizani kama amezidi.

Swali kwa wasomi wote ambao tumeajiriwa na tunalalamika mishahara ikichelewa, au ikikosa increments je hizi degree zinatusaidia kweli au zinatufelisha?
 

FRESHMAN

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
4,456
2,000
naomba unitajie msomi moja tu aliyetoboa kati ya wengi hapa tanzania ambaye ana savings milion 40 benk na hajazidi miaka 28.. ambaye hela yake imeletwa na elimu yake.

daimond ana miaka 29... na umesema ni mmoja kati ya wengi... naomba unitajie na msomi mmoja kati ya wengi ambaye ana miaka 29 hapa tanzania mwenye asset au kipato kumzidi diamond ambapo elimu yake na ajira yake imemfanya apate hizo asset... iwe vita ya mmoja mmoja tu

Ndo anakosea kufananisha kuna mamilioni ya watu kama babu tale na diamond hapa bongo ambao for years wamepambana na hawajatoboa nataka appreciate kuwa kwa bongo elimu inatoa kuliko sector Nyingine yoyote
 

The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
41,565
2,000
Shule zote zinafundisha kuajiriwa.....
wasomi wengi wanafundishwa kuajiriwa ..
ukiweza kujiajiri ni freedom kubwa sana
but kwa kila Babu Tale mmoja au Diamond mmoja alieweza
kuna wengine 200 au zaidi wameshindwa na hali zao mbaya kupita maelezo

So kuajiriwa ni nafuu kuliko kushindwa kujiajiri..ingawa kujiajiri ni better ukiweza fika
 

prospilla

JF-Expert Member
Mar 31, 2015
844
1,000
Ugumu wa maisha kwa mtu aliyesoma na ambaye hajasoma ni tofauti mkuu, mtu ambaye hajasoma anakuwa na maisha magumu haswaaaa, ila hawa wa degree si kwamba wana maisha magumu hapana ila tu hawana fedha za ku afford luxuries. Ila basic needs wanazimudu bila wasiwasi ukilinganisha na wengi ambao hawakufanikiwa kiwango cha juu cha elimum
 

FRESHMAN

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
4,456
2,000
Wasomi wangapi unaowafahamu wewe? Acha ulimbukeni...elimu haina mbadala hata hao unaowataja hawana academic freedom hawawezi kufanya kazi nyanja za kimataifa.

wapi nimeponda elimu sio muhimu... soma thread upya? nimeuliza wasomi tunakosea wapi?? je degree zetu zinatusaidia kweli.... wewe ni mjinga sana hata kusoma na kuelewa huwezi
 

Iceberg9

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
18,267
2,000
Kila kitu kina nafasi yake na umuhimu wake katika maisha yetu... Wapo waliotumia degree zao wakatoka ila kwakuwa sio celebrity huwezi ona mafanikio yao public, wapo ambao hawana elimu wametoka kama hao nk.... Maishi siyo ya kukariri wewe endelea kukariri utaishia kuhesabu utajiri wa wenzio tu
 

lelulelu

JF-Expert Member
Dec 8, 2017
313
250
Ugumu wa maisha kwa mtu aliyesoma na ambaye hajasoma ni tofauti mkuu, mtu ambaye hajasoma anakuwa na maisha magumu haswaaaa, ila hawa wa degree si kwamba wana maisha magumu hapana ila tu hawana fedha za ku afford luxuries. Ila basic needs wanazimudu bila wasiwasi ukilinganisha na wengi ambao hawakufanikiwa kiwango cha juu cha elimum
acha uongo mkuu
 

Beira Boy

JF-Expert Member
Aug 7, 2016
17,954
2,000
naomba unitajie msomi moja tu aliyetoboa kati ya wengi hapa tanzania ambaye ana savings milion 40 benk na hajazidi miaka 28.. ambaye hela yake imeletwa na elimu yake.

daimond ana miaka 29... na umesema ni mmoja kati ya wengi... naomba unitajie na msomi mmoja kati ya wengi ambaye ana miaka 29 hapa tanzania mwenye asset au kipato kumzidi diamond ambapo elimu yake na ajira yake imemfanya apate hizo asset... iwe vita ya mmoja mmoja tu
Hayupo
 

ZEE LA HEKIMA

JF-Expert Member
Aug 10, 2015
1,312
2,000
Wasomi wa Tz hawataki ku risk usomi wao wakajiajiri kama Bill Gates alivyofanya hata chuo asimalize. Pili wasomi wa Tz wanajikweza na hawana nidhamu ya kujituma. Hawawezi kuwa kama Wachina ambao hawachagui kazi (hata biashara ya mahindi ya kuchoma wanafanya). Mwisho wasomi wengi hawana nidhamu ya kudunduliza (to save money for future investment). Msomi wa Tz akiwa na mshahara wa milioni anataka akae nyumba 'ya hadhi yake' anataka "atanue" na mabinti warembo. Hiyo milioni haitoshi. Akienda kozi akapata promosheni ya kupata mshahara milioni mbili anaongeza matumizi mara mbili na haweki hela yoyote. Ndio maana mshahara unapochelewa siku mbili hata huku JF mapovu yanaanza kuwatoka watu. Kamwe mshahara hauwezi kumfanya mtu tajiri.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom