Maisha ni vita, usikariri kutumia silaha Moja

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,339
51,884
MAISHA NI VITA, USIKARIRI KUTUMIA SILAHA MOJA!

Anaandika Robert Heriel

Wataalamu WA vita watakubaliana na Mimi kuwa uwapo kwenye vita hakuna kanuni ya Moja Kwa Moja inayotumika, mtapigana kadiri adui ajavyo na kadiri Hali ilivyo, hakuna kukariri silaha Fulani ndio lazima uitumie kila sehemu, silaha itatumika kulingana na Mazingira.

Hivyo ndivyo maisha ya binadamu yalivyo, maisha kikanuni na kifomula yanayutumia mfumo wa mchanganyiko wa matukio yanayokuja bila kutarajia hivyo mtu atapaswa asitumie formula Moja kuyaendesha maisha yake, yaani mtu awe Flexible upesi kadiri awezavyo.

Jana na leo na kesho huja Kwa namna yake. Leo umzima kesho sio ajabu ukakikuta kwenye Wheelchair ukiwa hauna miguu, hivyo kanuni na formula zinatakiwa zibadilike.

Maisha ni vita, na kila vita ina silaha, na agenda.
Silaha katika maisha ni Nguvu, akili, Rasilimali, muda, Imani, n.k.

Agenda ya vita ni maslahi ya kila mmoja kuishi Kwa furaha, ambayo ndio huitwa mafanikio Kwa kila binadamu.

Furaha zinatofautiana Kati ya mtu na mtu hivyo hata upambanaji katika vita na silaha zitakuwa tofauti.

Elimu ni sehemu ya silaha iliyopo kwenye Akili, kwani hutoa maarifa, ufahamu, Ujuzi na kukuza kipaji.

Kwenye maisha sio kila Mazingira utapaswa utumie silaha ya Elimu, utapigwa, zipo sehemu za kutumia elimu ikiwa vita itahitaji hivyo, lakini kama maisha hayatakuruhusu kutumia elimu haimaanishi hakuna silaha zingine, na Kama utafikiri unasilaha moja tuu ambayo ni elimu basi ni rahisi kushindwa vita.

Au usidhani Kwa vile Hauna Elimu basi ukafikiri ndio vita umeshindwa, hasha! Zipo silaha zingine Kama kutumia Nguvu Kama walivyosema wahenga; mtaji wa Masikini ni nguvu zake mwenyewe, IMANI, Iwe Imani ya Mungu au Imani ya kishirikina au Uchawi vyovyote utakavyoona, vita ni vita.

Muhimu ni kuwa kila Jambo linamatokeo na hatma yake.

Mazingira hayaruhusu Nguvu, basi tumia akili.
Mazingira hayaruhusu akili, tumia nguvu.
Mazingira hayaruhusu akili na nguvu, tumia IMANI.
Usikubali kushindwa.

Kizazi cha sasa kinatabia ya kukariri Hali inayopelekea kupoteza mapambano mengi.

Ukiona unashindwa Vita ya mjini, nenda kijijini
Ukiona unashindwa Vita ya shamba, nenda Mjini.
Ukiona unashindwa vita ya Ardhi basi tumia anga.
Ukiona unashindwa ardhini basi tumia Maji.

Weka akilini, usikariri kwenye vita, kuwa na uwezo kubadilika upesiupesi kuendana na Kasi ya vita.

Ukiona Jambo lolote unashindwa kuliondoa au kulishinda basi litumie Kama nyenzo ya kujipatia Mapato,

Mfano, wewe ni mlevi, umeshindwa kuacha pombe, anzisheni mashindano ya walevi kisha watozeni watu pesa waje waangalie mchezo wenu wa pombe.

Wewe ni mgomvi, unapenda kupigana na Kupiga wengine, jiingize kwenye michezo ya ngumu, nenda kawe Mwanajeshi au polisi ukapigane na wahalifu.
Utakuwa mgomvi wa kulipwa.

Kila la Kheri

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Nakubaliana. Neno nguvu kwenye mada yako lipamue kimaana. Watu wasijui ni nguvu pekee za misuli zipo mguvu nyingine pia.
 
Pesa imetufanya watumwa, ukiwa na pesa unapata kila kitu kutoa upendo wa kweli na uhai.

Tutafute pesa ila tusisahau kuishi.

Tusiabudu pesa.
 
nakubaliana na wewe ila elimu ukiweza kuitumia vizuri basi unakua tayar upo mbele nkimaanisha una advantage kubwa sana na asie na elimu
 
Kuna wengine watakuwa wamehalalishiwa ushirikina hapa,
Na ndipo watapoenda kufa ya mambo ya ajabu ajabu,
Na kwa mawazo yangu haiwezekani uwe na elimu halafu ushindwe na maisha,
Ukishindwa manake huna elimu
 
Back
Top Bottom