Wild Flower
JF-Expert Member
- Jul 20, 2023
- 977
- 1,965
Jeshi la Polisi limewataka wananchi kuacha matumizi ya silaha bandia, likisema vitendo hivyo ni makosa yanayokiuka sheria na vinaweza kuhatarisha usalama wa watu na mali zao. Akizungumza leo Juni 19, 2026 katika maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma, Mrakibu wa Polisi Kamisheni ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Kitengo cha Udhibiti na Usimamizi wa Silaha, Neema Laizer amesema baadhi ya wananchi wamekuwa wakitumia silaha bandia kwa njia mbalimbali bila kufahamu kuwa matumizi yake yanaweza kusababisha taharuki na kuchukuliwa hatua za kisheria.
Amesema silaha bandia zinafanana kwa kiasi kikubwa na silaha halisi, jambo ambalo linaweza kuwafanya wananchi na vyombo vya ulinzi na usalama kushindwa kutofautisha kati ya halisi na bandia wakati wa matukio mbalimbali. “Matumizi ya silaha bandia ni makosa kwa mujibu wa sheria, tunawasihi wananchi waache tabia ya kutumia au kumiliki silaha hizo kwa namna inayoweza kuhatarisha usalama wa jamii,” amesema Neema.
Pia, Neema amewataka wazazi na walezi kuacha tabia ya kuwanunulia watoto vifaa vinavyofanana na bastola au bunduki kama zawadi, hatua hiyo si sahihi katika malezi na inaweza kuwajengea watoto mtazamo usiofaa kuhusu matumizi ya silaha.