Maisha na mikasa ya safari yangu nchini DR Congo miaka ya 2000's hadi kutaka kupigwa risasi hadharani

Chai imeanza sasa.

Mwakibolwa alipambana na M23 na wala sio ADF.

We hadithia tu khs Safari yako hayo mengine utaanza kutunywesha chai ya motoooo.

Acha ujuaji, M23 ndiyo iyo ya Sultan Makenga ila ndani ya Congo kuna waaasi wengi mno wakiwemo ata ao Adf na wengineo sasa kuna wakati haujui unapigana na M23, au maimai au Naru au wengineo sasa unaweza jikuta unaisi unapigana na M23 kumbe unapigana na Maimai....na apa kwenye aya mapigano ya M23 akumbukwe General wa Congo marehemu mamadou Ndala
 
kuna mjinga mmoja anajifanya mjuaji humu anajifanya mwanajesh kisa kapewa gwanda na masufuria ya upishi
 
Inaendelea sehemu ya nane..... nawasalimu kwa kicongo mko byee ?

Haya tusonge tena ebwanae sasa bunduki zikawa zimeelekezwa kwetu vijana wa mafuta wameshasepa zao kwa kusindikizwa na risasi nyingi tu kimbembe kwetu tuliobaki niseme tu siku hiyo nikaona sasa sina uhai tena nasubiri kifo tu basii akili ikawa imeruka kitambo lakini rama katulia tu anawacheki tu harakati zao yani jamaa wanarusha hewani lisasi hatari kama wameona magaidi vile sasa niseme kidogo sehemu tuliyokuwa ni kama pale ambako hata mtu akikupiga robo huwezi kupata msaada yani tupo chaka kama sehemu kulikuwa na godauni hivi halafu kuna ukuta mlefu hivi ...ambao ndo wale vijana waliuruka .

Ghafla kikatoka kibao kwa yule kiongozi wao rama akakiona akajikinga kwa mkono hakikufika usoni kumbuka mimi niko nyuma ya rama na tetemeka kishenzi yani kiongozi wao akawa anafoka akaamriklsha ikala chini (yani tukae chini) .

Ngoja niseme kitu kidogo kuna hali ya kiasili huwa inatokea vitu viwili vikikutana na vikiwa na haiba( sifa ) yenye ufanano amini usiamni haviwezi shikamana matokeo yake vitapatana na kuheshimiana sasa wakati watwambia ikala chini mimi mtu mzima nipo chini kitambo lakini rama kakomaa hakukubali kabisa kukaa chini askali moja akageuza bunduki akataka kumpiga nakitako rama akakwepa kwa kuzuia kwa mikono kumbuka hapo sasa mimi kihoro juu najiuliza huyu jamaa rama ana akili kweli sasa ya nini kwa nini asikae tu chini .

TUHAME STORY KIDOGO.

Kama nilivyosema hapo nyuma kuna utofauti mkubwa sanaa kati ya mtu ambae sio muoga na mtu jasiri sasa pale rama alikutana na mtu jasiri mwenzio ndo maana nikasema majasiri wawili wa kikutana lazima pachimbike na mwisho lazima lazima waheshimiane yani mtu jasiri hata kama moja ana siraha mwingine hana asiekuwa nasilaha huwa haogopi chochote inakuwa sawa na yule kama vile wote wana silaha

Kipindi cha vita kuliibuka vitoto niseme kama vile vilikuwa vina sumbua Dar sijui mnaviita PANYA ROAD wale ndo wajasiri ninaowaongelea yani vinajua kabisa nchi hii ina dola ngumu lakini wao wanaingia nakusimamisha mtaa bila uoga tena na visilaha vya kienyeji lile sasa ndo chimbuko la watu jasiri sasa kutokana na ugumu wa maisha na makuzi congo vijana kama wale walikuwa wengi sanaa kwenye majimbo mbali mbali .

Sasa wakati vita inaendelea askali wakongo wakawa wanaasi hivyo kukatokea upungufu mkubwa sanaa wa wanajeshi wapiganaji ndo kiaina serikali kupitia viongozi wa majimbo na chama tawala wakawa wanawapenyeza jeshini kiaina kwa makubaliano vita ikiisha wataajiriwa lakini halikuwa lengo la serikali za majimbo kadhaa sio kongo nzima na ndo hivyo vikundi vya waasi vilivyokuja kujitokeza baadae ya vita na wengi wao walikuwa under 25 yani walikuwa wanachukuliwa miaka kama kumi na sita 16 na kuendelea anafundishwa kurusha risasi basi .
Kazi imeisha kesho asubuhi wanapandishwa kwenye roli frontline kupigana yani vikawa vinapiganishwa wao kwa wao katika majimbo yenye waasi vilikufa sanaa sasa baada ya vita kupoa waliorudi sasa mjini ndo kasheshe yake hiyo kama hao tuliokutana nayo yanii hata makanali wa jeshi walikuwa wanaviogopa hivyo vitoto kumbuka vimetoka kupigana vita tena vita ya uso kwa uso vimerudi mjini vimezaga yani nimwendo wa vurugu vina siraha nzito nzito na kombati mchamganyiko wa rangi yani wanaweza kupora gari wakawa wanatembea barabarani tena kwenye line ambayo sio yao wole wako umzibie barabara utajuta yanii ukiona gari linakuja usoni kwako wewe pisha hata kwa kuingia mtaroni lakini yeye apite .

Jiji lao so walikuwa wanajulikana migari yao mibovu haina taa wala madirisha yanii nimwemdo wa kuendesha tu ilimradi vurugu tu mtaani sasa ujichanganye uwe mgeni yani utapata tabu vingenevyo uwe na mtu ambae ni mcongo na maarufu au uwe na watu ambao wapo kwenye system angalau utanusurika.

TURUDI KWENYE STORY.

Sasa walitukamata pale nao hawakuwa wanajeshi wenyewe walikuwa wale vijana yani wale madogo ndo walikuwa wametuotea tena tuna mali mafuta pesa na gari mpya .

Sasa kama nilivyosema majasiri wanaheshimiana amini usiamani swala rama ukakata kutii maelekezo yao likaibuwa maswali sasa yakutaka kutujua sisi ni akina nani na kwanini tupo pale halafi cha kushangaza pembeni tumepaki gari mpyaa kabisa hili nalo nafikiri liliwachanganya kidogo kwa kifupi tu ni kwamba kwa kipindi hicho hadi sasa wanaoununua gari mpya ni serikali na watu wazito serikalini basii nadhani liliwatisha halafu hapo hatujaongea so hawajajua kuwa sisi ni raia wa wapi

Maswali ya kaanza ...

Wao :Nyinyi ni akina nani ?
Sisi: hatukujibu rama akatoa passport akawapa .KOSA

kile kiongozi chao kikasema sasa nyie na madocoma( document) mbele ya lisasi zinasema nini?ý

Moja akawa anamwambia wenzie wachukue mafuta chukua hiyo petrol mgari ( yani achukue zile dumu za mafuta.

Rama ndo akaonge sasa wakasikia kiswahili kimenyooka wakasema nyinyi batized ( alimaanisha wataanzania)?

Rama akasema ndio .

Wakauliza sasa mko mnafanya nini apa mnaiba mazutu(mazutu ni mafuta) mcongo .

Hapo ndo rama akawa anawaelezea kuwa tumeishia mafuta hivyi kuna rafiki zetu walikuja kutuuzia mafuta sasa walivyowaona nyie ndo wakakimbia kuogopa sisi tumeishiwa yani akabadili story kutoka sisi kuuza hadi kuwa wanunuzi na hiyo baadae ilitusaidia na kama tungesema tunauza mafuta labda hali ingefika kulazima wenye magari wafike pale tungeoneka sisi sio waaminifu tena wale maboss wangetuharibia kumbuka mpaka.mda huo wanajua tupo guest kule tumepaki .

Sasa katika kuhoji hoji maswali.ya hapa na pale ila kwa ukali na mikwara kibao kumbe kuna mmoja anajua kusoma akachukua ile pasaport akaisoma akaelewa kweli sisi ni watanzania ishu nikawa wanataka yale mafuta rama nae akawa anakoma nao .
Kuna kijana moja katika lile kundi akaamuuliza rama hizi gari niza kuprezince? ( yani kamaanisha gari niza ikulu si mpyaa?) Rama akaitikia ndio pale pale hawakukaa tena wakaondoka fasta hawakutaka hata kukaa tena yani ujanja wao wote sema hizi gari ni za ikulu huguswi tena wanakuwa wanajua ni za wakubwa na kuharibiwa kutawatia hatiani hata kuuawa

Congo kuna wababe wapo kwenye system ya chama tawala asikwambie mtu yani uguse gari lake atakusaka popote pale hata roho atakutoa sasa kumbe yale magari wale jamaa nao ni watu wa system kwenye chama tawala naona ujio wa zile gari walishajua ni za kina nani wakaona isiwe tabu wakasepa za sisi tukachukua mafuta yetu tukageuka tukarudi guest tukatulie kwanza .

Saa nane wale jamaa wakafika wakatupa chetu tukawakabidhi magari yao ila wakafurahi sanaa walikuja na dereva wakamwambia asubuhi atupitie lifti hadi boda wakati wakuondoka kwakweli walifurahi na walituongezea hela kidogo na yale mafuta tuliwaauzia madereva wengine
wa IT pale pale . Asubuhi tukaanza safari ya kurudi homeland tanzania na ndo mwanzo wa kuanza kazi za magari ya IT ukawa umeanza yakawa ndo Maisha yangu kuzunguka nchi mbali mbali ila katika harakati zangu nimeenda kongo zaidi kuliko nchi zingine.

Asante kwa kunifuatilia

MWISHO.

Simulizi inafikirisha sana...

Safi sana... Chapter Closed...
 
hhhaahaaa ama kweli kuna watu hamkati tamaa hapa duniani yanii bado mlikuwa mnaifuatilia hii story wazee niwaombe radhi sana sanaa sikuwa na simu kwa muda mrefu then nilikuwa nashughulikia kesi zetu za mirathi zikanivuruga akili nikasahau kuwa hata mimi ndo niliandika hii story1 kwa masikitiko makubwa ni Wahiidi kuwa akili ikitulia ntakuja kamalizie nilipoishia pia ntakuja na story mpya kuhusu hii ishu ya mirathi iliyokuwa imenitenga kabisa na jukwaa hili.asante sana na

stay tune..
 
Tunasubiri mkuu hii stori yako kama ilikuwa kweli basi umepitia mengi sana.
 
hhhaahaaa ama kweli kuna watu hamkati tamaa hapa duniani yanii bado mlikuwa mnaifuatilia hii story wazee niwaombe radhi sana sanaa sikuwa na simu kwa muda mrefu then nilikuwa nashughulikia kesi zetu za mirathi zikanivuruga akili nikasahau kuwa hata mimi ndo niliandika hii story1 kwa masikitiko makubwa ni Wahiidi kuwa akili ikitulia ntakuja kamalizie nilipoishia pia ntakuja na story mpya kuhusu hii ishu ya mirathi iliyokuwa imenitenga kabisa na jukwaa hili.asante sana na

stay tune..
Sawa
 
Kweny tukio la jamaa kudandia gari Ata bongo yapo sana iyovi msimba na kitonga mara nyingi sana matukio hayo kipindi Cha nyuma yalitokea sana Kuna jamaa walimshushia godoro si chini ya mia mbili kweny scania pale kitonga anakuja kufika iringa town godoro zote wamepiga chini jamaa alikua analia kama mtoto ila na madereva wa IT mnakimbiza sana gari kipande Cha kutoka mikumi had Unafika Iringa mnapiga sana chini gari sjui wengi inakuwa ugeni wa njia au ila yoyote Kwa yoyote Rama alikua mjanja mjanja Sana siku na mim nitakuja na nyuzi ya matukio niwahi shudia wakati nikiwa utingo wa malori ya mizigo
 
Ukileta utushtue hapa mkuu
 
Tupo na wewe mkuu
 
Tunasubiria mkuu
 
Inaendelea sehemu ya Pili.

Kwanza nikili tu kuwa sintojibu comments za watu ntakuwa straight moja kwa moja kwenye story yangu.

Haya basi tuendeleee safari ikawa imeanza alfajiri ya j2 ile wanaume tukaanza kupiga gia kwakweli mwendo wa magari ya IT si wa mchezo kumbuka kesho tumeshaambiwa ifikapo jumanne asubuhi tunatakiwa tumeshavuka boda ya tunduma upande wa pili NAKONDE kuna mizigo pale tunatakiwa tubebe ya wale jamaa imeachwa pale na bus la TaQwa .wazee tukaamsha mashine kama unavyojua gari ikiwa mpya ni kutembea tu mwanzo mwisho...

Jamaa yangu Rama alikuwa mzoefu wa njia check point za maaskali na tochi zinapokaa hivyo ilibidi mimi nikae nyuma yake akiaamsha nami naamsha akipunguza mwendo nami napunguza na kweli bwana mbele unakuta wazee na vitochi vyao wanaomba document na hela ya soda sisi tunachapa mwendo saa nne asubuhi tukanywa supu msamvu-morogoro tukafungasha nyama choma pale duma mwendo hapo sasa speed ikawa ni noma yanii jamaa yangu Rama anakimbia hadi naogopa aise .

Basi mwendo ukawa mwendo kweli kweli pia usisahau abiria tulikuwa tunabeba wa hapa na pale ili kupata kusave angalau kale ka hela ketu kasiishie njiani saa mbili usiku tunaingia Mbeya aise kama sijasahau tukapata hotel pale mwanjelwa sehemu safi tukapaki magari yetu lodge tukala tukalala mapema ili asubuhi tuwahi Tunduma ili tusubiri bus la Taqwa tuchukue mizigo yetu.

Tukalala pale kila mtu nachumba chake kama kawaida Rama akawa na mchuchu wake pale chumbani sijui alikomtoa ila mimi nilivyochoka hakika sikuwa hata na hamu ya demu mzee nikaangusha mapema saa kumi na mbili asubuhi tupo kwenye chuma zetu tunaitafuta Tunduma taratibu kama kawaida tuna vichwa vyetu viwili vitatu .

Saa tatu tupo Tunduma tunakunywa supu tukaonana clearing wa jamaa akafuta bond na kuclear baadhi ya document sisi tukawa tunasubiri mizigo japo jamaa alitutaka tuvuke siku hiyo hiyo upande wa pili lakini tulikata tukamwambia tutasubiri hapa hapa mizigo. Saa nne taqwa ikaingia tukaenda chukua mizigo tukapakia kwa gari mizigo yenyewe ni makapeti ya nyumbani tukafunga vizuri kabisà tulala .

Mapema asubuhi tukaamka tukaka kwenye foleni ya kuvuka boda baada ya kugonga passport zetu kufikia saa nne tukawa tumevuka boda ya tunduma tupo Nakonde jamaa yangu akanishauri tupumzike ili tutembee usiku lli tusipisha na maroli pia kuna kuwa na atuluvi hivyo akashauri tukapumzike mahala jioni ndo tuamshe .ikabidi nimsikilize tukaenda eneo pale pale boda ukiwa pale nakonde unaweza dhai upo tanzania kumbe ni upande wa zambia yani kunamchanganyiko wa wabongo na wazambia kibao.

Saa kumi na mbili tukaamsha aise sikujua.kumbe Zambia kubwa aise tulitembea giza likaingia aise unatembea kilomita hata mia hupishani na gari lolote halafu pori tupu.

Nyie tukafika kwenye kimji fulani kinaitwa SELENJI tukapaki hapo ili tule na tupumzike ebwanae kulala huo mji ni bora kulala kwenye gari kuna baridi seleenji njombe ikasome tukala pale kwenye hotel ya wasomali tukapaki na magari yetu pale tukalala pale asubuhi mapema bila hata kuoga tukaamsha mapema hapo ndipo nilipo anza kuona usumbufu wa askali wa zambia aise mnasemaga askali wetu wetu wanapenda rushwa nenda zambia yani gari mpya anakwaMbia kosa lako gari ni chafu gari hiyo ipo transit aise yote umwachie hata kwacha elfutano tu aise jamaa wana njaa sijapa ona.

Tukawa tunaitafuta mji wa KAPIRI MPOSHI hapo unajionea watu wana uolima aise kule jamaa wanalima serious sijui kwanini kuna njaa namna ile ...zambia kupata wali maharage ni ishu.

Kama sijasahau kutoka selenji kuna mji unaofuata pale unaitwa MPIKA ( mtanikumbusha kama ntakuwanimesahau) aise kile kipande ni hatari kutembea asubuhi sanaa au usiku kumbe wanapiga mawe hatariii wazambia ni washenzii.

Itaendelea.....soon.
Mwaka 2000 kulikua na tochi barabarani?
Nimeishia hapa kusoma,nshajua hii ni chai
 
hhhaahaaa ama kweli kuna watu hamkati tamaa hapa duniani yanii bado mlikuwa mnaifuatilia hii story wazee niwaombe radhi sana sanaa sikuwa na simu kwa muda mrefu then nilikuwa nashughulikia kesi zetu za mirathi zikanivuruga akili nikasahau kuwa hata mimi ndo niliandika hii story1 kwa masikitiko makubwa ni Wahiidi kuwa akili ikitulia ntakuja kamalizie nilipoishia pia ntakuja na story mpya kuhusu hii ishu ya mirathi iliyokuwa imenitenga kabisa na jukwaa hili.asante sana na

stay tune..
Karibu sana mkuu tunakusubili.
 
bongo man wadau walijua kuwa wakati waasi wanauvamia ule mji walidhani na wewe umeondoka na maji kutokana na ukimya.
 
Back
Top Bottom