Maisha halisi ya member wa JF ni tofauti kabisa na walivo humu

We jamaa hapo mwishon umenifanya nicheke
Yan na ID ya mshana alivo na mawan yake duuu!
Juzi wakati naenda Dodoma nilikaa siti moja na mzee ana kama miaka 50 or 60, aisee nilishangaa sana kuona yule mzee anatumia Jf.
Nilijaribu kumlia chabo nione Id yake ila alikuwa makini sana anapost huku anaficha simu na kuniangalia usoni...nadhani alikuwa Mshana Jr.
 
Bana eeh Argh!!! mi wala usije kunishangaa na jiko langu mahindi ya kuchoma nikisembeza mdogomdogo katikati ya halingumu yamaisha mahindi yenyewe wateja hakuna mpaka kamvua kakinyesha angalau alooo!!! Acha tu ...

Watu wanaham na mahindi ila pesa ya kununua hawana na mimi kugawa bure siwezi Basi taabu tupu

Usipate tabu mkuu ukitaka kuniona napatika Unyanyembeee au Mboka Manyema ... Taboraaa pale karibu kabisa na stend mpya ya mabasi ya mikoani almaarufu Mnyanyembe mchoma mahindi muulize mkatisha tiketi yeyote atakuleta mpaka kijiweni kwangu ...

Karibu uniungishe muhundi wa kuchoma mixer kwa pilipili mswaki full ugwadu babu yangu njoo utest ... kinyanyembe tena sio hio mindi yenu ya kubanikwa mnayo kula huko kwenu D'salaam ... Kwa sababu ma JF members wengi wapo D'salaam

Muhindi unachomwa haubanikwi njoo ule muhindi halisi kwa pilipili mswaki upate ladha tofauti


KARIBUNI
 
Back
Top Bottom