Llio 002
JF-Expert Member
- Jul 14, 2015
- 1,639
- 2,086
Wote tunafahamu lengo la ndoa ni kuishi milele, ila kutengana kupo na kumethibitishwa na vitabu vyetu tukufu ila huja kwa dharura zake. Wengi wanapotengana hutengeneza chuki, kudharauliana na pia kutosikilizana, jambo linalopelekea kutoweka kwa amani, upendo na mshikamano kwa wanatalaka hao.
Ugomvi wao unapelekea watoto kukosa malezi ya upande mmoja, kama sio baba, basi watayakosa ya mama, huku kila mmoja akimuombea mwenza apate pigo (afilisike) ili ithibitike kuwa yeye ni mtu muhimu kwake.
Hatuna haja ya kuombeana mabaya pale tunapotengana, hatuna haja ya kuwatelekeza watoto kisa tumetawaliwa na hisia za kishetani, badala yake tuombeana kheri na tulee watoto wetu vizuri na kwa pamoja. Tushirikiane kwenye mambo yote ya kheri.