Maisha baada ya kifo

تَبَارَكَ الَّذِي بِيَدِهِ الْمُلْكُ وَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ​

الَّذِي خَلَقَ الْمَوْتَ وَالْحَيَاةَ لِيَبْلُوَكُمْ أَيُّكُمْ أَحْسَنُ عَمَلًا ۚ وَهُوَ الْعَزِيزُ الْغَفُورُ​

hilo ndilo jibu...
 
sio wote wanaojua lugha ulioitumia
 
ni kweli
google imerahsisha sana
ni kweli mkuu imelahisisha kwa wale ambao hawaelewani lugha katika kuwasiliana ,,sasa wewe unaelewa kiswahili na mimi naelewa kiswahili kwanini usitumie kiswhili
 
1.Kwanza ufahamu dini imeanza zamani mno kutoka kwa Adam mpaka watu wa sasa na mitume karibuni laki moja na ushei imekuja duniani kuhubiri ni jinsi gani mungu anahitaji viumbe wake waishi hapa duniani lakini pia na kuwapa elimu tosha juu ya maisha yao ya sasa na baada ya kifo. Lakini inasemekana kutakuwa na vizazi ambavyo havikupata ujumbe wa mungu kwasababu mbali mbali hawa wanahukumu zinazoendana na ujuzi wao maana mungu hawezi kumhukumu kiumbe chake katika hali ya ujinga. Mkuu mimi ni mwislam, moja katika mafunzo niliyowahi kufunzwa katika dini ni kwamba. Unapofanya baya moja yaani dhambi linachukuliwa moja kama lilivyo, kama ulikuwa na nia ya kufanya baya lakini kutokana na sababu mbali mbali hukufanikisha haliandikwi kabisa yaani halina hukumu. Na kama ukifanya jema moja inachukuliwa kama umefanya mara 10 katika hesabu na kama ulikuwa na nia kufanya jema lakini kutokana na sababu mbali mbali hukufanikisha unaandikiwa kama umefanya mara moja.

2. Mkuu, nakusahihisha kidogo sio kwanini kuwepo na hukumu? bali kwanini kuwepo na hesabu kwasababu hukumu ni adhabu au salama kuenda motoni au peponi. Mungu wetu amesema katika maandiko kwamba yeye ni hakimu muadilifu, sasa asipoleta hiyo siku ya hukumu si itakuwa sio sawa. Hata wewe, iwe umekaa pahala umetulia halafu aje mtu akupige ngumi bila ya sababu yoyote si lazima utamrudishia halafu utasema kwanini umenipiga? Lazima utahitaji kufahamu kosa lako ni lipi? Sasa na Yeye huyo mungu anahitaji kumpa mtu hesabu yake ili afahamu mwenyewe kwanini ameingia kwenye moto au mbinguni na watu wengine wapate kushuhudia. Na wale walio kuwa wakipinga huku duniani kama hakuna hesabu wala mungu wamuone huyo mungu mwenye akiwalipa. Kuwepo hesabu haina maana mungu hafahamu yupi ataenda motoni na yupi haendi. Na ndio mjuzi zaidi
 
Inakuaje Mungu awe ni mmoja alaf hajulikani yupi ni wa kweli!
Mkuu issue ni Perspective juu ya MUNGU, tatizo liko kwetu, ukiangalia kwenye hizo dini ulizotaja kuna sehemu wanaamii pamoja, ila kuna sehemu mtazamo unatofautiana. kwa kigezo hicho tu kinatosha kusema ni perspective yetu ndio ina shida mahali.
Ieleweke kwamba huu ni mtazamo wangu binafsi, na sio fact nimeongea kwa Mwanga na uelewa kidogo nilio nao, hivyo i accept the different na mtu mwenye mtazamo tofauti na wangu.
 
Wahindi, wachina, wajapani, burma, sri lanka, mongolia
Mkuu most of Dini zinahimiza Upendo kwa watu wote, Kumbuka ukimpenda unayemuona basi Mungu automatically ndio kumpenda Mungu. Hakuna Dini isiyohimiza Upendo ndugu ( nazungumzia mlengo wa dini, sizungumzii Mtu au kikundi cha watu ambao wao wameamua kutokuwapenda watu/ kuua etc)

Kwenye vitabu vingine wamesema Dini safi ndio hii, kuwasaidia Wajane na yatima katika shida yao.
Lakini pia Mahalai pengine wakasema Amri iliyokuu ni Kumpenda Mungu kwa moyo wote, roho yote na Akili yote, lakini pia Mpende jirani yako kama nafsi yako.

Of which katika haya mambo utafahamu kuwa Upendo ndo kitu pekee kinaunganisha watu, Budhist,Shinto,Judaism, Christians, Muslim etc etc.

Ndo maana Utasikia, Makundi tofauti ya watu wanatoa Misaada ya kusaidia wagonjwa, yatima wajane hiyo ni ibada tosha kwa Mungu, kwa kadiri ninavyoamini mimi.
 
Hili ndilo nilitaka kulisema.
UPENDO tu.
Mitafaruku ya ulimwengu sababu ni ukosefu wa UPENDO wa kweli.
 
You are precisely accurate, altogether we go there .
 
Sasa utaabudu vipi masanamu.wakati hayana pepo wala moto?
Wakutoa hukumu ni mmoja tu nae ni mungu mwenyewe.
Mungu amesema ametuunba ili tuje tumuabudu.
Sio kuabudu masanamu
Masanamu yanawalipa uoni nchi kama China au Japan zilivyopiga hatua kimaendeleo , kwanini waangaike na Allah ambaye wafuasi wake wanalipuana mabomu ?
 
Jibu tamu sana kuliko hata mistari ya kukariri
 
Kawadanganya nani kuna maisha baada ya kifo ?
Tafuteni pesa km mimi navyoteketeza mamilioni kila siku kwa kujirusha viwanja vyenye watoto wakali
Watu wa namna yako ukiwafuatilia unakuta ni mwenyekiti wa jumuiya ndogo ndogo za kikristu
 
This is a well explanation of pure famous heresy in christistian history so called GNOSTICISM, hawa hawakuoa wala kula nyama
 
Maendeleo ni AKILI ZAO.
si sababu ya kuabudu masanamuu
Masanamu yanawalipa uoni nchi kama China au Japan zilivyopiga hatua kimaendeleo , kwanini waangaike na Allah ambaye wafuasi wake wanalipuana mabomu ?
 
Wanadamu wanatumia ujanja ujanja kuwaaminisha watu ili wasiogope kifo.Kifo kipo na ukishakufa ndio mwisho wako,hakuna kwenda motoni wala peponi hizo zote ni kufarijiana. Swali la kujiuliza kuku,samaki n.k unavyowaua na kuwala huwa wanaenda wapi? jibu utakalopata hata binadamu ni hivyo hivyo.
 

Umeuliza maswali sahihi, lakini sehemu yenyewe ndio chaka! Tafuta mtu serious ujadili naye heart to heart kama lengo ni kupata majibu. Hapa utaishia kuwa confused...

My gentleman advice!
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…