MaxShimba
Platinum Member
- Apr 11, 2008
- 36,008
- 4,092
Na Anneth Kagenda na Simon Mhina
Kamati ya Maimamu ya kuokoa mali za Waislamu imetishia kusoma dua ya Ahla-badri kuwashitakia kwa Mwenyezi Mungu, watu wote waliohusika kuwadhulumu Waislam kiwanja chao kilichoko Chang'ombe, Dar es Salaam.
Sambamba na hatua hiyo, Waislamu hao wamesema watafanya maandamano ya siku mbili yatakayohitimishwa na kongamano kubwa katika viwanja vya Jangwani, kwa lengo la kumshinikiza Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya makazi, Bw. John Magufuli ajiuzulu.
Maandamano ya kwanza yatafanyika Septemba 7 na ya pili Septemba 17, wakati wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Akitangaza mkakati huo kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika kwenye Msikiti wa Mtoro, jijini Dar Salaam jana, Katibu wa kamati hiyo, Sheikh Khalifa Khamis, alisema wanaamini Mwenyezi Mungu atawaongoza vyema hadi kufanikisha kurejesha kiwanja chao.
``Tarehe 17 Septemba, wakati wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani tutaitisha mhadhara kwenye viwanja vya Jangwani na kusoma dua ya Ahla-Badri kumshitakia Mwenyezi Mungu juu ya dhuluma hii kwa Waislam na kumtaka Magufuli ajiuzulu,`` alisema.
"Kamati inamtaka Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Bw. John Magufuli, ajiuzulu kwa kuwa aliwahadaa Waislamu na kushindwa kuwarejeshea kiwanja na kufuta hati ya umiliki aliyopewa mfanyabiashara Bw. Yusufu Manji," alisema.
Alifafanua kuwa Waziri Magufuli alimuahidi Mufti wa Tanzania, Sheikh Issa Simba, mbele ya Halmashauri Kuu ya BAKWATA kwamba serikali itakirejesha kiwanja hicho kwa Waislam wakati ambao Bw. Manji alikuwa ameshakabidhiwa hati ya ardhi hiyo huku akiwa hajalipa pesa.
Akisimulia kwa ufupi kuhusu sakata hilo, Sheikh Khalifa alisema kuwa Februari 26 mwaka jana kamati yao ilikutana na waandishi wa habari na kutoa taarifa kwamba kiwanja namba 311/1 kitalu `T` kilichopo Changombe jijini kimeuzwa isivyo halali na baadhi ya watumishi wasio waaminifu wa BAKWATA kwa mfanyabiashara Manji.
Alisema baada ya kutolewa kwa tamko hilo, Mufti wa Tanzania Sheikh Issa Simba, aliunda tume ya kudumu ya kuchunguza na kutoa ripoti kwa kipindi cha wiki tatu, namna kiwanja hicho ambacho ni wakfu, kilivyouzwa.
Machi 29 mwaka jana Sheikh Simba alikubali mapendekezo ya tume na kuwafukuza katika uongozi wa BAKWATA maofisa saba wa ngazi za juu waliobainika kuwa walikula njama kwa kutumia hati za kughushi na kukiuza kiwanja cha wasilamu kwa Bw. Manji.
Alisema Kamati hiyo ya Maimamu ilimwandikia barua Waziri Magufuli na kumwomba akirudishe kwa Waislamu kwa vile serikali ya awamu ya kwanza ilikitoa ili kijengwe chuo kikuu cha Waislamu.
Aliendelea kusema kuwa Mufti aliwaongoza wajumbe wa Halmashauri Kuu ya BAKWATA wanaowakilisha Waislamu mikoa yote Tanzania na kumwambia Bw. Magufuli kuwa msimamo wao ni kuitaka serikali ikirejeshe kiwanja hicho.
Alisema walitoa maelezo hayo baada ya Waziri kuitaka halmashauri hiyo ya Waislam kutoa msimamo wake juu ya umiliki wa kiwanja hicho.
Alisema baada ya kimya cha muda mrefu kamati ilipata taarifa kuwa serikali imekataa kuifuta hati aliyopewa Bw. Manji na badala yake, mfanyabiashara huyo aliweka Sh. milioni 86.7 katika akaunti ya Waisilam.
Aidha kamati ilimpa Bw. Manji muda wa siku 20 kuamua kwa hiari kukirejesha kiwanja hicho kwa Waislamu naye akaahidi kuwa atakuwa tayari kufanya mazungumzo na kamati kwa nia ya kupata suluhisho juu ya mzozo huo.
Kwa mara nyingine, Sheikh Khalifa alimuomba Rais Jakaya Kikwete kuingilia kati sakata hilo ili kurejesha hati ya kiwanji hicho mikononi mwao na kutaka serikali kuheshimu masuala yanayohusu imani za raia.
SOURCE: Nipashe