Tumeongea sana na kujadiliana hata siku ya kutambulishana rasmi.
Kila ninapomshauri juu ya kutoka kwao anasingizia hajamaliza maandalizi ya kuhamia kwake. Hii story ya maandalizi ya kuhamia inaenda mwaka sasa. Kila siku hana pesa kwamba anaandaa mazingira.
Naomba nikukumbushe tu kitu kimoja, umri wako sasa ni 40+ sio 30+ uliyoweka hapo…. tumeumbiwa kusahau hivyo tunakumbushana.
Una miaka 41 to be precise.
View attachment 2095014
Mpalestina katika ubora wako.......kwani wewe unavyo jisifia hivo na kujiweka hiyo class katika hayo mahusiano unaongeza Nini Cha ziada ....? Kuna ulazima gani wa kuwa na wewe.....? Lipi ambalo lipo kwako kwa wengine hamna .....? .....for sure hao wanaume wasio na akili unawaendesha Kama makatapila ndio levo zakoAiseee haya mapenzi mimi mbona sina? Yaani amekugeuza chuma ulete wewe ndo mtoa pesa? Uko nae miaka 9? Wewe umerogwa sio bure, mpuuzi anaishi kwao miaka hiyo yote?
Kweli kuna wanawake mnapenda kiboya sana.mimi mwanaume ambae hatowi chochote kwangu siwezi mvumilia zaidi ya miezi 3.
Amka usingizini, huyo fala anakuona wewe ndo una shida sana wewe ndo unamuhitaji kuliko yeye snavyokuhitaji.
Manina zake nyau huyo.mpigie simu mwambie aje muongee, akifika uwe umeshaandaa nguo zake mkabidhi funga mlango.
Au muulize alipo akisema yupo nyumbani mwambie unakuja kumuona, nenda na mizigo yake yote.
Ikiwezekana hama huo mtaa, mwambie vitu vyake umeviacha ndani akavifate, kha yaani nimesikia hasira sana huu upuuzi siwezi ufanya.
Mpuuzi huyo ana nini cha maana kinachokufanya uendelee kuwa mtumishi wake?
Mwanaume wa hivyo awe wa mwisho kwako, umepoteza muda mwingi sana.sasa amka usingizini.
Ukipata mwingine, hakikisha usimfiche ualisia wako muoneshe mwanzoni kuwa anatakiwa kuwajibika kwako kama mwanaume.lazima atowe pesa kwa ajili yako.
Tangu niwajuwe wanaume walivyo wapuuzi siteswi na mapenzi, zamani nilikuwa nawaza atanionaje nikimwambia mambo ya pesa?niliteseka sana
Nikawaza hawa ni wa kuwambia indirectly.
Kuna mmoja huyoanataka kunipandisha nyeunge niende kwake ahaaaaa nimenyoosha maelezo, nikamwambia mimi sipandi basi masaa 13 nimekalisha tako kwenye basi kukufata, nikamwambia nasubiri tiketi ya ndege asipotuma kwangu nakula nakusaza. Na ataituma asipotuma sina cha kupoteza kwake.
Inabidi nimzoeshe hivyo asije niona mimi ni wa kusafiri na nyeunge kha. Mtu uwezo anao afu nijitese? Nyooolooo zake
Dada leo hii hakikisha huyo tegemezi anaondoka kwako mwambie umepata mwanaume mwingine. Ishiiiiiy



ILA MSHIKAJI ANAZINGUA😂😂😂😂😂😂 vijana wa siku hizi wanapenda mtelemko zaidi ya sisi wa kike.
Habari humu ndani?
Kwa kweli ashukuriwe sana alieanzisha JF
Maana kuna muda unatamani kuongea you dont know mtu wa kukusikiliza. Ila JF inasaidia sana kufanya wengine tutoe yanayotuumiza mioyoni mwetu.
Ipo hivi, nimekua kwenye mahusiano kwa muda mrefu sana zaidi ya miaka 9 na huyu mwenzangu. Tulianza mahusiano tukiwa chuo kikuu. By the time tumeanza mahusiano, sikuwahi kufikiria ndoa. Ingawa mwenzangu alinitamkia mara kadhaa ingawa sina hakika kama ni hali ya utani ama la.
Sasa tumekua watu wazima 30+. Kila mtu ana kazi yake, mi mdada nimepanga kwangu na mwenzangu anaishi kwao bado. Kiukweli maisha ambayo tulikua tunayaishi sikuyapenda. Kila mara mwenzangu anatoka kwao kuja kwangu. Ingawa mimi nina kipato kikubwa sana zaidi ya mwenzangu, lakini bado mimi ni mwanamke ninayehitaji mapenzi ya mwanaume. Lakini mwenzangu amekua kama mtoto kwangu. Anakuja nyumbani kwangu, kila kitu nafanya mimi. Na bado kuna muda ananiomba nimnunulie zawadi.
Kiukweli nilikaa naye chini nikamueleza. Binafsi kupata pesa nyingi zaidi yake sikuona kama ni kikwazo. Nilichohitaji ni kufanya vitu vya kimaendeleo zaidi kuliko starehe. Ila mwenzangu utasikia "Naenda kwenye mpira sasa utanitumia nipate japo mbili tatu?" Kiukweli hali hii ilinifanya nipunguze sana mapenzi kwake. Mwenzangu akaanza wivu labda nina mtu.
Kiukweli, nimejaribu kuongea naye mara kadhaa. Mwenzangu hata mpango wa kujiinua yeye kama yeye hataki. Na sasa nimegundua kwamba wamerudiana na ex wake. Nilichokifanya sikumwambia lakini nilimuomba same day same time, kila mtu afanye maisha yake. Amejaribu kunibembeleza lakini sioni cha maana anachokiongea.
Kuna baadhi ya mali zake ambazo zipo kwangu, nimeshamuomba mara kadhaa azichukue na hataki. Nikimwambia kuwa nazigawa anasema atatuma mtu azifate. Ikifika siku ya kuzifata hata nimwambie mtu anamletea, hajibu chochote.
Nimeamua kuondoka kwenye maisha yake. Sioni future wala sioni akibadilika. Ila l feel bad. Though najua kuèndelea kumganda mtu wa namna hii, itanifanya mimi nisipige hatua ya maisha.
This is what l wanted to share with you JF family.
Kama jamaa amezingua kiasi hicho piga chini,tena mapema sana ucipoteze mdaHivi mkuu umewahi kukutana na mwanamke ambaye anakuthamini na ukiwa mkweli mkafanya maisha pamoja? Ni mimi. Ila mwanaume sawa anapokea kidogo basi kwa hicho kidogo chako nunua hata unga. Hakuna. Vocha ya buku nilimuomba tangu hatujakorofishana hadi sasa haijafika. Kweli hayo mahusiano upo na mwanaume?
Akipata shida ni mimi wa kwanza kunishirikisha. Akipata shida hakuna anayemsikiliza zaidi yangu. Lakini yeye anataka nimthamini mimi nikiwa na shida wala hana habari. Kuna siku nimeumwa mafua akagoma kuniletea chakula. Do you think naondoka sababu ya pesa mkuu?
Dm pleaseHabari humu ndani?
Kwa kweli ashukuriwe sana alieanzisha JF
Maana kuna muda unatamani kuongea you dont know mtu wa kukusikiliza. Ila JF inasaidia sana kufanya wengine tutoe yanayotuumiza mioyoni mwetu.
Ipo hivi, nimekua kwenye mahusiano kwa muda mrefu sana zaidi ya miaka 9 na huyu mwenzangu. Tulianza mahusiano tukiwa chuo kikuu. By the time

Wanawake wengi wanashindwa kuwa independent ila wewe umeweza na hongera kwa ilo,sio kila kitu mwanaume sometimes men tunakuwa na madhambi sana kwa wanawake ila kama upo free from stress ni vizuri sana kulinda afya ya akili ucje jiua kisa mwanaume.Tushaumizwa zaidi sasa hivi hatuogopi kitu.nilikuwa dada mwenye upendo sana siombi hata mia nasubiri nipewe sipewi kumbe wengine wanapewa nilivyotendwa nikaamka usingizini.
Sasa hivi ni mwendo wa usipotoa endelea na maisha yako. Nimenene, nimenawili sina stres mungu anipe nini?
Mapenzi ni utumwa sometimes.
Nb sitaji kuwa nataka hela, nakujengea mazingira unaitoa kwa kujiongeza usipojiongeza mimi nakaa kimya mpaka utakapojiongeza.
Short& clearNI ngumu mwanamke kumlea mwanaume asiyekuwa na kazi.


Ila huyo anaye mzungumzia huyo mwanamke anakosa ule uanaume.Umekimbia mwanaume ambaye Hana akili ya maisha lakini ana mapenzi, unakutana na mwanume mwenye akili ya maisha lakini ni hit and run, Hana muda na wanawake Wala mapenzi ......
Huwezi pata mwanaume mkamilifu hii dunia ...
Unachofanya unakimbia tatizo tu ,![]()