ERoni
JF-Expert Member
- Jan 9, 2013
- 55,610
- 131,053
...2009 ukiwa binti mdogo tu, miaka 24 ukaamua kuishi kimahusiano na mtu alokuzidi 14 good years, sina uhakika kama uliamua kuwa huyo angekuwa mumeo. Naamini kwa vile ulitoka humble beginning uliamua kuwa nae ili akukwamue kiuchumi...mwisho wake uaingia kwenye mahaba niue.Anyway ilikuwa mwaka 2009 nikiwa nina mwaka mmoja after ku graduate degree ya Ualimu. Nilipokutana na kaka/baba mmoja mwenye miaka 38 mimi nikiwa na 24.
Kumbe yeye yupo kwenye ndoa kwa miaka 4.
Bahati nzuri alinikuta nikiwa najitegemea (Nimepanga chumba kimoja ) kama watoto wa kimaskini wengi tunavyoanza maisha. Hivyo alinikuta nikiwa nimejitosheleza kwa kidogo nilichokuwa nacho.
Bahati Bahati nzuri nimetokea kwenye familia ya single mama hivyo. Nilijifunza kuwa mchakarikaji tangu kipindi nilipokuwa nasoma. For now ninabiashara zangu mjini hapa Dodoma (yeye akiwa msaada mkubwa sana kwa mimi kufika hapa nilipo)
shule naenda hivyo hivyo kwa kusua sua. (Walimu watanielewa hapa).
Alinikuta nikiwa single kwani mi masuala ya mapenzi nilikuwa sihangaiki nayo (inawezekana ni kwasababu nimetokea familia isiyokuwa na baba)Hivyo for the first time nikaingia kwenye mapenzi seriously. Sikujua kama jamaa ameoa kwani nilikuwa naenda hadi kwake nakaa hata siku nyingi kidogo japo sijawahi kuhamia. KUMBE AMEOA NA FAMILIA(mke na mtoto mmoja) YAKE IPO HAPAHAPA MJINI. Hiyo nyumba aliijenga kwa siri (sijui kwanini ). Eli79 hapa huoni kuwa kuna serious problem kati ya huyu mume na mkewe? Halafu nimkute ana jichetua huko atanijua mi ni nani!
Baadae sana 2011 alivyojua penzi limekolea akaniambia kuwa ye ameoa lakini anataka mi niwe nyumba ndogo (sio siri I cried). Sikuamini kama ni kweli mpaka siku nilipothibitisha na nilimtaka tuachane japo haikutokea.
now tuna kama mwaka wa 6/7 And we are happy.
(Sisemi hatukwazani) changamoto zipo kwani sisi hatuishi mbinguni! Ugomvi wa kila siku ni ndoa ya serikalini. Mi sikupanga kuolewa maishani (May be the past eats the future)
Kuhusu mafanikio ya kukaa nae (economically) ni makubwa mno ukizingatia mimi ni mtu wa kazi siku zote. Nina vingi nilivokuwa naviota (sijui kama ni vyote).
Sioni kama kuna kitu mkewe ananizidi kwani yawezekana ninamzidi hata ada ya mwanaye anayesoma Martini Luther huwa inapita kwangu.
Kuhusu ugomvi na mkewe alishawahi kunichokonoa sana sema mi niko bize hawezi nipata. Ninaishi and am happy.
Sasa hapa Eli79 je ni kweli wote wanaotembea na waume za watu ni wawindaji?
Sijaandika mengi sana ikiwemo na kuitwa kwenye vikao daah!
...Sasa una 30yrs bado umefungwa kwenye kamba za huyo mume wa mtu, sidhani kama kuna kingine waweza ku claim zaidi ya ku play innocent girl. Amani ya mwanamke mwenzako umeichukua, yeye amebaki kuwa mshika pembe, lakini in a long run, utabaki kushika pembe, tena kwenye umri ambao utakuwa unahitaji mwenza zaidi ya sasa..
..Mna watoto?