Mahusiano na mume wa mtu ni shughuli pevu

Mahusiano na mume wa mtu ni shughuli pevu

Mwana jukwaa uitwaye "malaika mimi" naomba nikupongeze kwa mada yako nzuri inayoelimisha na kuzindua! Pamoja na kwamba kuna post zingine zililenga kufurahisha genge, lakini somo limeingia kuwa mwisho wa siku iwe Leo au kesho, huwezi kufaidika kwa kuishi na mume wa MTU! Ni kuishi na Bomu!
 
Tafadhali usiibe! Hakuna sababu hata kidogo ya kufanya hivyo! Si Mungu atakupa wa kwako peke yako! Nguvu zake zooote zitaishia kwako! Usipoiba hutaibiwa! Inawezekana! Halafu ukisubiri wa kwako mapenzi yake matamu sana hakuna mfano! Hakuna raha duniani kama kuishi na mume/mke kwa uaminifu!

Bora usaidie kutoa somo...
Maana mimi nimeshaonekana nina conflict of interest...
Nikiandika lazima wapinge...

Wanapretend to be happy...
Unless wasiwe binadamu wa kawaida lazima dhamira zao zinawasuta....

Mfano huyu dada ameonyesha hana interest ya kufuatilia kwa undani maisha ya huyo mume alokimbia familia....jiulize why? kama si kujilipua...liwalo na liwe...akirudi kwa mkewe aende...is this normal? Is this love?
 
Darln nimejitahidi kuongea frankly kadri nilivyoweza. Binafsi huwa sina cha kupoteza kwasababu mwanaume kwangu ni emergency.

Inawezekana alichowahi kukifanya aliyeitwa babaangu ndicho kinachonitafuna hadi keshokutwa. Japo kwa sasa nahisi kufurahia mahusiano.

Bado nina tatizo na wanaume ndio maana huwa nawaambia kabisa sana jitahidini kutulia kwa wake zenu, wanaatjiri sana watoto wao, maana kuna manyang'au yakiwadaka nje huwa wanapoteza vitu vingi sana.

Mwanaume haibiwi kwa kuwa sote tunajua wanaume hawabakwi kwa hiyo ni wao ndio ambao huwa wanaamua kuibiwa![/QUOT

Nimesoma post zako humu, kwa dhati kabisa nakupongeza kwa kuwa wazi! Kwa dhati pia nakupa pole kwa sababu umekuwa mhanga wa mazingira! Siwezi kuthubutu kukulaumu japo ni kweli kuwa unachoendelea nacho si sahihi.

Ila ninachoweza kukushauri ni kuwa angalia uwezekano wa kutengeneza maisha yako. Unasema kuwa una furaha, hiyo ni dalili ya kwanza ya tatizo lako. Huwezi kuwa na furaha na amani katika hali uliyonayo hata kama ukionekana kuwa una kila kitu na moyo wako ni shahidi katika hili. Unasema una furaha kama njia ya Ku suppress hisia kuwa kuna watu hawana tatizo kama lako, hivyo unataka uonekane kuwa uko sawa tu na wengine wakati siyo! Ndio maana unasema kuwa hata mke wake hakuzidi kitu! Hapana , anakuzidi yeye anakula kwa amani iliyo haki yake, wakati wewe unapokonya haki ya mwingine! Dhamiri yako lazima itakusuta!

Ushauri wangu kwako, you are still young! Mwambie Huyo mchepuko wako , siwezi kuendelea kuiumiza dhamiri yangu kwa kuishi na mume wa MTU! Lawama zote ni za huyo bwana lakini msamehe!

Mwombe Mungu akusamehe na akuokoe! Anza maisha mapya, vinginevyo kuna siku Mungu atasikia kilio cha huyo mama mwenye mume, huwezi jua Mungu atafanyaje? Afadhali uamue mapema wakati bado kijana, Mungu atakupa mume maana ni haki yako, mwamini Mungu!

Na kama akila kwa Amani does it concerns to me? Nijitahidi kutengeneza Maisha yangu how? We unafikiri maisha yangu ni yapi? Unayoishi wewe yanaweza kuwa maisha yangu kweli? Teh teh
Kama kipimo cha mi kuwa sawa ni kuwa na ndoa Basi inawezekana kweli sipo sawa kama sivyo basi niko sawa.

Anyway hili somo hebu lianze kwa waume zenu.
 
Mwana jukwaa uitwaye "malaika mimi" naomba nikupongeze kwa mada yako nzuri inayoelimisha na kuzindua! Pamoja na kwamba kuna post zingine zililenga kufurahisha genge, lakini somo limeingia kuwa mwisho wa siku iwe Leo au kesho, huwezi kufaidika kwa kuishi na mume wa MTU! Ni kuishi na Bomu!

Kufaidika ni kufanyaje? Samahani lakini. Unajua kufaidika ni subjective term.
 
Bora usaidie kutoa somo...
Maana mimi nimeshaonekana nina conflict of interest...
Nikiandika lazima wapinge...

Wanapretend to be happy...
Unless wasiwe binadamu wa kawaida lazima dhamira zao zinawasuta....

Mfano huyu dada ameonyesha hana interest ya kufuatilia kwa undani maisha ya huyo mume alokimbia familia....jiulize why? kama si kujilipua...liwalo na liwe...akirudi kwa mkewe aende...is this normal? Is this love?

Good morning, naona umepata wa kukusaidia lets go. ... Wengine wamebanwa na majukumu.
 
Ni malaika sampuli ipi? Unataka mume wa mtu, kwa nini usiwe na wa kwako? Mbona ukimwomba Mungu atakupa! yuko wa kwako peke yako! msubiri!

We na wewe umekurupuka, fuatilia kwanza huyo niliye mjibu hivyo alinambia nini hadi nikamwambia hivyo. Halafu umechelewa hujui kitu ilikotoka unaquote quote tu kiholela usiku wa manane.
 
Ujue kuna kitu sijakielewa hapa, na ninadhani na nyinyi wanawake hamkielewi! Kukaa na mumeo kwenye nyumba nzuri na watoto hapo hapo wakati akitaka kutuliza moyo, mtu wa kucheka naye, mtu wa kumpa furaha si wewe mke wake ni mchepuko ina maana gani? Mchepuko hasikudanganye mtu, ata kama nimeupangia nyumba vichani but mi mwenyewe napata raha huko si mbaya!
Mnasema eti anautumia mchepuko, si kweli! Kama mchepuko unaupenda, unaupenda kuliko hata mke wa nyumbani! Then nikwambie kitu, kama umeolewa utaniambia, ata kwenye swala la mapenzi mchepuko unafaidi kuliko mke wa nyumban! Utajitupa kwenye romance, kunyonya hapa na pale, lakini ukirud nyumbani unatimiza wajibu, round moja inatosha!

Sasa unapoudumiwa si kwamba wewe ni bora kuliko mchepuko ila jamaa anawaudumia wanawe, so nawe unaponea hapo hapo! Kwa hiyo unakuwa kama house girl na estate manager, si mpenzi, mtu wa kwanza kufikiriwa akiwa na amu ya mapenzi! We michepuko unaijua au unaisikia? Inategemea na mchepuko lakini, lakini kuna mingine safi sana na haiendekezi kuongwa, ukiwa nacho unampa, kama huna anakuelewa! In short mchepuko nao unapenda tu kama wewe unavyopenda, na si kweli kuwa michepuko hipo kimaslahi!

Na ambaye hana watoto?
 
Na kama akila kwa Amani does it concerns to me? Nijitahidi kutengeneza Maisha yangu how? We unafikiri maisha yangu ni yapi? Unayoishi wewe yanaweza kuwa maisha yangu kweli? Teh teh
Kama kipimo cha mi kuwa sawa ni kuwa na ndoa Basi inawezekana kweli sipo sawa kama sivyo basi niko sawa.

Anyway hili somo hebu lianze kwa waume zenu.

Ouw ouw ouw! bintikiziwi loh salaaahle! somo lianze wapi tenaaa?
Me naona kama lianze kwao wenyewe kwa wenyewe hiviii .. kwa nini mumeo achepuke? huoni kuna shida hapo? Kama wewe uko sawa na bado anachepuka ni umajinuni wa mumeo! hata asipochepuka na mimi atachepuka kwingine na tukisema michepuko wagome waanze wote kudai kua na waume zao ndio umekwisha mana mumeo akili mbili ambaye kwake kuchepuka ni dini ya pili ataenda kwa makahaba mfe mapema bora atulizane na mchepuko ulioamua kutulizana nae!
 
Last edited by a moderator:

Hahahaaa mi sipo! Kuna sehemu inabidi tuanze kupajenga. Kuanzia kwa mke, mume halafu kwa mchepuko. Kwanini mtu achepuke? Hili ni la kwanza, hapa utasikia wanawake wanavyoleta excuses eti ohhhh mwanaume wangu mdhaifu ametegwa kidogo tu hahahha mi huwa nawasikiliza naishia kusikitika tu.
 
Ategwe amekua nguruwe pori! wanajitoa fahamu tu tena na uongo juuu sina mke! haya sasa na kukanwa wanakanwa
 
Katikanpitapita zangu nikakutana na hii......

Waume za watu wanawindwaaaaa

Sema.mijanaume yenyewe haijitambui
 
Attachments

  • 1437648259396.jpg
    1437648259396.jpg
    77.4 KB · Views: 268
Bora usaidie kutoa somo...
Maana mimi nimeshaonekana nina conflict of interest...
Nikiandika lazima wapinge...

Wanapretend to be happy...
Unless wasiwe binadamu wa kawaida lazima dhamira zao zinawasuta....

Mfano huyu dada ameonyesha hana interest ya kufuatilia kwa undani maisha ya huyo mume alokimbia familia....jiulize why? kama si kujilipua...liwalo na liwe...akirudi kwa mkewe aende...is this normal? Is this love?

You have said it all hun.
Lazima uonekane una conflict of interest simply sababu ukweli wanaujua na hawapendi kuusikia. You can't be that cold afu upritend you are happy. Huwezi kufurahia maisha ambayo ndani ya nafsi yako ukijitafakari unajiona mjinga. Wakati mwingine tuupende ukweli maana unatuweka huru.
 
Kweli kabisa mkuu inategemea

Mi kuna ninaowafahamu wanafaidi kuliko hata nyumba kubwa

Kuna faida gani kubwa zaidi ya kuupata moyo wake? What is the use ikiwa all he keep thinking is his wife and children??.

Unless you have just agreed to pass on time...
 
Back
Top Bottom